Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi
……………………………………………………………………………………………..
Mtandao wa Malezi Makuzi na
Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania – TECDEN ni chombo kinachoundwa na
mashirikia mbalimbali yanayofanya kazi za kuhudumia watoto wadogo
Tanzania. Mtandao huu ulianzishwa mwaka 2000 na kusajiliwa rasmi mwaka
2004. Makao makuu ya Mtandao huu yapo Jijini Dar es salaam. Hadi kufikia
mwaka 2014 Mtandao huu una jumla ya mashirika wanachama wasioungua 200
katika mikoa 14 ya Tanzania bara na Visiwani yanayotoa huduma kwa watoto
wadogo Tanzania
Lengo kuu la Mtandao ni kuboresha huduma za watoto wadogo Tanzania ili waweze kukua na kufikia utimilifu wao
Shughuli Kuu za Mtandao ni pamoja na:-
• Kufanya ushawishi na utetezi wa masuala yanayohusu uboreshaji
wa huduma na kulinda haki za watoto wadogo ikiwa ni pamoja na kushawishi
maboresho ya sera na kufuatilia utekelezaji wa sheria na miongozo
mbalimbali inayohusu uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.
• Kuhamasisha jamii na watoa huduma kutambua umuhimu wa
kuimarisha na kuwezesha watoto wadogo kupata mahitaji na haki zao za
msingi.
• Kuimarisha mifumo ya upashanaji habari na kuelimishana katika ngazi zote za huduma kwa watoto wadogo.
• Kutafiti na kutumia matokeo ya utafiti katika kushauri uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.
Dhana ya Malezi Makuzi na Mendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM)
Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ni istilahi ya
jumla ya programu na vitendo vinavyoandaliwa kuwasaidia watoto (kuanzia
mimba, kuzaliwa hadi miaka 8) ili kukua vizuri kimwili, kiakili,
kijamii, kihisia, kimaadili na kiroho. Watoto wanahitaji kuchangamshwa
katika nyaja na hatua zote za ukuaji, kiakili kwa michezo, kujifunza
kuzungumza, kukaa, kutambaa, kutembea na kupatiwa fursa ya kuanza
kujifunza mambo mbalimbali pamoja na utamaduni wao.
Utoaji wa huduma jumui za MMMAM.
Huduma hizi hujumuishwa ili kuwawezesha watoto wengi kupata
huduma jumuishi za MMMAM zitolewazo na sekta mbali mbali katika mkabala
jumui. Huduma hizi zinapaswa kupatikana kuanzia ngazi ya familia ,vituo
vya afya ya msingi,vituo vya kulelea watoto mchana, vituo vya Malezi
Makuzi ya awali ya mtoto vinavyomilikiwa na Jamii, madarasa ya awali na
madarasa ya msingi hususani darasa la kwanza na la pili.
Katika kutekeleza shughuli zake
Mtandao wa TECDEN umekuwa ukishirikiana na mashirika mbalimbali ya wabia
wa maendeleo ikiwemo shirika la Children in Crossfire kutoka nchini
Ireland na shirika la Better Way Foundation kutoka nchini Marekani
Ili kujua habari zaidi za TECDEN
na masuala ya utoaji huduma kwa watoto wadogo na faida zake, unaweza
kutembelea ofisi ya Mtandao makao makuu iliyopo Jengo la Posta mkabala
na Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi na Makao Makao Makuu ya Polisi jijini
Dar es Salaam.
Unaweza pia kuwasiliana kwa njia
ya simu au barua pepe na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi
kwa namba 0754 690 556 na barua pepe ecdnetwork@gmail.com na ghumpibr@yahoo.com
No comments:
Post a Comment