WAZIRI wa n Nchi Ofisi ya Makamu
wa Pili wa Rais Muhamed Abuod Mohamed amesema atamuandikia barua Waziri
wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mathias Chikawe
kuongeza fedha za usafiri kwa askari wa Jeshi la Polisi mara baada ya
kustaafu na kurejea makwao.
Hayo ameyasema leo huko Baraza la
Wawakilishi Chukwani wakati akijibu suali la nyongeza la Mwakilishi wa
Jimbo la Wawi Saleh Nassor Juma alietaka kujua sababu za askari polisi
anapostaafu kulipwa shilingi 66,000 kwa ajili ya nauli yake na
kusafirisha mizigo kwa masafa ya kilomita 20 kiwango ambacho ni kidogo
na hakikidhi haja.
Waziri Aboud amesema kutokana na
kadhia hiyo atalazimika kuandika barua kwa Waziri Nchimbi kuliangalia
suala hilo ili kulitafutia ufumbuzi na kuwaondoshea shida asikari hao
wanapostaafu.
Aidha Waziri huyo alisema kuwa
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar jukumu lake ni kuratibu masuala
ya Muungano na kazi ya usimamizi iko chini ya Wizara ya Mambo ya
Ndani.`
Waziri Aboud akitoa ufafanuzi wa
madai ya askari watatu waliostaafu kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja
ambapo ilielezwa kuwa walipewa milioni 16 ili kurudi makwao kwamba
taarifa hiyo sio kweli.
Alisema ana elewa kuwepo kwa
askari hao na kusema askari anapostaafu hutaarishiwa usafiri wa mizigo
pamoja na familia zao hadi makwao jambo ambalo hufanyika kwa kutegemea
mstaafu alikuwa na cheo gani.
Baada ya ufafanuzi huo alisema
kuwa Kamishna wa Polisi aliwaita askari hao ofisini kwake na
kuwafahamisha utratibu ulivyo,na askari hao baadae waliridhika.
No comments:
Post a Comment