Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Uwekezaji
ya UTT, Migangala Simon.
Ofisa
Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT, Migangala Simon
(katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo, kuhusu ushirikiano wa uwekezaji katika soko la hisa kwa nchi
zinazounda jumuia ya Afrika Mashariki.
Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Uwekezaji ya UTT imesema ushirikiano wa uwekezaji katika soko la hisa
wa nchi za jumiya ya Afrika Mashariki utaleta tija kwa nchi hizo.
Akizungumza
Dar es Salaam leo Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo, Migangala
Simon alisema uwepo wa ushirikiano utasaidia hata nchi moja ikiwa na
matatizo iwe rahisi kusaidiana.
“Kwa
mfano Tanzania sasa hivi inaelekea katika uchaguzi mkuu ambao unatarajia
kufanyika Oktoba mwka huu inavyoelekea hivyo fedha nyingi zitatumika
lakini kukiwepo na ushirikiano na umoja ni lazima nchi nyingine kusaidia
kupitia soko la hisa,”alisema.
Alisema
kampuni hiyo ina jumla ya mifuko mitano,kuna mfuko wa umoja,wekeza
maisha, mfuko wa watoto,mfuko wa ukwasi na mfuko wa jikimu.
Simon alisema mifuko yote ina lengo la kusaidia wananchi wote walio katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Pia huwa
tunawasaidia watoto katika maendeleo yao hapa nchini hususani elimu
watoto hao ni wale walio chini miaka 18,”alisema.
Simon
alitumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kujiunga na kampuni hiyo na
kuweka hisa zao ambapo watapata gawio kubwa kulingana na hisa
walizoweka. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
No comments:
Post a Comment