Mkuu
wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema (wa pili kutoka
kulia) akimtambulisha viongozi wa chuo cha CBE ,Makamu wa pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd (katikati) leo jijini Dar es salaam
wakati wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50. Kulia ni Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akipata maelezo kutoka
kwa Bi. Esther Kibua, mwanafunzi wa mwaka wa 3 wa chuo cha Elimu ya
Biashara CBE kampasi ya Dar es salaam juu ya namna chuo hicho
kinavyowaandaa kuitumia elimu wanayoipata chuoni hapo pindi
watakapomaliza masomo yao. Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimuuliza swali Bi.
Esther Kibua, mwanafunzi wa mwaka wa 3 wa chuo cha Elimu ya Biashara
CBE kampasi ya Dar es salaam alipotembelea banda la maonesho la
wanafunzi wa Chuo cha CBE leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za
kilele cha miaka 50 ya chuo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akifafanua akifafanua jambo alipotembelea banda la maonesho la Idara ya Mizani na Vipimo la Chuo cha CBE leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za kilele cha miaka 50 ya chuo hicho.Kushoto ni Mwalimu wa Idara ya Mizani na Vipimo wa Chuo hicho Bw. Faraja Nyoni.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

No comments:
Post a Comment