Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akiwaeleza wahariri wa vyombo vya habari nchini wajibu na umuhimu wa
vyombo vya habari katika mchakato huu wa upatikani wa katiba mpya
ikiwemo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa mchakato huu kwa mustakabali wa
Taifa pia alivipongeza vyombo vya habari katika elimishaji wa wananchi
katika mchakato wa Bunge Maalum la Katiba, Wakati wa Mkutano na Wahariri
wa Vyombo vya Habari jana Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la wahariri Absalom Kibanda akiongea wakati wa mkutano
uliowakutanisha wahariri wa vyombo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamduni
na Michezo ambapo Dkt. Fenela Mukangara ambapo waliwataka wahariri kuwa
wamoja katika masuala ya kitaifa hasa yatakayopelekea kuibomoa nchi
yetu pia aliwaasa wahariri kutumia kalamu zao vizuri kuwaelimisha
wananchi katika mchakato huu wa kuelekea upatikaji wa Katiba Mpya
kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene, Naibu
Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mh.Angela Kairuki na Mwisho ni Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara jana
Jijini Dar es Salaam.
Mzee
Kingunge Ngombale-Mwiru akiongea na wahariri wa vyombo vya habari
ambapo ambapo aliwaeleza kuhusu umuhimu wa upatikanaji wa katiba mpya
kwa maendeleo ya Taifa ikiwa katiba iliyopendekezwa imezingatia Masuala
muhimu ya ukuzaji uchumi wan chi pia uzingatiaji wa makundi mbalimbali
katika jamii na alisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kuendelea kutoa
elimu kuelekea upatikanji wa katiba mpya kwani katiba ni chombo cha
ukombozi wa nchi.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la wahariri Absalom Kibanda akisamiana na Mzee Kingunge
Ngombale-Mwiru wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya Habari na
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Mh.
Hamadi Rashid Muhamed akiwaeleza wahariri wa vyombo vya habari ambapo
alieleza furaha yake kwa katiba inayopendekezwa kujikita katika kutatua
changamoto za muungano zitakazopekea kuimarika kwa muungano wa Tanzania
bara na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment