Picha zote na Ingiahedi Mduma-Wizara ya Fedha tukiwa Washington DC.
……………………………………………………………………………
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile, mchana wa leo
ametiliana saini makubaliano ya mkataba wa kuanzisha Mradi wa Maji
katika Wilaya ya Same na Mwanga. Dr. Likwelile alisaini Mkataba huo kwa
niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Kiarabu
ya Maendeleo ya uchumi ya Afrika . Aliye wakilisha Benki hiyo ni Eng.
Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi
Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia.
Aidha katika kutiliana saini Mkataba huo Dr. Likwelile
alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa Serikali ya Tanzania inatambua
kuwa BADEA imetoa Dola za Kimarekani milioni 12.0 sawa na shilingi
Bilioni 20.1 za Kitanzania kwa ajili ya kusaidia mradi wa maji katika
Wilaya ya Same na Mwanga. Hivyo inatoa shukrani zake za dhati kwa BADEA
kwa kusaidia kuchochea maendeleo ya Tanzania.
“Msaada huu tulioupata leo utaisaidia Serikali kutatua tatizo la
maji katika wilaya ya Same na Mwanga, hii inaonyesha ni jinsi BADEA
unaunga mkono na kutekeleza jukumu zima la kushiriki katika masuala ya
kijamii na ya kiuchumi kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo tunaomba
muendelee kutusaidia”. Alisema Dr. Likwelile.
Dr. Likwelile alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa, kama
anavyofahamu gharama za mapendekezo ya mradi mzima ni Dola za Kimarekani
million 110.43 na hii inahitaji uchangiaji kutoka katika mifuko mingine
kama mfuko wa maendeleo wa Saudia , Mfuko wa Kimataifa wa OPEC na
Serikali kuchangia fedha kusaidia mradi huu. Kwa hili sina wasiwasi nalo
kwani ninafuraha kujua kwamba umeshakubaliana na ninaujasiri kuwa
jitihada zako zitafanikiwa.
“Mradi huu wa maji wq wilaya ya Same na Mwanga unalenga kusaidia
kuwepo kwa maji kwenye jamii mbalimbali zilizopo kwenye mradi huo.”
Aliongeza Dr.Likwelile.
Aliendelea kusema kuwa,mradi huo utakapo kamilika :
(i) utaongeza kiwango cha watu wengi kuweza kupata maji safi na salama ya kunywa.
(ii) Uchumi wa Same na Mwanga utaimarika pamoja na hali ya afya
kwa jamii nayo itakuwa imara hasa kwa maeneo yale yanayoguswa na mradi.
(iii) Hali ya maisha ya watu wa Same na Mwanga itainuka.
“Mafanikio ya ukamilishaji wa mradi huu ni muhimu sana kwa
uchumi wa jamii na maisha bora kwa watu wa wilaya ya Same na Mwanga”.
Alisema Likwelile.
Dr. Likwelilie alimalizia kwa kusema kuwa“Tanzania na Saudia ni
marafiki wa muda mrefu sana, hivyo tutazidi kushirikiana na kuhakikisha
kila kitu kinaenda sawa”.
Hali ya hewa ya mjini Washington Dc. ni mvua za vipindi na baridi kiasi.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji – Wizara ya Fedha
Washington D.C
11/10/2014
No comments:
Post a Comment