TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, April 27, 2012

FRANCIS CHEKA NA MADA MAUGO WAPIMA UZITO TAYARI KWA MPAMBANO WAO


WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wamewapima uzito   na bondia  Mada Maugo  na  Na Francis Cheka wote wamekutwa na kilogramu 76.5 ambapo mpambano wao utafanyika Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.
“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D.

Thursday, April 26, 2012

Benki ya NBC yaandaa mkutano wa masuala ya kuchumi

Maofisa wa ABSA Capital ambayo ni sehemu ya Benki ya ABSA ya Afrika Kusini wakiwa katika  mkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA Capital jijini Dar es Salaam jana jioni. Katikati ni Ridle Markus, Jeff Gable (kushoto), Pius Tibarazwa (wa pili kushoto) wa NBC Tanzania na Michael Keenan (kulia) wa ABSA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kulia) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo wa makampuni katika mkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA Capital ambayo ni sehemu ya Benki ya ABSA ya Afrika Kusini jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kushoto) akimsikiliza mmoja wa maofisa wa  ABSA Capital ambayo ni sehemu ya benki ya ABSA ya Afrika Kusini, Jeff Gable,  katika mkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA Capital kwa wateja wa makampuni wa NBC, jijini Dar es Salaam jana jioni. Wa pili kushoto ni Mohamed Sayed wa ABSA Capital na Mkuu wa Idara ya Fedha na Masoko wa NBC, Pius Tibarazwa.
Mkuu wa Idara ya Fedhana Masoko wa  Benki ya NBC Tanzania, Pius Tibarazwa (kushoto) akizungumza na mmoja wa maofisa wa ABSA Capital ambayo ni sehemu ya Benki ya ABSA ya Afrika Kusini, Jeff Gable katika mkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA
Capital kwa wateja wa makampuni wa NBC, jijini Dar es Salaam jana jioni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (katikati)akisalimiana na baadhi ya wateja wa makampuni wa benki hiyo katikamkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA Capital ambayo ni sehemu ya Benki ya ABSA ya Afrika Kusini jijini Dar
es Salaam jana jioni.

CHEKA AMUWEKA KIPOLO KASEBA KUKUTANA SIKU YA SABASABA


 Bondia Japhet Kaseba  katikati akisaini mkataba kabla ya pambano lake na bondia Francis Cheka.
Bondia  Francis Cheka kushoto akisaini mkataba kabla ya pambano lake na bondia  Japhet Kaseba.
Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro  amesaini mkataba wa kupigana na  bingwa wa kick Boxing. Japhet  Kaseba   katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Cheka amesema anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mchezo wa masumbwi na mabondia wengi wanamtaka   kupigana  na yeye.
Najua mabondia wa hapa bongo kila mtu anataka kucheza na mimi tu wanajua mimi ndio nalipa kwa soko la bongo na nitahakikisha kila anaekuja mbele yangu namtandika kifupi Tanzania akuna bondia mwenye uwezo zaidi yangu alisema Cheka.
Kaseba nilimpiga kwa K.O tareha 3 October 2009 nilimpinga anataka tena wembe kwa ngua ngumi ni sehemu ya maisha yangu siwezi kukataa na mimi ndio napata ridhiki yangu humu hivyo nitahakikisha anaekuja mbele yangu namtwanga tu bila huruma nitaanza na Mada Maugo 28 April na huyo namuweka kama kipolo

Nae Promota wa mpambano huo Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni mpambano ambao aujawai kutokea kwa kuwa mabondia hao wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya Nchi
Mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae;

MOHAMED MTONGA: HAKUTATOKEA UBADHIRIFU TENA WIZARA YA FEDHA


NA MWANDISHI WETU
 
WIZARA ya Fedha nchini imesema baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu  wa Serikali (CAG), kubaini matumizi mabovu ya mishahara hewa na mikataba mibovu, wizara hiyo haitarajii  kujitokeza tena kwa ubadhirifu huo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Mohamed Mtonga wakati akifufunga semina ya siku nne ya maodita wa ndani jijini Dar es Salaam leo.
Alisema lengo la semina kwa washiriki hao ili kuwa ni kuwajengea uwezo ambao utawasaidia katika kazi zao haswa  kudundua maeneo hatarishi ya upotevu wa fedha.
Mtonga alibainisha kuwa mafunzo hayo yawasaidia kubaini matumizi yasiyo ya kawaida kwa haraka kwa kuwa wizara imeanzisha mfumo mpya kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa njia ya kompyuta.
Alisema teknolojia hiyo ya kisasa ambayo inauwezo wa kugundua makosa hayo haraka katika maeneo mbalimbali, hivi sasa inatumiaka katika nchi ya Kenya ambapo imefanikiwa kwa kiwango cha juu.
Mtonga alisema kutokana na mafanikio ya nchi hiyo, Tanzania imeamua kuwapeleka maodita wake wanne (4), kwenda kujifunza teknolojia hiyo ambapo itaanza kutumika hivi karibuni hapa nchini.
Aidha, alisema Wizara ya Fedha imetoa muongozo unaowataka kila Katibu Mkuu wa Wizara kufanya uchunguzi katika kubaini maeneo hatarishi katika ofisi zao kitendo kitakacho wasaidia kugundua haraka  ubadhirifu wa mishahara hewa na mikataba bandia kwa kutumia teknolojia hiyo.
Cheo hicho cha Mkaguzi Mkuu wa Ndani kimeanzishwa kisheria hivi karibuni kwa ajili ya kuboresha na kuongeza nguvu katika kazi za ukaguzi wa fedha ambapo hapo awali hakikuwepo. 

  POLISI WAPIGWA FAINI MIL 1/- KILA MMOJA


 
 
Kamati ya Ligi ya TFF imewafungia mechi tatu na kuwapiga faini y ash. milioni mmoja kila mmoja wachezaji tisa wa timu ya Polisi Dodoma baada ya kumpiga mwamuzi Martin Saanya kwenye mechi dhidi ya Azam iliyochezwa Aprili 14 mwaka huu mjini Dodoma.
Wachezaji hao walioadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 25(g)(iii) ni Noel Msekwa, Frank Sindato, Abdallah Matila, Bantu Admin, Salmin Kisi, Madope Mwingira, Sihaba Mkude, Kaliyasa Mashaka na Ibrahim Massawe.
Iwapo wachezaji hao watahama Polisi na kujiunga na timu nyingine, watahama na adhabu zao.
Vilevile timu ya Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri. Pia timu hiyo imepewa barua ya onyo kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi dhidi yao na Yanga iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MTIBWA SUGAR YAPOTEZA MECHI DHIDI YA AZAM


Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemuondoa mwamuzi Rashid Msangi wa Dodoma kwenye orodha ya waamuzi kwa kuvuruga mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyochezwa Aprili 23 mwaka huu.
Pia waliokuwa waamuzi wasaidizi wa mechi hiyo; Samuel Mpenzu na Abdallah Uhako wote kutoka Arusha nao wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Vilevile Kamati imeipa Azam ushindi wa mabao 3-0 kwa mujibu wa Ibara ya 31 ya Kanuni za Nidhamu za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). Kwa mujibu wa kanuni hiyo, timu itakayohesabika kupoteza mechi (Mtibwa Sugar) itakuwa imefungwa mabao 3-0.
Kwa mujibu wa Kanuni ya Ligi Kuu ya Vodacom kifungu cha 22(3-6) Mtibwa Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000, imepoteza mapato yote ya mchezo huo na inatakiwa kulipa faini hiyo kabla ya mechi inayofuata.
Nao makamishna watatu; Abdallah Mitole wa Dar es Salaam, William Chibura (Musoma) na Omari Mawela (Mwanza) wameondolewa kwenye orodha ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kushindwa kufika kwenye mechi walizopangiwa kusimamia bila taarifa.
Makamishna hao wametakiwa kutoa maelezo ya maandishi wakieleza sababu za kutofika kwenye mechi. Mechi walizokuwa wamepangia ni Coastal Union vs Ruvu Shooting (Mitole), Kagera Sugar vs Yanga (Chibura) na Kagera Sugar vs African Lyon (Mawela).
Nayo Moro United imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya wachezaji wake kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadirishia (dressing rooms) wakati wa mechi namba 171 kati yao na Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 8(16).
Pingamizi la Villa Squad dhidi ya African Lyon kuwa wakati wa mechi yao ilitumia wachezaji wawili (Mohamed Samata na Benedict Jacob) ambao mikataba yao imemalizika limetupwa kwa vile wana leseni halali za kucheza ligi.
Pia mwamuzi wa mechi namba 160 kati ya Moro United na Oljoro JKT, Nathaniel Lazaro wa Kilimanjaro amefungiwa miezi sita na kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa kutozingatia kutunza muda kwa mujibu wa kanuni ya 26(1)(f).
Vilevile Kamishna wa mechi ya Moro United na Oljoro JKT, Ali Mkomwa wa Pwani na Said Mnonga wa Mtwara aliyekuwa mwamuzi msaidizi mechi kati ya Villa Squad na Coastal Union wameandikiwa barua za onyo wakitakiwa kuwa makini kwenye michezo wanayosimamia.

MECHI YA TWIGA STARS, ZIMBABWE YAFUTWA

 
Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) na Zimbabwe iliyokuwa ichezwe keshokutwa (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imefutwa.
Uamuzi huo umefanywa na Chama cha Mpira wa Miguu Zimbabwe (ZIFA) ambayo sasa imeamua kucheza mechi ya kirafiki na Zambia. Mechi hiyo itachezwa Aprili 28 mwaka huu jijini Harare.
Twiga Stars inaendelea na mazoezi chini ya kocha wake Charles Boniface Mkwasa katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) iliyoko Ruvu mkoani Pwani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na jitihada za kuitafutia mechi za kirafiki Twiga Stars kabla ya kucheza mechi ya mashindano dhidi ya Ethiopia ambayo itafanyika Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa.

HARAIKI YA WANAFUNZI YAPAMBA SHEREHE ZA MUUNGANO WA TANZANIA.

(NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO)
DAR ES SALAAM
Haraiki ya  wanafunzi wapatao  1,727 kutoka shule za msingi mbalimbali Tanzania bara na visiwani  wameipamba vizuri sherehe ya maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika  leo katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kati ya wanafunzi hao, ni wanafunzi 727 ambapo 500 wanatoka Tanzania bara, 200 Tanzania visiwani na 27 ni mahodari wa kucheza sarakasi ambao waliingia uwanjani na kutengeneza maumbo mbalimbali pamoja na kuimba wimbo maalumu uitwao Uamuzi wa Busara.
Maumbo yaliyotengenezwa na haraiki hiyo ni pomoja na bendera ya taifa, herufi zenye  umbo la miaka 48 ya Muungano, na maumbo ambayo ndani yake walicheza salakasi na ngoma za asili za ndalandala kutoka Tanzania bara na chaso kutoka Zanzibar.
Maumbo mengine ni pamoja na madini ya Tanzanaiti ambayo hayapatikani sehemu yoyote duniani zaidi ya Tanzania na maumbo ya mazao ya uchumi ya katani na pamba yanayolimwa Tanzania bara na karafuu Tanzania visiwani.
Haraiki hiyo imeandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na wakufunzi wake ni Kilema Athuman Kambangwa akisaidiwa na Mwalimu Grace Ernest Kabohora kutoka shule ya msingi Wailesi katika manispaa ya Temeke.
Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa ni Rasi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kauli mbiu ni “Shiriki kikamilifu katika Sensa na mchakato wa Mabadiriko ya Katiba”.(Mwandishi Shaaban Mpalule)

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA WANANCHI MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipunga mkono kusalimia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Aprili 26, 2012 katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wananchi wakati alipokuwa akiingia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuongoza maadhimisho ya mika 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo asubuhi (Picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipowasili katika uwanja wa Uhuru kuongoza sherehe za Muungano zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.
Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo (Picha na Freddy Maro)
Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Baadhi ya Viongozi wa Kiserikali wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Uhuru, wakisimama wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Jakaya Kikwete, akisalimiana na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Aprili 26, 2012 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo leo.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo leo.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa pole na haraka, wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo leo.
Watoto wa shule mbalimbali za msingi wanaounda kikundi cha alaiki, wakionyesha manjonjo ya michezo na maumbo mbalimbali wakati wa sherehe hizo leo.
 
Kikundi cha Sanaa cha JKT Oljoro, kikionyesha umahiri wake wa kuimba na kucheza 'Kiduku' wakati wa sherehe hizo.

ANGALIA PICHA ZA MAADHIMISHO YA MUUNGANO


 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akipunga mkono kusalimia wananchi wakati akiingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za maadhimisho ya Miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais na amiri jeshi mkuu akikagua gwaride leo asubuhi.(Picha kutoka IKULU)

Wednesday, April 18, 2012

Matumizi ya ardhi yashirikishe jamii

MIGOGORO ya ardhi imeendelea kuzikumba jamii nyingi katika maeneo mbalimbali nchini hivyo kusababisha migogoro.
Jamii inatumia muda mwingi kutatua migogoro hiyo badala ya kufanya shughuli za maendeleo.

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba, ardhi ndio tegemeo kubwa kwa jamii za wakulima na wafugaji ambao ndio sehemu kubwa ya Watanzania.

Ardhi ndio mtaji pekee ambao Watanzania wengi waishio vijijini wanaitegemea kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kuweza kuwapatia chakula na kipato.

Licha ya kuwepo kwa mamlaka zinazohusika na usimamizi pamoja na ugawaji wa ardhi, migogoro hiyo imeendelea kuwa sehemu ya maisha kwa jamii nyingi.

Kama sheria za usimamizi na umiliki wa ardhi zipo, kitu gani kinasababisha migogoro ambayo inagharimu maisha na mali za Watanzania wasio na hatia?

Sisi tunasema kuwa, sheria za ardhi zinatoa haki ya kutumia ardhi na si kuimiliki hivyo inatosha kumhakikishia mtu kuwa, kitu chochote ambacho atakiendeleza katika ardhi husika, kitalindwa kwa maslahi yake si lazima kumwambia ardhi hiyo ni yako ili aiendeleze.


Migogoro ya ardhi husababishwa na mambo mbalimbali ambayo baadhi yake ni upungufu katika sheria za ardhi, mamlaka zinazohusika na ugawaji wa viwanja kugawa kiwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja na fidia ndogo.

Licha ya kufanyika marekebisho katika sheria za kusimamia matumizi ya ardhi, bado migogoro hiyo imeendelea kuchukua nafasi miongoni mwa jamii nyingi za Kitanzania.

Upo umuhimu mkubwa wa kushirikisha jamii katika kufanya maamuzi yanayohusu matumizi ya ardhi. Kama wananchi watashirikishwa, migogoro mingi iliyopo vijiji itapungua.

Ipo tabia ya baadhi ya Halmashauri za vijiji, kupitisha taarifa feki inayoamua matumizi ya ardhi ya kijiji bila ridhaa ya wananchi.

Serikali nayo inachangia migogoro hii pale inaposhindwa kulipa fidia kwa wananchi baada ya kutwaa ardhi kwa ajili ya kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Umefika wakati wa wananchi kuelimishwa juu ya sheria mbalimbali za ardhi ili watambue haki na wajibu wao katika suala zima la umiliki na matumizi ya yake.
Posted: 15 Apr 2012 11:41 PM PDT

Na Pendo Mtibuche, Dodoma

HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma, bado inakabiliwa na tatizo la mimba katika shule mbalimbali za msingi na sekondari.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Bi. Betty Mkwasa, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wadau wa elimu na kujadili changamoto zinazowakabili wanafunzi.

Alisema tatizo la mimba na utoro kwa wanafunzi limekuwa sugu na kuwaomba wadau hao, waone umuhimu wa kulitafutia ufumbuzi.

Bi. Mkwasa alisema tatizo hilo linatokana na changamoto mbalimbali za baadhi ya wanafunzi wa sekondari kutembea umbali mrefu, kukosekana kwa hosteli na zile zilizopo nyingi hazitambuliki 'bubu' na hazina ulinzi kwa watoto hao.

Aliongeza kuwa, wanafunzi wengi wa kike wanaosoma sekondari wamepanga mitaani ambapo nyumba wanazoishi si salama kwa maisha yao jambo linalosababisha baadhi ya wasichana kuingia kirahisi katika vishawishi.

“Halmashauri hii pia inakabiliwa na tatizo kubwa la utoro kwa wanafunzi shuleni hivyo kusababisha wale wanaofaulu shule ya msingi kwenda sekondari, kutoripoti shuleni na hawafuatiliwi.

“Kutokana na hali hii, nawaagiza Watendaji wa Kata na Vijiji, kuhakikisha mnawafuatilia wanafunzi watoro na kuwachukulia hatua wazazi au walezi wa wao,” alisema Bi. Mkwasa na kusisitiza kuwa, suala la miundombinu katika shule mbalimbali za msingi na sekondari hairidhishi.

Alisema halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa nyumba za walimu, matundu ya vyoo kwa shule mbalimbali na thamani za shule hivyo aliwaomba wadau hao kutafuta ufumbuzi.
Posted: 15 Apr 2012 11:38 PM PDT
Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bw. Matina Nkurlu (katikati), akionesha nambari ya Mshindi wa Droo kubwa ya mwezi ya kumpata mshindi wa promosheni ya M-PESA, ambapo mkazi wa Kitangiri mkoani Mwanza, Bw. Revocatus Mkama, alishinda na kupata sh. milioni 10. Kushoto ni Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Bakari Maggid na Mtaalamu wa huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom, Bi. Reenu Verma. (Na Mpigapicha Wetu)
Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam  KA M P U N I y a Ma w a s i l i a n o y a Vodacom Tanzania  imepunguza gharama  zake za kutoa fedha kwa kupitia  huduma yake ya M-Pesa hadi
asilimia 20 kwa mteja anapotoa  fedha kwa wakala yeyote wa  huduma hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Vodacom, Bw. Rene Meza alisema
gharama hizo zimepunguzwa  rasmi kuanzia leo kwa wateja wa Vodacom sasa wanao uwezo wa kutoa fedha kutoka kwa wakala yeyote nchini na watatozwa kwa hizi gharama mpya na nafuu zitakazosaidia zaidi shughuli za kiuchumi na kijamii za watu waliosajiliwa na hudu ma ya Vodacom M-Pesa.
"Tunaelewa hali ya uchumi nchini na tunafahamu jinsi M-Pesa  ilivyokua huduma muhimu na bora katika maisha ya kila siku ya Watanzania, Hivyo tumeamua kuifanya iwe nafuu zaidi na rahisi kwa wateja wetu," alisema
Mkurugenzi huyo katika taarifa iliyotolewa ya kutambulisha
gharama mpya za kutoa fedha.
Alisema upunguzaji huu umekuja miezi michache baada ya
kampuni ya kupunguza gharama za kutuma fedha na kuwa ndogo kwa kiasi cha kuanzia sh. 50 kwa muamala na kuzindua promosheni ya siku 90 iitwayo 'Tuma na Ushinde' ambapo sh. milioni 480 zitashindaniwa kwa kipindi chote
cha promosheni.
Alisema jukumu letu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu
wana furaha na wanajiwezesha kupitia huduma ya M-Pesa.
Tutaendelea kuboresha bidhaa na huduma zetu ambazo tunatoa kwenye M-Pesa ili kuhakikisha umuhimu kwa maisha ya kila siku ya wateja
Posted: 15 Apr 2012 11:32 PM PDT
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Kawe Bi. Halima Mdee (CHADEMA) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Bi. Ester Bulaya (CCM) wameamua kujitokeza kumsaidia msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayetuhumiwa kumuua aliyekuwa mwigizaji marehemu Steven Kanumba.
Wabunge hao juzi waliamua
kwenda kumuona Lulu na kwa sasa
wameamua kuendesha kampeni ya
kuchangisha fedha za malazi kwa
ajili ya familia yake.
Bi. Mdee kupitia ukurasa wake wa
mtandao wa kijamii Twitter alisema
Lulu anahitaji mwanasheria makini
wa kuweza kumnasua kwenye kesi
hiyo akiwemo Mwanasaikolojia wa
kuzungumza naye ili aweze kuwa
vizuri kiakili.
Mbunge huyo wa Jimbo la Kawe
aliandika katika ukurasa huo kuwa
“Leo (mwishoni mwa wiki) mimi
na Mheshimiwa Bulaya tulikwenda
kumuona Lulu Oysterbay Polisi.
‘She really needs our support’ (
kwa kweli anahitaji msaada wetu).
Kwanza ‘she is only 17’ (kwanza
huyu ni binti wa miaka 17 tu).
“Pili anahitaji sana psychological
support (msaada wa kisaikolojia).
Nawaomba watu wenye taaluma
hiyo wasisite kwenda kumuona.
Wasiliana na 0714282527 Steve
Nyerere. Tatu anahitaji wanasheria
makini wa kumsaidia na kwa
yeyote ambaye yuko tayari naomba
awasiliane nami 0759 569823
(Halima Mdee). Nne, at that
tender age (kwa umri huo Lulu)
ndio alikuwa anategemewa na
familia yake. Now (sasa) yuko
ndani matatizo yamezidi kuwa
makubwa.
“Kwa yeyote anayeguswa,
naomba atume chochote kwenye
namba hii 0754 878890 ni namba
ya M-Pesa ya mama yake tumsaidie
huyu mtoto!...”Again (tena)..
namba ya M-PESA kwa wanaotaka
kumsaidia Binti yetu Lulu ni
+255754878890. Ni namba ya
mama yake,” aliongeza Bi.Mdee.
Posted: 15 Apr 2012 11:29 PM PDT
Na Mwandishi Maalum,
Ikulu Zanzibar SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kulinda uhuru wa dini zote lakini haitavumilia vitendo vyovyote vya uvunjaji wa sheria vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa jina la dini huku ikisisitiza uadilifu kwa viongozi wa dini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo -jana katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya kumweka wakfu Askofu wa 10 wa Dayosisi ya Zanzibar Michael Henry Hafidh.
Alisema, ustawi wa dini mbalimbali Zanzibar unahusika
na Sera ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya uhuru wa kuachia kanisa kuendesha seminari zao na makongamano yao bila ya kuingiliwa.
Alieleza kuwa, kwa kiasi kikubwa shughuli hizo za kidini zimekuwa zikiendeshwa kwa amani ambapo kwa bahati mbaya pamoja na hayo kumekuwepo nyakati ambapo
kutofahamiana kumejitokeza katika baadhi ya  akongamano.
"Serikali imeweka utaratibu maalum wa utoaji ruhusa wa
makongamano hayo, taratibu hizo ni pamoja na utunzaji wa amani nakutobughu dhiana kidini‚ tuelewe sote kwamba viongozi wa dini ni walimu na walezi wa jamii na anadhamana kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu," alisema Dkt.Shein.
Aidha, alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kufanya kila linalowezekana kulinda haki za Watanzania katika kufuata dini na kuabudu dini waitakayo na kuishi bila ya kubaguliwa kutokana na sababu ya dini, kabila au rangi.
Alisema, hakuna budi wananchi wote kwa pamoja kujivunia na kuiendeleza hali ya amani na utulivu iliyopo hapa nchini ambapo ziko nchi mbalimbali wamekuwa wakikosa hali hiyo kwa sababu ya migogoro inayotokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kidini, kisiasa na kikabila, Pamoja na hayo Dkt. Shein alisema kuwa licha ya kuwa Tanzania haina dini ya serikali kama ilivyokuwa ikisisitizwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wa amamu zilizofuata lakini Watanzania wengi ni wafuasi na waumini wa dini zenye madhehebu tofauti.
Kutokana na hilo Dkt. Shein alisisitiza jukumu la kulinda
heshima baina wananchi na usalama wa nchi linategemea sana mafunzo yanayofundishwa na yanayohutubiwa na viongozi katika nyumba za ibada.
Pia, alisisitiza viongozi wa dini mbalimbali wana wajibu
wa kuhakikisha sehemu za ibada zinatumika kwa ibada tu bila ya kuingiza mambo mengine na kutoa mwito kwa Jumuiya zote za kidini na wananchi kuendelea kuheshimiana na kuishi bila ya kubaguana.
"Sote tuwe na lengo moja la kuiletea maendeleo nchi yetu kwa manufaa ya watu wake wote,” alisema Rais.
Pia Dkt. Shein aliwaeleza waumini hao kuwa mambo yao
waliyomueleza ameyasikia na atayafanyia kazi.
Posted: 15 Apr 2012 11:27 PM PDT
Na Pamela Mollel, Manyara
 SHUGHULI za uchimbaji wa madini katika Kitalu D eneo la Mererani wilayani S ima n j i r o Mk o a wa
Manyara umesimamishwa kwa muda na Ofisi ya Madini Kanda ya Kaskazini baada ya kuibuka kutoelewana kwa wamiliki wa mgodi huo.
Mg o d i u l i o s imami s hwa
unamilikiwa na wakazi wawili
wa mkoani Arusha ambao ni
Bw.Kitinda Kimaro pamoja na
Anthony Ngoo ambapo ulipewa
leseni ya uchimbaji yenye namba
PML No.0003601 miaka iliyopita.
Kwa mujibu wa vyanzo vya
habari vilivyolifikia gazeti hili kwa
masharti ya kutokutaka majina
yao yaandikwe magazetini vilidai
kwamba ofisi hiyo imesimamisha
kwa muda wa mwezi mmoja
shughuli za uchimbaji katika mgodi
kuanzia Machi 26 mwaka huu hadi
Mei 3, mwaka huu.
Vyanzo hivyo vya habari vilieleza
kuwa lengo la kusimamishwa kwa
shughuli hizo za uchimbaji katika
eneo hilo, lililenga kutoa muda kwa
pande mbili zinazovutana kutafuta
suluhu ya namna ya kufanya kazi
kwa maelewano.
Hata hivyo, Majira ilifanikiwa
kupata nakala ya barua ya
kusimamisha shughuli za uchimbaji
katika mgodi huo yenye Kumb.Na
DA 74|503|VOL II|160 ya Machi
26 mwaka huu iliyoandikwa na
kusainiwa na Ofisa Madini Mkazi
wa Mererani mkoani Manyara
Injinia L .P Mayala.
Katika barua hiyo ambayo nakala
imepelekwa moja kwa moja kwa
Kamishna Msaidizi wa Madini
Kanda ya Kaskazini, Mkuu wa
Kituo cha Polisi Machimboni
pamoja na kwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Usuluhishi na Usalama
ilitaka pande mbili kuwasilisha
mapendekezo wa kufanya kazi
kwa maelewano mnamo Aprili 3,
mwaka huu.
Ha t a h i v y o , g a z e t i h i l i
lilipowasiliana na Kamishna wa
Madini Kanda ya Kaskazini,
Bw.Benjamin Mchwapaka alikiri
ofisi yake kusimamisha kwa muda
shughuli za uchimbaji katika mgodi
huo huku akisema kuwa wanasubiri
maagizo waliyoyatoa kwa pande
zote mbili yatekelezwe hadi pale
watakapokutana tena.
Alisema kwamba, pande mbili
zinazovutana katika mgodi huo
endapo zisipoweza kukubaliana ofisi
yake itachukua maamuzi magumu
kwa kuzingatia maslahi ya pande
zote huku akikataa kuzungumzia
maamuzi yatakayochukuliwa.
Posted: 15 Apr 2012 11:21 PM PDT
Kiungo wa Manchester United, Michael Carrick (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Aston Villa, Gabriel Agbonlahor katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyochezwa jana Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester. (AFP)
Posted: 15 Apr 2012 11:18 PM PDT
Na Elizabeth Mayemba
VINARA wa Ligi Kuu Simba, jana waliendeleza ubabe katika mechi za ligi hiyo baada ya kuinyuka Maafande wa Ruvu Shooting bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Bao la Simba lilifungwa dakika ya 80 kupitia kwa Patrick Mafisango ambaye alipokea pasi ya Haruna Moshi 'Boban'.

Kwa ushindi huo Simba imeendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 53, ikifuatiwa na Azam FC ambayo imefikisha pointi 50.

Simba ilianza kwa kishindo mechi hiyo, ambapo dakika ya saba Salum Machaku akwa na kipa wa Ruvu alishindwa kuiandikia bao timu yake baada ya kuchelewa kupiga shuti na kuwahiwa.

Dakika ya saba Simba ilikosa bao lingine kupitia kwa mshambuliaji wake Gervas Kago ambaye kabla ya kupasiwa Boban Na Victor Costa 'Nyumba' waligongeana na vyema lakini, Kago akashindwa kutumbukiza mpira kimiani.

Baada ya kosa kosa hizo, Ruvu Shooting ilizinduka dakika ya 18 Mohamed Kijuso akiwa na kipa Juma Kaseja alishindwa kutumbukiza kimiani baada ya kuwahiwa na Costa.

Kipindi cha pili Ruvu Shooting walionekana kuimarika na dakika 48, Abdallah Juma ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Kijuso alishindwa kufunga akiwa na wavu huku kipa Kaseja akiwa ametoka golini.

Katika kipindi hicho Simba iliwatoa Kago na Machaku na kuwaingiza Uhuru Selemani na Edward Christopher.

Dakika ya 78 Mafisango alikosa bao la wazi baada ya kupasiwa pasi murua na Uhuru Selemani, lakini hata hivyo badala ya kufunga akapaisha mpira juu.

Sunday, April 15, 2012

DIAMOND ASHINDA TUZO TATU KWA MPIGO KILIMANJARO MUSIC AWARD 2012

 Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utunzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora  Kilimanjaro Music Award 2012 zinazofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania  na nje ya nchi.

Msanii  Nassib Abdul ‘Diamond’ usiku huu ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award, baada ya kujinyakulia tuzo tatu.
“Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo ninachukua tuzo ya tatu sasa hivi, alisema Diamond baada ya kushinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka, kupitia wimbo Moyo Wangu, ambayo ilikuwa ya tatu usiku huu.
Diamond alizishinda nyimbo za Hakunaga ya Suma Lee, Wangu ya Jay Dee, Ndoa Ndoana ya Kassim na Bongo Fleva ya Dully Sykes.
 Mwanamuziki Diamond akipiga picha na mama yake wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kutoka kulia pamona na wanenguaji wake mara baada ya kupokea tuzo yake ya utuzni bora wa nyimbo.
 Mwimbaji wa muziki wa Taarab ambaye ameshinda tuzo ya mburudishaji bora kwa wanawake Malkia Khadija Omar Kopa akitumbuiza katika hafla hiyo usiku huu.
 Malkia Khadija Omar Kopa akishukuru wapenzi wake mara baada ya kushinda tuzo ya mburudishaji bora, wa pili kutoka kushoto ni mume wake na wengine ni watoto wake.
 Watoto wa Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa wakishuka jukwaani mara baada ya kumtunza mama yao wakati alipokuwa akitumbuiza katika hafla hiyo.
 Kulia ni Msanii Profesa Jay na kushoto ni Mkubwa Fella meneja wa kundi la TMK Family wakimkabidhi tuzo Roma Msanii wa muziki wa Hiphop aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa Hiphop.
 Burudani kutoka THT zikiendelea
 Burudani zikiendelea kwa nguzu zote.

MAMBO YANAZIDI KUPAMBA MOTO TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARD 2012 MLIMANI CITY USIKU HUU


 Mwanamuziki Diamond katikati akiwa jukwaani na wenzake kabla ya kuimba wimbo wa msondo katika hafla ya kukabidhi tuzo za wanamuzikii bora za Kilimanjaro Music Award zainazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam kulia ni Khalid Chokoraa wa bendi ya mapacha watatu.
 Msanii HBaba akiwa amezungukwa na vimwana katika hafla hiyo
 Mtayarishaji wa muziki P. Funk kulia akiwa na msanii wa muziki wa Hiphop Jay Moo.
 Wakurugenzi wa ASET kutoka kulia ni Asha Baraka akiwa na kaka yake Baraka pamoja na mdau mwingine katika hafla hiyo.
 Kulia ni Dina Marios wa Clouds akiwa na Asma Makau kutoka Clouds pia.
 Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu kulia akibadilishana mawazo na Mulamu Ghambi katika hafla hiyo.
Mohamed Nasor kushoto akiwa na Evance Aveva wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo usiku huu.

UTOAJI WA TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARD 2012 moto MOTO USIKU HUU MLIMANI CITY

Mwanamuziki Ali Kiba akitoa shukuranbi zake kwa mashabiki wa muziki  mara baada ya kutangazwa mshindi katika tuzo za muziki za Kilimanjaro Music Award zinazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo ameshinda kwa wimbo wake unaoitwa Dushelele
Mwmnamuzki Ali Kiba akipokea tuzo yake kutoka kwa Mtangazaji wa Clouds Dina Marios mara baada ya kutangazwa mmoja wa washindi katika tuzo hizo, kushoto ni mtangazaji wa ITV na Radio One Rainfredy Masako
Kundi la THT likitumbuiza katika tuzo hozo usiku huu.
Wadau wakiwa katika hafla hoiyo ya kutoa tuzo za muziki kutoka kulia ni Steven Nyerere mchekeshaji, Meneja huduma kwa wateja wa Multchoice Ronald Shelukindo, Frank Mgoyo na wadau wengine.
Mchekeshaji Steve Nyerere akiwa katika picha ya pamoja na Sinta mwigizaji wa zamani.
Kulia ni Taji Liundi na mbunifu wa mavazi Asia Idarous wa Khamsini.
Mdau Kelvin Twisa ndani ya nyumba pia.
Meneja wa kinywaji cha Redds Vicktoria  Kimaro akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Kutoka kushoto ni wadau Benny Kisaka, Mabakila, Evance na Juma Pinto.
Kulia ni Oscar Shelukindo na kushoto ni Kabula Nshimo kutoka TBL na wadau wengine wakiwa katika hafla hiyo.
Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro George Kavishe kulia na Mumongae kutoka TBL.
Kutoka kulia ni mdau Henry Mdimu, na kushoto ni Juddy Moshi.
Mdau Nick Butty yupo ndani ya nyumba pia.