Edgar Lungu ni waziri wa sheria wa Zambia na anaongoza kinyang'anyiro cha Urais Uchaguzi wa Rais unafanyika hii leo nchini Zambia baada ya Kiongozi wa Nchi hiyo Michael Sata kufariki dunia mwaka jana.
Haya ni mambo matano ya kufahamu kuhusu uchaguzi huo.
1. Uchunguzi wa kitabibu Baada ya vifo vya Marais wawili hivi karibuni, kumekuwa na wito kwa wanaowania urais -edgar Lungu,Hakainde Hichilema,Edith Nawakwi na Nevers Mumba, ambao wote wako kwenye miaka ya 50 kufanyia uchunguzi wa kitabibu afya zao ili kujua kama wataweza kutumikia wadhifa huo. Mjadala huu uliibuliwa na Mbunge mmoja Sylivia Masebo, ambaye ameingia upinzani akitoka Chama tawala , Patriotic Front Mbunge huyo amedai kuwa Edgar Lungu hali yake ya kiafya haiko sawa kuwa Rais wa Zambia na kumpa changamoto ya kufanya vipimo. Lakini Msemaji wa Lungu alisema Lungu yuko tayari kufanya vipimo vyovyote, wakati wowote.Lakini haifahamiki kama ameshafanya vipimo hivyo.
2. Swala la rangi
Rais wa mpito Guy Scott Guy Scott,
Raia wa Zambia mwenye asili ya Scotland aliteuliwa kuwa Rais wa mpito wa nchi hiyo siku moja baada ya Sata kuaga dunia. Yalizungumzwa mengi kuhusu Scott kuwa Rais wa kwanza mweupe barani Afrika lakini kwa Raia wengi wa Zambia rangi ya ngozi yake haikua tatizo kwao,wengi wao wakisema wanamuona kama Raia mwingine yeyote wa Zambia. Kwa muda mrefu tangu miaka ya 90 Scott amekuwa akijihusisha na siasa akihama chama kimoja kwenda kingine hata akajiunga na chama cha PF akiwa mgombea mweza wa Sata, walikuwa marafiki wakubwa. Uhusiano wake na mgombea Edgar Lungu si mzuri.Tofauti zao zilidhihirika baada ya Scott kumuondoa Lungu kwenye nafasi yake ya Katibu Mkuu. Kuelekea uchaguzi wa mwaka 2016. Uchaguzi nchini Zambia hufanyika kila baada ya miaka mitano, hivyo atakayeshinda atakuwa Rais kwa kipindi cha chini ya miaka miwili, kisha utaitishwa uchaguzi Mkuu mwaka 2016.
3. Uhusiano na China
Lugha ya Mandarin hufunzwa katika shule za umma nchini Zambia
Lugha ya Mandrin hufundishwa katikashule nyingi nchini Zambia. Hii ni ishara ya uhusiano uliopo kati ya China na Zambia nchi inayozalisha madini ya sahaba ingawa uhusiano huo umekuwa na vuta nikuvute zake. Kuna madai kwamba makampuni ya China yanawatumia vibaya wafanyakazi wenyeji kwa kuwalipa mishara duni. Bwana Sata alishinda uchaguzi mwaka 2011, hasa kwa sababu ya kukosoa makamapuni ya kichina kwa kuwakandamiza wafanyakazi wenyeji. Alipokuwa mamlakani uhusiano huo uliendelea kunawiri.
4: Muhula wa miaka 2 Uchaguzi nchini Zambia hufanyika kila baada ya miaka mitano. Yeyote anayeshinda uchaguzi huu, atasalia mamlakani kwa chini ya miaka 2 hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika mwaka 2016. Zambia ni nchi yenye demokrasia huku vyama kadhaa vikitoa ushindani mkali kwa chama tawala. Uchaguzi umekuwa ukifanyika tangu kumalizika kwa utawala wa chama kimoja mwaka 1991. Wazambia sasa wanawatarajia viongozi wao kuondoka ofisini bila vurugu.
5. Baada ya Kaunda
Marais wawili waliaga dunia wakiwa madarakani, mmoja aliaga dunia
baada ya kumaliza muda wake na wa nne, Rupiah Banda bado yu hai.
Kaunda, alizaliwa mwaka 1924, bado ni mwenye nguvu akielekea kuwa na umri wa miaka 91.
Kaunda
alitawala kwa miaka 27 na siku tisa. Kifuatiwa na Frederick Chiluba
aliyetawala kwa miaka 10 na siku 61, Levy Mwanawasa aliongoza Zambia kwa
miaka sita na siku 230 huku Banda akitawala kwa miaka mitatu na siku
86., Marehemu Sata alitawala kwa miaka 3 na siku 35.
No comments:
Post a Comment