Waziri wa usalama nchini Kenya
Joseph Nkaissery amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi
waliofyatuliwa gesi ya kutoa machozi wakati walipokuwa wakiandamana
kupinga unyakuzi wa kipande cha ardhi ambacho kilikuwa uwanja wao wa
kuchezea.
Bwana Nkaissery amempa mnyakuzi wa ardhi hio siku moja
kuondoa sehemu ya ukuta iliobaki baada ya wanafunzi kuuangusha na kisha
kuondoka katika eneo hilo.
Nkaisery ameongeza kwamba serikali itaweka uzio katika ardhi hio na kuiwacha kuwa uwanja wa kuchezea wa wanafunzi hao.
Wakati
huohuo, amewaonya wanaharakati dhidi ya kukiuka sheria kila wakati
wanapojiandaa kufanya maandamano badala ya kuchukua sheria mikononi
mwao.
Mnamo Jumatatu, wanafunzi watano na polisi mmoja walijeruhiwa katika
vurugzu zilizotokea baada ya wanafunzi kuandamana kupinga unyakuzi wa
ardhi yao kutoka kwa mtu aliyekuwa na mipango ya kufanya ujenzi.
Wakenya
wamekosoa polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wanafunzi ,
hali ambayo imesababisha afisa ammoja mkuu kusimamishwa kazi kwa mda.
Shirika
la kutetea masilahi ya watoto, la Save The Children, pia limelaani
kitendo cha polisi dhidi ya wanafunzi hao ambao walikuwa wanaandamana
kwa amani kutetea uwanja wao uliokuwa umenyakuliwa.
No comments:
Post a Comment