TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, June 27, 2016







Mashine za tiketi za kieletroniki kuanza kutumika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.

MPALULEBLOGS:
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisisitiza jambo wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi zakieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
Mhandisi kutoka kampuni ya B.C.E.G ya China Bw. Xiong (kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge(kulia) kuhusu mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
Mtaalamu wa Mashine za tiketi za kieletroniki kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew Emmanuel (kushoto) akimuelekeza jinsi ya kutumia moja ya mashine hizo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipotembelea kuangalia maendeleo ya uwekaji wa mashine hizo uwanjani hapo Leo Juni 27,2016.
Mtaalamu kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew Emmanuel akirekebisha moja ya mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.



Baadhi ya wananchi wakijaribu kutumia mashine ya tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM

MKUTANO WA MASHAURIANO YA KITALAM JUU YA KUANZISHA VITUO BORA VYA UVUVI WAFANYIKA ZANZIBAR

Na Mwashungi Tahir- Maelezo Zanzibar

WAZIRI wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Hamad Rshid Muhammed, amesema ipo haja kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU kuungana kwa pamoja katika kuangalia soko la ndani katika masuala ya uvuvi ili kukuza uchumi wa nchi hizo.

Akifungua mkutano wa siku mbili wa Nchi wanachama wa Umoja wa Arika AU, wa kujadili namna ya uzalishaji wa samaki, taaluma bora ya uvuvi na namna ya kuwawezesha wavuvi, uliofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Mazizini, Hamad alisema soko la Afrika limekuwa likishuka kutokana na kutokuwa na wataalamu wa kutosha katika sekta hiyo.

Alisema mara nyingi nchi hizo zimekuwa zikijadili suala la kilimo kutokana na kuonekana ndio muhimu kwa jamii, lakini sasa ipo haja kuzungumzia suala la bahari kwa umuhimu wake hasa katika kukuza kipato cha wananchi na taifa kwa ujumla.

Aidha, aliwataka Waafrika kutumia fursa zilizopo katika nchi zao katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuwapatia wadau husika elimu itakayowajengea uwezo wa kujua nyenzo ziliopo nchini ili waweze kufaidika nazo pamoja kuwashawishi kutumia masoko ya ndani kwanza kabla ya kutumia masoko ya nje.


Meza kuu ikisikiliza utaratibu wa Mkuta kutoka kwa Masta Solomon hayupo (pichani). Mkurugenzi kutoka Umoja wa Africa- Ofisi ya rasilimali wanyama Simplice Noula akitoa tarifa ya ofisi yake katika Mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.
Waziri wa Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rshid Muhammed akifungua Mkutano wa siku mbili wa mashauriano ya kitaalam juu ya kuanzisha vituo bora vya uvuvi na ufugaji samaki Africa, uliofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Mjini Zanzibar.

Waganga wa tiba asili watakiwa kujisajili

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma —————————- Waganga wa tiba asili ambao wamekuwa wakitoa huduma ya tiba pasipo kujisajili wametakiwa kujisajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili waweze kutambulika kisheria. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla ameyasema hayo leo, Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge Viti Maalum Mhe. Zainabu Mussa Bakar juu ya udanganyifu unaofanywa na waganga wa tiba asili wa kutoa dawa feki kwa wagonjwa. “Waganga wa tiba asili wapo kisheria, ni kweli wapo wanaotoa dawa feki, na wengi wao ni wale ambao hawajasajiliwa, hivyo tumewaagiza kujisajili ili tuweze kuwatumbua na dawa zao ziweze kuhakikiwa na kusajiliwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu,” alifanunua Mhe. Kigwangalla. Mhe. Kigwangalla amesema kuwa, mganga yoyote atakaye kiuka agizo hilo la kujisajili basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Aidha, amesema Wizara iko makini na ufuatiliaji wa dawa feki nchini kwani wanapopata fununu ya uwepo wa dawa feki hutuma kikosi kuchunguza na ikibainika kuwa dawa ni feki basi hatua kali huchukuliwa kwa muhusika. Aliendelea kwa kusema kuwa, ili kudhibiti uingizwaji wa dawa feki nchini Wizara hiyo hufanya uhakiki wa muda mrefu kuchunguza iwapo dawa inayopendekeza kuingia nchini siyo feki na inafaa kwa matumizi ya binadamu, ikiwa dawa haina madhara yoyote basi inasajiliwa kwa ajili ya kuingia sokoni. Vilevile Mhe. Kigwangalla amesema kuwa, Wizara imewaagiza waganga wa tiba asili kufunga dawa zao kwa kutumia vifungashio maalum vya madawa ambavyo vitasaidia dawa hizo kuendelea kuwa salama kwa mtumiaji kwa kipindi kilichopangwa kutumika.

WATUMIAJI WA UMEME WA JUA WA MOBISOL WAFIKIA 50,000.



Sunday, June 26, 2016

BREAKING NEWZZZ: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na afanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa


 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. 
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine. 
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi. 
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu. Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine. 
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri. Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali. Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)

ARUSHA
1.      Arusha            -           Mrisho Mashaka Gambo
2.      Arumeru        -           Alexander Pastory Mnyeti
3.      Ngorongoro   -           Rashid Mfaume Taka
4.      Longido          -           Daniel Geofrey Chongolo
5.      Monduli         -           Idd Hassan Kimanta
6.      Karatu             -           Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
1.      Kinondoni      -           Ally Hapi
2.      Ilala                 -           Sophia Mjema
3.      Temeke         -           Felix Jackson Lyaviva
4.      Kigamboni     -           Hashim Shaibu Mgandilwa
5.      Ubungo          -           Hamphrey Polepole

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHITIMISHA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR'AN TUKUFU YA KIMATAIFA

RAIS WA VoWET MAIDA WAZIRI AZINDUA UMOJA WA WANAFUNZI WA BIASHARA(BAA) ATOA SEMINA YA UJASILIAMALI, (TIA) DAR ES SALAAAM

SERENGETI BOYS YAONGOZA GOLI 3-0 DHIDI YA SECHELLES UWANJA WA TAIFA,MPIRA UNAENDELEA.

GARI ZITAKAZOKAMATWA KWA KUHUSIKA NA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA KUFILISIWA-SMZ


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepanga mikakati maalum ya kuzifilisi gari zitazokatwa au kuhusika uingizaji wa dawa za kulevya kwa lengo la kudhibiti uingizaji, usambazaji na utumiaji wadawa hizo nchini . Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed huko Mnara wa kumbukumbu Kisonge katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Usafirishaji na Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani amesema serikali haitamuonea muhali yoyote atakae husika na uingizaji wa biashara ya dawa za kulevya kwa lengo la kutomeza janga hilo linathiri jamii na kupoteza nguvu ya Taifa. Amesema wafanyabiasha wa bidhaa hiyo hawalitakii mema Taifa kwani wao ni wahujumu wanaorejesha maendeleo ya nchini wanawaumiza vijana na watoto na kupoteza nguvu kazi ya Taifa hivyo wanahitaji kufichuliwa kwa nguvu bila ya kuwaonea muhali. Ameeleza kuwa tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya linamtoa mtu katika hadhi yake ya ubinadamu kwa kutengwa na jamii na kumsababishia madhara makubwa ikiwemo maradhi ya Ini, Figo, Ukimwi na Ugonjwa wa akili pamoja na kupoteza viungo muhimu vya mwili. Aidha Waziri Aboud amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa siasa wanawatumia vibaya madaraka yao kwa maslahi yao binafsi kuwatumia vijana kinyume na sheria jambo ambalo linachangia vijana hao kijiingiza katika vikundi viovu na hatimae kujiingiza katika utumiaji wa dawa hizo kwa kuwapotezea malengo na kuiathiri jamii. Waziri huyo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni 200 Duniani wameathitika na utumiaji wa dawa za Kulevya ambapo Zanzibar watu 10000 wameathirika na utumiaji wa dawa hizo kati ya 3200 wanatumia niia ya kujidunga sindano . Hata hivyo Waziri huyo amewata wazee na walezi kuwalea vyema watoto wao kwa kuwafunza maaadili mema ili kuweza kujiepusha na kujiingiza katika vikundi viovu sambamba na kuwapokea walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya kwa kuwajali , kuwakubali, kuwasidiana pamoja na kuwapa ushauri kwa lengo la kuwaondolea matatizo yao ili wasirejee tena katika janga hilo. Nae Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Moh’d Mahmoud ameitaka jamii kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuwadhiti janga hilo kupitia njia zote zinatumika kupitishia dawa hizo kwa kukata minyororo iliomo katika sehemu husika kwa lengo la kutokomeza uingizaji wa bidhaa haramu nchini. Akitoa taarifa ya Jeshi la Polisi Mngwali Ussi amesema jumla ya kesi 79 zimeripotiwa kati ya kesi saba zinahusiana na dawa za kulevya ambazo zinaendelea mahakani na kesi 72 za makosa tofauti ambazo ziko chini ya upelele wa polisi. Wakitoa ushahidi vijana waliopata nafuu wameionya jamii wasiwaachie watoto wao kukaa katika vikundi na kujiepusha na marafiki waovu kwani ndio kishawishi kikubwa kinachopelekea watoto hao kujiingiza katika dimbwi la dawa hizo Siku ya Kupambana na Usafirishaji na Utumiaji wa Dawa za Kulevya Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 26 Juni ambapo Ujumbe wa Mwaka huu Tuwajali, Tuwasikilize Watoto na Vijana.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWATAKA WAISLAMU NCHINI KUDUMISHA AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO

MPALULEBLOGS:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa tafrija ya Futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waisalm wa Tanzania (Bakwata) iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Kinondoni Muslim ambapo alimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuwahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) waendelee kuombea amani katika Taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akizungumza wakati wa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania ambapo alisema uongozi wa sasa wa BAKWATA umedhamiria kudumisha umoja,upendo na mshikamano baina ya Waislamu wote nchini, Tafrija hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania.
Sehemu ya wageni waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislam katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jopo la Masheikh Sheikh Suleiman Amran Kilemile akitafsiri moja ya aya ya Quran inayojenga na kuimarisha umoja na mshikamano kwa waislam.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Shekh Alhad Mussa Salum akitoa utambulisho wa wageni wa jumuiya mbali mbali za waislam waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi wa Wanawake Waislamu Tanzania wakisikiliza kwa makini nasaha za viongozi mara baada ya kufuturu katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania.

======  =====  =======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI amewahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- waendelee kuombea amani katika taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.

Kauli hiyo ya Rais imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN kwa niaba ya Rais katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- katika uwanja wa shule ya sekondari ya KINONDONI MUSLIM jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema jamii yeyote inayolelewa na kukua katika misingi ya kufuata maandiko ya Mwenyezi Mungu ni vigumu kujiingiza kirahisi katika vitendo vinavyomchukiza Mungu vikiwemo vitendo vya uhalifu.

Rais MAGUFULI pia amewatakia kheri waumini wote wa dini ya kiislamu kote nchini katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa upande wake, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh ABUBAKAR ZUBEIR ameipongeza serikali kwa hatua inazochukua katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa nchini na kusisisita kuwa Viongozi wa BAKWATA na wataendelea kushirikiana na serikali katika kukemea vitendo viovu katika jamii kama hatua ya kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinakoma hapa nchini.

Mufti wa Tanzania pia ametoa rai kwa waislamu wote nchini wadumishe umoja,upendo na mshikamano miongoni mwao katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mfungo kama kitabu kitukufu cha QUR’AN kinavyoelekeza.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais.
26-Jun-16

KAMATI YA MASHINDANO NA USAJILI YA COASTAL UNION YAWEKA BAYANA MIKAKATI YAO

WATUMISHI eGA WAASWA KUBORESHA MIFUMO YA TEHAMA KUONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO NDANI SERIKALI.

k7 







Mh.January Makamba Ashiriki Mahafali ya 24 ya Chuo cha Biblia mkoani Tanga

MASAUNI AKABIDHI MSAADA WA PAMPU NA KUKAGUA MIRADI JIMBONI KIKWAJUNI

MPALULEBLOGS:
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi wa Operesheni za Kiufundi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar, Maulidi Hassan Khamisi(kulia), bomba za pampu ya maji itakayotumika kuunganisha mtandao wa maji .Mradi huo una umbali wa kilomita 3.5. ukiwa na lengo la kutatua kero ya maji jimboni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiangalia mafundi wakiweka tuta barabarani wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa barabara katika jimbo hilo ikiwa na lengo la kutimiza ahadi za ujenzi wa barabara kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mhandisi wa Mradi wa Uwekaji wa Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, Ephantus Mathi (kushoto)kutoka Kampuni ya Central Electrical, akitoa maelezo juu ya mradi huo kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia). Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salum Jazeera.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wataalamu wa Mradi wa Uwekaji Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni.
Mafundi kutoka Kampuni ya Central Electrical wakiendelea na uwekaji wa nyaya za umeme katika moja ya nguzo ya taa katika mitaa ya Jimbo la Kikwajuni ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi za Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni.