Wafanyakazi wa kampuni ya WABAG Constraction wakiendela na ujenzi wa wa kituo cha kuasfisha maji cha ruvu juu .
…………………………………………………………………………………….
WAZIRI wa maji Jumanne Maghembe
ametoa siku 90, kwa mkandarasi Megha Engineering Infrastructure Limitedi
anaesambaza bomba la maji mradi wa Mlandizi Kimara kufanikisha mradi
huo na kupeleka ripoti ya maradi,mamlka ya maji safi na maji taka
(Dawasco), kwalengo la kupata tathimini ya mradi.
Alitoa agizo hilo Januari 20, 2015 mkoani Pwani wakati akikagua
miradi minne ya Dawasco,yakusambaza maji Ruvu juu na Ruvu Chini
kufikisha Jijini Dar es Salaam.
Alisema,mpaka sasa mkandarasi alitakiwa aweamelaza kilomita 20,lakini chakushangaza mkandarasi huyo amelaza kilomita 12,tu.
Maghembe alisema utendaji kazi wa mkandarasi huyo ni mbovu na
nimewaagiza wabadilike na nitakuja kuwatembelea baada ya siku 90,na kama
hakutakuwa na maendeleo itabidi tuwafukuze.
“tumempatia mkandarasio huyu kiasi cha dola za kimarikani
59,ambao nisawa na bilioni 96 za kitanzani fedha hizi watanzania
watazilipa hivyo ni vema mkandarasi huyu afanye kazi iliyomleta,”alisema
Maghembe
Kwaupande wa maradi wa Ruvu juu wa kusafisha maji Waziri
Maghembe aliridhika na utendaji kazi wa mkandarasi anayejenga mradi huo
na kumtaka amalizie kufunga pampu mpya ili mgao wa maji upungue Dar es
Salaam.
Aidha alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Arcado Mutalemwa
kuhakikisha pampu zilizokwama bandarini zinafika leo na kufungwa siku ya
Alhamisi.
No comments:
Post a Comment