Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)
kinatarajiwa kutoa wahitimu wengi wa program ya teknolojia ya sanyansi
za maabara ili kupata wataalamu wa kufundishia masomo ya sayansi kwa
skuli za sekondari.
Hayo ni miongoni mwa ahadi za Mkuu
wa Chuo hicho dkta Richard Masika wakati wa mahafali ya sita ya Chuo
hicho yaliofanyika jijini hapa hivi karibuni.
Katika taarifa yake hiyo kwa naibu
waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi Jenista Mhagama alisema kwa
miaka mingi kuna upungufu wa walimu wengi wa masomo ya sanyansi na
wataalamu wa masuala ya maabara katika skuli za sekondari.
Alisema hali hiyo inathiri kwa
kiwango kikubwa ufundishaji wa masomo ya Sayansi kwa wafunzi wanaochukwa
masomo hayo na kushindwa katika ufaulu kwa kukosa walimu wenye ubora.
“ kutokana kutambua hali hiyo chuo
kikaamua kuanzisha mpango huo ilikuwapata wataalamu wengi zaidi ili
kwenda sambamba na kupanuka kwa ujenzi wa sekondari hapa
nchini”alitanabaisha dkta Masika.
Alisema kuwa skuli zinahitaji
waalimu wengi zaidi wa masomo ya sayansi na wataalamu wa maabara,hivyo
kwa kutambua umuhimu huo ndio maana tuanzisha mpango huo.
Alisema kuwa kutokana na chuo
kutambua umuhimu huo ndio maana kikaanzisha Programu hiyo wa kutoa
wataalamu hao wa maabara ilikuendana na mpango wa serikali wa matokeo
makubwa sasa.
Pia alisema kutokana na hatua hiyo
ufundishaji wa masomo hayo kwa vitendo utaongeza uelewa,umahiri na
ufaulu katika masomo ya sayansi,hatua ambayo itawezesha taifa kupata
wataalamu waliobobea katika Sayansi.
“Programu hiyo utakwenda sanjari
na ujenzi wa maabara katika shule za serikali za kata na utaongeza ari
ya wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi”alisema dkta Masika.
No comments:
Post a Comment