Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy
Mwalimu amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika baadhi ya viwanda
vya Arusha lengo likiwa ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali
kuhusu viwanda kutotumia magogo kama nishati ya uzalishaji viwandani
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Arusha Bw. Fidelis Lumato mara baada ya kutembelea
kiwanda cha A –Z cha Jijini hapo kukagua masuala ya Mazingira.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Bw. Binesh
Haria Afisa Mwendeshaji wa Kiwanda cha A to Z cha Jijini Arusha. Naibu
Waziri alikuwa na ziara ya ukaguzi wa masuala ya Mazingira kiwandani
hapo.
Shehena
ya magogo iliyobaki katika Kiwanda cha Sunflag. Kiwanda hicho kwa sasa
kimebadilisha matumizi ya nishati ya uzalishaji kutoka kwenye magogo na
kutumia makaa ya mawe.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (Katikati) akipata
taarifa fupi kutoka kwa kwa uongozi wa Mkoa wa Arusha mara baada ya
kufanya ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani hapo kuangalia masuala ya
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix
Ntibenda na Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Mapunda.
Moja ya boiler
inayotumia makaa ya mawe katika Kiwanda cha Sunflag. Awali Kiwanda
hicho kilikuwa kinatumia nishati ya Magogo katika shughuli za uzalishaji
kiwandani hapo. Serikali imepiga marufuku matumizi ya magogo ili
kuhifadhi mazingira.
No comments:
Post a Comment