Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid akimshukuru Mkurugenzi wa
kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical inayojishughulisha na
masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha
upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati
Nyamwage kata ya Mbwala hivi karibuni.
Baadhi
ya akina mama wakimshukuru Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif
Rashid kwa kuwapatia vifaa tiba kuwalinda na kuimarisha afya ya mama na
motto.
(Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid akiongea na wananchi wa kata
ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Juma Ligomba hivi karibuni kabla
ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakavyotumika katika zahanati
mbalimbali wilayani humo.
Diwani
wa kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Juma Ligomba
akimkaribisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid kuongea
na wananchi wa kata hiyo hivi karibuni kabla ya kukabidhi vifaa tiba
ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid (kushoto) akiteta jambo na
diwani wa kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Juma Ligomba
(kulia) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo
vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo. Wa kwanza
kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical
inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia ambayo
imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba
vilivyokabidhiwa katika zahanati Nyamwage kata ya Mbwala hivi karibuni.
Wananchi
wa kijiji cha Nyamwage kata ya Mbwala wilayani Rufiji mkoa wa Pwani
wakimkasikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid hivi
karibuni kabla ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitakavyotumika katika
zahanati mbalimbali wilayani humo.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid (aliyevaa shati la batiki)
akishirikiana na wananchi wa kijiji cha Nyamwage kata ya Mbwala wilayani
Rufiji mkoa wa Pwani kufungua kitanda kwa ajili ya akinamama
kujifungulia hivi karibuni wakati anakabidhi vifaa tiba kwa ajili ya
wilaya hiyo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical
and Pharmaceutical inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba Peter
Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya
vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati Nyamwage kata ya Mbwala hivi
karibuni
…………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid amekabidhi
vifaa tiba vyenye thamani ya sh milioni 23.8 ambavyo vitakavyotumika
katika zahanati mbalimbali wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na kitanda kimoja kwa ajili ya
akina mama kujifungulia chenye thamani ya sh. Milioni 1.5, vitanda 50 na
magodoro manne.
Makabidhiano hayo ya vifaa hivyo yalifanyika mwishoni mwa wiki
katika zahanati ya Nyamwage iliyopo kata ya Mbwala wilayani Rufiji huku
yakishudiwa na wananchi wa eneo hilo wakiwa mashuhuda wa makabidhiano
hayo.
Akikabidhi vifaa hivyo, Dkt. Seif aliwaasa wananchi wanaotumia
zahanati hiyo kuvitumia na kuvitunza vizuri vifaa hivyo ili kupunguza
tatizo la akina mama wajawazito kupata adha wakati wa kujifungua na
wagonjwa wengine wanakaopata huduma katika zahanati hiyo.
Dkt. Seif alisema kuwa vifaa hivyo vinatokana na moyo wa
wanarufiji waishio jijini Dar es salaam na marafiki wa Rufiji ambao
wameanzisha mfuko wa Maendeleo wa Wanarufiji unaolenga kuinua maisha ya
wananchi wa wilaya hiyo katika kusimamia upatikanaji wa huduma za jamii
ikiwemo afya, umeme, upatikanaji wa maji safi na salama, elimu, kilimo,
biashara na ardhi.
Kuhusu suala la umeme, Dkt. Seif alisema kuwa mpaka sasa wilaya
ya Rufiji vipo vijiji 39 ambavyo tayari vimeunganishiwa huduma hiyo
ambapo taendelea kusaidia kuboresha vitu vingi akitolea mfano Nyamwage
ilivobadilika na kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi.
Na kwa upande wa huduma ya maji kwa wananchi wa Rufiji, Dkt.
Seif alisema kuwa kamati ya mfumko wa maendeleo Rufiji kwa kushirikiana
na marafiki wa Rufiji watachima visima zaidi ya 25 katika vijiji
mbalimbali ili kuwapunguzia wananchi adha ya upatikanaji salama na
kutumia muda mwingi katika shughuli za kiuchumi waweze kujiletea
maendeleo yao kwa kushirikiana na Serikali.
Dkt. Seif alibainisha kuwa umoja wa wanarujiji hao walifanya
harambee mwaka jana jijini Dar es salaam iliyoongozwa na Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano Mhe Dkt. Mohamed Gharib Bilal ambapo zilipatika
sh. Milioni 900 ambapo lengo la harambee hiyo lilikuwa kukusanya sh.
Milioni 1.5.
“Wenzetu wamejitahidi wamefanikiwa kukusanya kiasi hicho katika
harambee hiyo leo hii wanarufiji tunapokea michango ya wenzetu
wanaothamini afya zetu na maendeleo ya wilaya yetu” alisema Dkt. Seif.
Aidha, Dkt. Seif alisema kuwa mfuko huo umeanzishiwa akaunti
yake ambapo michango yote huwekwa pamoja na kamati husika inapanga ni
vipaumbele vipi vifanyiwe kazi kwanza na ni kwa eneo gani la wilaya na
kwa wakati gani.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical
inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia alisema
kuwa kampuni yake imesukumwa na moyo wa kuwasaidia wanarufiji kwani
yeye amesomea wilayani humo hivyo kampuni yake inathamini na itaendelea
kusaidia masuala ya kiafya ambayo ndio kiini cha ufanisi wa maaenedeleo
wilayani humo.
Kampuni hiyo katika kufanikisha
utoaji wa huduma bora za jamii imechangia na kutoa vitanda 50, mifuko 50
ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara na kuahidi kutoa
madawati 10 pamoja na pesa sh. Milioni 10.
Harambee ya kusaidia Rufiji iliyofanyika jijini Dar es salaam
ilifanikishwa na kusimamaiwa na wanarufiji kwa kushirikiana na kampuni
ya Giant Surgical and Pharmaceutical na Jumuiya wa Kiislamu ya
ISTIQAAMA.
No comments:
Post a Comment