Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
Mohamed Asenga Akifungua kikao cha baraza la madiwani mwishoni mwa wiki
,kulia kwake ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Diwani wa Kata ya
Sitalike Slivester Nswima na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Said Juma Maraba.
Wataalam wakifuatilia kwa umakini mjadala wa kikao cha madiwani Halmashauri ya Nsimbo
(Picha na Kibada Ernest-Katavi)
……………………………………………………………………………
Na Kibada Kibada –Katavi
Madiwani wa
Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wameshauriwa
kupima Afya zao na hasa maambukizi ya VVU kabla ya kuchukua fomu za
kugombea Udiwani kwenye Kata zao ili waweze waweze kuwa mfano kwa watu
wanaowaongoza na kutambua afya zao kama kweli watakuwa na nguvu za
kutosha kuwatumikia wananchi waliowachagua kwa kipindi cha kuwepo
madarakani.
Diwani wa Kata
ya Kapalala Reward Sichone alitowa ushauri huo kwenye kikao cha
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Nsimbo baada ya kuwasilishwa kwa
taarifa ya kamati ya kuthibiti ukimwi iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa
hiyo Diwani wa Kata ya Sitalike Silvester Nswima.
Diwani Sichone
alieleza kuwa ni vizuri kwa madiwani hasa wa Halmashauri ya wilaya ya
Nsimbo wanao tarajiwa kumaliza muda wao mwaka huu wakaandaliwa
utaratibu na Halmashauri wa kupimwa maambukizi ya VVU kabla ya kumaliza
muda wao wa uongozi mwaka huu ili waweze kuwa mfano kwa watu wao wanao
waongoza.
Alilieleza
Baraza hilo la madiwani kuwa endapo watapimwa afya zao mapema
itawafanya wajitathimini kabla ya kuchukua fomu za kugombea udiwani.
Sichone
alisema endapo diwani atapimwa na kukutwa anamatatizo kwenye afya
yake itamsadia kuona kama kweli atakuwa na uwezo wa nguvu za kufanya
kazi za wananchi kwenye eneo lake.
Alifafanulia
kuwa haitakuwa vizuri kwa diwani ambaye atapimwa na kukutwa na
maambukizi ya VVU halafu achukue fomu za kugombea tena wakati anajua
kuwa hana nguvu za kufanya kazi za wananchi wake hivyo swala la
madiwani kupima afya zao ni jambo la msingi sana
“Jamani mnacke
lakini mambo haya ni muhimu sana katika jamii zetu hasa wananchi
tunaowaongoza wakiona tunafanya namna hiyo wanakuwa na imani nasisi
ingawa kupima siyo lazima ni hiari ya mtu “alisema Diwani Sichone.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti Ukimwi wa Baraza la
Madiwani Sylvester Nswima ambae ni Diwani wa Kata ya Sitalike
alipinga ushauri huo wa Diwani Sichone
Nswima alieleza
kuwa swala la Madiwani kupimwa afya zao kwa pamoja haiwezekani kwani
kupima ni hiyari ya kila mtu na sio lazima,hivyo kila mtu atapima kwa
muda wake na kwa hiari yake.
Naye Mwenyekti
wa Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Assenga alisema kitendo cha
madiwani kupima afya zao kinaweza kuwa ni mfano mzuri kwa watumishi
na wananchi wa Halmashauri ya Nsimbo kuona viongozi wao wakimwa afya
na kuwafanya nao wataiga mfano wa kupima mara kwa mara afya zao.
Aliwatoa
wasiwasi kwa kusema kuwa “Madiwani tusihofu kupimwa bali tuangalie
utaratibu wa kuwaita wataalamu waje watupime afya ili tuwe mfano kwa
watu wengine kwenye Halmashauri yetu na Mkoa wa Katavi kwa ujumla
wake”alisema Mwenyekiti Mohamed Assenga.
Katika taarifa
ya utekelezaji wa shughuli za ushauri nasaha na upimaji wa VVU kwa
hiariwalifanikiwa kupima watu 1221 kati ya wanaume 668 na wanawake ni
551 ambapo kati ya watu hao waliopima waliokutwa na maambukizi walikuwa
watu 36 kwa Halmashauri ya Nsimbo.
No comments:
Post a Comment