Viongozi wa kanisa hilo wakimshangilia mbunge huyo kwa msaada wake |
Waumini wa kanisa hilo wakifurahia misaada ya mbunge wao |
katibu mwenyezi wa wilaya ya Ludewa Filix Haule (kushoto ) na mmoja kati ya madereva wa mbunge Filikunjombe Bw Andondile wakisogeza vinanda viwili vya kisasa kwa mbunge Filikunjombe |
Mbunge Filikunjombe kulia akikabidhi msaada wa vinanda kwa viongozi wa kwaya katika kanisa la RC Madunda |
Kiongozi wa kwaya kanisani hapo akifurahia msaada wa vinanda kulia na mbunge Filikunjombe |
Mbunge Deo Filikunjombe (kushoto) akikabidhi msaada wa kinanda kwa viongozi wa kwaya kwaya katika kaniksa hilo la RC Madunda leo |
Mzee Nkwera ambae ni mshauri wa kisiasa wa mbunge Filikunjombe akizungumza kanisani hapo |
Bw Mgaya akimshukuru mbunge Filikunjombe |
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amechangia kiasi cha Tsh milioni 15 kwa ajili ya ukarabati wa kanisa la Roman Katoriki parokia ya Madunda wilayani Ludewa pamoja na kusaidia vinanda viwili kwa kwaya mbili kanisani hapo.
Akikabidhi msaada huo leo mara baada ya ibada ya jumapili mbunge Filikunjombe alisema kuwa amefika kanisani hapo baada ya kuomba kinada na kwaya ya kanisa hilo na hivyo kutokana na kuwepo kwa kwaya mbili amelazimika kutoa msaada wa vinanda kwa kwaya zote pamoja na kusaidia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ukarabati wa kanisa hilo.
Kwani alisema kuwa kanisa hilo ni mmoja kati ya makanisa makongwe yaliyojengwa miaka ya 1980 katika wilaya hiyo ya Ludewa na kuwa kanisa hilo ndilo kanisa la tatu kujengwa kwa wilaya ya Ludewa hivyo linahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa ili kuendelea kuwafanya waumini wa kanisa hilo kupata eneo la kuabudia.
Filikunjombe aliwataka waamuni hao na waumini wa madhehebu mengine katika wilaya ya Ludewa kuendelea kumwombea afya njema ili kupata nguvu ya kuwaletea maendeleo kama ambavyo ameendelea kufanya katika wilaya hiyo kama njia ya kuwashukuru wananchi wake kwa kumwamini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo la Ludewa .
“Imani ambayo wenzangu wananchi wa Ludewa mlioionyesha mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu kwa kunichagua kuwa mbunge kamwe sitaacha kuwakumbuka wananchi wangu wa Ludewa kila ninapokuwa bungeni mawazo yangu kurejesha ahsante yangu kwangu na kuona wilaya yetu ya Ludewa inaendelea kupiga hatua”
Pia mbunge huyo alisema kwa sasa mkakati wake na wa serikali ya Rais Dr Jakaya Kikwete ni kuona ujenzi wa barabara ya lami
kutoka Njombe hadi Ludewa inajengwa na tayari wakandarasi wa
kuanza ujenzi huo wamekwisha patikana ndani ya miaka hii miwili bararabara hiyo itakuwa imejengwa na ujenzi wake utafanyika kwa awamu tofauti.
kutoka Njombe hadi Ludewa inajengwa na tayari wakandarasi wa
kuanza ujenzi huo wamekwisha patikana ndani ya miaka hii miwili bararabara hiyo itakuwa imejengwa na ujenzi wake utafanyika kwa awamu tofauti.
Hata hivyo alisema kuwa akiwa mbunge wa jimbo hilo kamwe hatakubali kuona wana Ludewa anawapelekea maendeleo kwa upendeleo na kuwa lazima pande zote ikiwemo la milimani , mwambao wote wananufaika na matonda yake kwa kuwa na maendeleo wote.
Kwa
upande wake katibu wa itikadi na uenezi wa mkoa wa Njombe
Honoratus Mgaya akimpongeza mbunge huyo kwa kuendelea kusukuma
mbele maendeleo ya jimbo hilo ,alisema kuwa kazi zinazofanywa na
mbunge huyo zimekipatia heshima chama cha mapinduzi (CCM) na kuwa
utendaji mzuri wa kazi wa mbunge huyo ndio ambao umeitangaza wilaya
ya Ludewa .
No comments:
Post a Comment