TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 21, 2015

Msichanganye dini na siasa- Dr. Mary Nagu

maryNa Gladness Mushi, Arusha

WAZIRI wa Nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary , Nagu amewataka viongozi wa dini kutochanganya dini na siasa na badala
yake wahubiri amani kwani wakichanganya siasa watagawa waumini wao.
Dr Nagu aliayasema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
Jijini hapa kuhusiana na mahusiano baina ya viongozi wa dini na siasa
“viongozi wa dini wamepewa dhamana kubwa sana ya kuhubiri amani kila
mahali na ili kuhakikisha kuwa jamii inafuata kanuni za dini mnapaswa
kutochanganya dini na siasa ili wapatikane waumini wema ambao
hawafanyi maovu”aliongeza
Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa dini kumwomba mungu
sana ili kuwezesha kuweze kupatikana kwa katiba mpya huku akiwataka
watu kupiga kura za maoni ili waweze kuvuka katika mchakato huo kwa
amani.
Nae Askofu Solomo Masangwa kutoka katika kanisa la kkktalisema
kuwa ataendeleza ushirikiano zaidi na serikali ili kuhakikisha kuwa
dayosis hiyo inaendelea kukua kiuchumi na kimaendeleo katika
kuhakikisha kuwa jamii inanufaika na huduma za kanisa hilo.
Alieleza kuwa pia atasimamia kikamilifu mpango mkakati wa miaka 5 ambao
hadi sasa wameshauweka wa kuwapatia waumini huduma za miili na akili
ambayo itaongozwa na tunu za mwenyezi Mungu.
Hataivyo Mkuu wa kanisa la kiinjili kilutheri Tanzania KKKT  Dr Alex Malasusa aliwataka viongozi wa dini
kusimamia nafasi zao na tunu ili kuhakikisha kuwa amani
inazidi kuwepo wasiruhusu kuwepo kwa uvunjifu wa amani bali umoja
uzidi kuwepo .
Aidha aliwataka waumini kutumia haki yao msingi kushiriki kikamilifu
katika zoezi la mchakato wa katiba mpya pamoja na uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

No comments:

Post a Comment