DEREVA AFARIKI DUNIA BAADA YA GARI ALILOKUWA AKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA WILAYANI MBOZI.
DEREVA ALIYEKUWA AKIENDESHA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.910 CVF AINA YA TOYOTA NOAH ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA STANFORD LUENJE (30) MKAZI WA MBOZI ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI HILO KUACHA NJIA NA KUPINDUKA HUKO ENEO LA MLOWO WILAYANI MBOZI.

TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA
KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:30 HUKO ENEO LA MLOWO, KATA YA MLOWO,
TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA
MBEYA/TUNDUMA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NDIMYAKE MWAKISU (33) NA 2. ELISHA
MWASHUYA (30) WOTE WAKAZI WA MBOZI WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA HOSPITALI
YA WILAYA YA MBOZI KWA MATIBABU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA
KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment