Polisi nchini Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo wamewafyatulia risasi waandamanaji kwenye mji mkuu
Kinshasa walio na hasira katika kile kinachoonekana kama jitihada za
kutaka kuongoza uongozi wa rais Joseph Kabila.
Watu kadha
walitolewa eneo la kati kati mwa mji wakiwa na majeraha ya risasi ambapo
pia kulitoka makabiliano kwenye chuo kikuu cha mji huo.
Milio ya risasi iliripotiwa katika maandamano mengine katika mji ulio mashariki wa Goma.
Watu
kadhaa walipatikana na majeruhi ya risasi katikati mwa mji huo huku
ghasia zengine zikiripotiwa katika katika chuo kimoja kikuu.
Viongozi wa upinzani waliitisha maandamano hayo baada ya bunge dogo
kuidhinisha sheria siku ya jumamosi inayoagiza kufanyika kwa hesabu ya
idadi ya watu kabla ya uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka ujao.
Wabunge hao wa upinzani wamesema kuwa mpango huo utachelewesha uchaguzi huo ambao umekuwa ukingojwa kwa hamu kwa miaka kadhaa.
Rais
Joseph Kabila ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 15 amehudumu miula
miwili na hawezi kuwania tena urais kulingana na katiba.
Bunge kuu linatarajiwa kuungazia mswada huo wa uchaguzi hii leo.
No comments:
Post a Comment