Mke
wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi. Gracia Machel akiwa na Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia M. Simba (Mb)
alipofika kutambulisha progamu ya ulinzi wa watoto kwa Mhe. Simba jijini
Dar es salaam, tarehe 21/1/2015.
Mke
wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi. Gracia Machel akiwa na
mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia
M. Simba (Mb), na Katibu Mkuu Bibi Nuru M. Millao (wa pili kulia) na
baadhi ya wakurugenzi wa Wizara.
………………………………………………………………………………
By: Erasto T. Ching’oro- Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia an Watoto
Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini (Bi Gracia Machel)
yuko katika ziara fupi nchini Tanzania kusaidia kuhimiza Serikali na
wadau kutokomeza tatizo la ndoa za utotoni hapa nchini kupitia programu
na miradi mbalimbali atakayoifadhili ili kuwawezesha watoto wa kike
kupata haki ya elimu ambayo ni nyenzo muhimu katika kujikomboa dhidi ya
umaskini.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Wizara ya Maendeleo ya
Jmaii, Jinsia Na Watoto, jana tarehe 21 Machi, 2015; Mama Machel
aliipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya jamii,
Jinsia na watoto kwa jitihada zake kubwa inazozifanya kupambana na
tatizo la mimba na ndoa za utotoni. Aidha, ameshauri Wizara, asasi za
kiraia na wadau mbalimbali hususan viongozi wa mila/jadi na dini
kushirikiana naye na kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko
chanya kupitia programu hizo anazotarajia kuzianzisha. Alifafanua kuwa
mkoa wa Mara ndio utakaokuwa wa kwanza kunufaika na uanzishwaji wa
programu hiyo kwani mkoa huo ni miongoni mwa mikoa iliyo na mila
gandamizi dhidi ya wasichana na wanawake; na ukiwepo mfumo dume.
Akitoa akimshukuru Bi. Machel kwa jitihada zake za dhati
anazozifanya, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa
Sophia Simba (Mb) amesema ni kweli tatizo hilo lipo nchini lakini
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa haki za watoto yakiwapo mashirika
yasiyo ya Kiserikali, asasi za kiraia na vyombo vya habari kwa pamoja
wanashirikiana kupambana kikamilifu na tatizo hili kupitia mipango
shirikishi jamii ili kufikia ufumbuzi endelevu.
No comments:
Post a Comment