Asilimia 50 ya watu wazima nchini
Japan hawashiriki katika tendo la ngono kulingana na utafiti, swala
linalosababisha kupungua kwa idadi ya watu nchini humo.
Ripoti
hiyo iliofanywa na shirika la upangaji uzazi nchini humo imebaini kwamba
asilimia 49.3 ya watu 3000 waliohojiwa hawakushiriki ngono mwezi
uliopita.
Kati ya asilimia 48.3 waliohojiwa walisema kuwa
hawakushiriki katika ngono kwa mwezi moja huku asilimia 50.1 ya wanawake
wakijizuia kushiriki ngono.Takwimu zote zilipanda kwa asilimia 5 kutoka
kwa ufatiti uliofanywa awali mwaka 2012.
Walipoulizwa ni kwa nini
hawashiriki katika tendo la ngono, asilimia 21.3 ya wanaume walio
katika ndoa walidai kuchoka baada ya kutoka kazini huku asilimia 15.7
wakisema kuwa hawana haja ya kushiriki katika tendo la ngono baad ya
wake zao kujifungua.
Kati ya wanawake asilimia 23.8 walisema kuwa tendo la ngono linasumbua na asilimia 17.8 wakidai walikuwa wamechoka.
Swala
jengine la kushangaza ni kuongezeka kwa idadi ya vijana ambao hawana
hamu na tendo la ngono.Zaidi ya asilimia 20 ya wanaume walio kati ya
umri wa miaka 25 na 29 hakuwa na hamu ya kufanya ngono.
No comments:
Post a Comment