TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 28, 2013

ASASI YA “NEW LIFE IN CHRIST” YAKABIDHI MISAADA MBALIMBALI YA KIBINADAMU KWA WAFUNGWA WALIOPO MAGEREZANI LEO MKOANI KILIMANJARO

1 Mkurugenzi wa Doricas Aide International – Tawi la Tanzania, Bi. Stella Sozigwa(kushoto) akikabidhi Misaada ya Kibinadamu ya Wafungwa Waliopo Magerezani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja. Hafla fupi ya Makabidhiano ya Misaada hiyo imefanyika leo Desemba 27, 2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.2 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi wakati wa hafla ya kupokea Misaada ya Kibinadamu kwa Wafungwa waliopo Magerezani iliyotolewa na Asasi ya “New Life In Christ” leo Desemba 27, 2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.3  
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wa Gereza Kuu Karanga – Moshi wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati wa Makabidhiano ya Misaada ya Kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani iliyotolewa na Asasi ya “New life In Christ”.4  
Aina mbalimbali ya Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa kwa Wafungwa waliopo Magerezani na Asasi ya “New Life In Christ”. Hafla ya Makabidhiano ya Misaada hiyo imefanyika leo Desemba 27, 2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.5 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wawakilishi wa Asasi ya “New Life In Christ” mara baada ya kupokea Misaada ya Kibinadamu ya Wafungwa waliopo Magerezani (wa tatu kulia) ni Mwenyekiti wa New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bi. Elly Makyao(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Doricas Aide International – Tawi la Tanzania, Bi. Stella Sozigwa(wa tatu kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Magereza, Hamis Nkubasi na wa kwanza kulia ni Mratibu wa Huduma za Magereza toka Asasi ya “New Life In Christ”, Bw. Charles Shang’aa(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

ASHANTI, JKT RUVU KUJARIBU TIKETI ZA ELEKTRONIKI JAN 1!!

DSC_0125 
Moja ya Kikosi cha JKT Ruvu ya Pwani katika mechi za nyuma. Picha Maktaba
Timu za Ligi Kuu za Ashanti United na JKT Ruvu Stars zinapambana Januari Mosi mwakani kati moja ya mechi za kujaribu matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamzi, Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 1,000 na sh. 2,000 ambapo tiketi zinapatikana kupitia M-Pesa na mawakala wa CRDB Fahari Huduma. Tiketi zitaendelea kuuzwa hadi kipindi cha kwanza cha mechi hiyo kitakapomalizika. 
Mawakala 18 wa Fahari Huduma wanaouza tiketi hizo ni ABC Computer- Mtaa wa Samora, Abraham Anangisye Mwampetele- Maji Matitu, Apex Security Services- Mtaa wa Mibega, Kinyerezi, Athuman Fakhi Adam- Kongowe Mbagala, Fedha Investment Limited- Pamba Road na Fuya Godwin Kimbita- Tegeta Block.
Ghomme Health & Education Limited-Bahari Beach, Herman Arbogast Tarimo- Kigamboni, K- Finance Limited- Shekilango, Sinza, Koli Finance Limited- Mtaa wa Samora, LB Pharmacy- Mtoni Kijichi, Lista Phares Barnabas- Tabata Segerea na Maly Investment Company Limited- Mtaa wa Sikukuu, Kariakoo.
Wengine ni Micu Enterprises- Mtaa wa Congo, Kariakoo, S&D Collection Company Limited- Mikocheni, Shoppers Plaza, Therry Investment Limited- Tegeta Kibaoni, TSHS Distributors Limited- Mtoni kwa Aziz Ali na Wemerick Independent Vehicle- Mtaa wa Boko.
Pia mshabiki anaweza kununua tiketi kwa njia ya simu- mtandao wa Vodacom kwa kupiga *150*03*02# ambapo atapata namba atakayoitumia kufanya malipo kupitia MPESA. Katika MPESA namba ya malipo kwa TFF ambayo ndiyo mshabiki ataitumia kufanya malipo ya tiketi (business number) ni 888800. Vilevile mteja wa CRDB aliye katika mtandao anaweza kufanya malipo kupitia CRDB simbanking.
Baada ya kufanya maombi kupitia njia yoyote ya hizo tatu; MPESA, Fahari Huduma na CRDB simbanking, mshabiki atapata namba ambayo ataitumia ku-print tiketi yake kupitia mashine maalumu za kuchapia Tiketi ya TFF zilizo katika ATM za CRDB kwenye maeneo yafuatayo;
Benki ya CRDB tawi la Azikiwe, tawi la Holland House ambapo kuna mashine mbili, tawi la Vijana, tawi la Kariakoo, ATM ya Mtaa wa Shaurimoyo ambapo kuna mashine mbili na ATM ya CRDB iliyoko kituo cha mafuta cha Kobil Sabasaba, Mtoni kwa Aziz Ali.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF

Lipumba: Hali ya uchumi ni mbaya, Serikali ichukue hatua

uchumi 
Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza na waandishi wa Habri jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa tamko la kulaani kwa kitendo cha Naibu Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwazalilisha Wabunge wa upinzani akiwepo Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Picha na Venance Nestory 
…………………………………………………………………………………
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka wa matatizo ya kiuchumi, kwa kuwa hali ilivyo sasa ni mbaya.
Profesa Lipumba ambaye pia ni profesa wa uchumi alisema hivi karibuni Dar es Salaam kuwa hali ya uchumi imezidi kudorora na kusababisha maisha ya wananchi wengi kuwa magumu.
“Vijana wa siku hizi wengi hawana simile kushughulika na mambo yanapokwenda sivyo, ajabu ni kwamba wanaofanya mambo hayo yawe magumu wamekuwa wepesi wa kutetea kwa hoja zisizo na msingi kwa masilahi yao binafsi,” alisema.
Akizungumzia maazimio yaliyofikiwa kwenye Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kilichofanyika Desemba 21-22 mwaka huu Dar es Salaam, alisema hatua ya kupandishwa kwa gharama za umeme iliyotangazwa hivi karibuni na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni miongoni mwa mambo ambayo yanaendelea kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi, jambo ambalo lingeweza kuzuilika kwa shirika hilo kudhibiti wizi wa nishati hiyo.
Kuhusu hali ya kisiasa nchini, Profesa Lipumba alisema Baraza Kuu limetoa wito kwa vyombo vya Dola kuwa na weledi na uadilifu na kuacha kutekeleza amri za wanasiasa zisizojali utawala wa sheria na haki za binadamu ili vipunguze uhasama baina yao na raia.
“Serikali pia isitumie Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kushughulikia masuala ya uvunjifu wa sheria katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, badala yake kazi hiyo ifanywe na Jeshi la Polisi kwa mujibu wa taratibu za kisheria. Nao pia waongezewe uwezo wa kiutendaji,” alisema.
Alisema CUF inaona si vyema kutumia JWTZ kudhibiti vurugu kwa kuwa wanajeshi hao hawana mafunzo ya kukamata wananchi wenye tuhuma za uhalifu isipokuwa wamefundishwa jinsi ya kulinda usalama wa nchi katika mipaka.
CHANZO: MWANANCHI

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAJAMBAZI-8 
“PRESS RELEASE” TAREHE 27.12. 2013.
WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU  KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 26.12.2013 MAJIRA YA SAA 20:10HRS HUKO ENEO LA KATUMBA, KATA YA KATUMBA, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA, BARABARA YA MBEYA/TUKUYU. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE  LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AMANI S/O ABILIA, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KATUMBA NA  KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI HASA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KWENYE MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE. 
[B.N.MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WATOTO 15 WATINGA FAINALI ZA SHINDANO LA “MO KIDS GOT TALENT 2013″, FAINALI KUFANYIKA LEO JIONI LEDGER PLAZA – BAHARI BEACH

DSC_1821 
Lango kuu la kuingilia kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar panapofanyika shindano kali la kusaka kipaji cha SUPA STAA wa watoto na vijana! la “MO Kids Got Talent 2013″
.Wazazi wahamasishwa kujitokeza kwa wingi, kuona vipaji vya watoto wao.
.Fainali kuanza saa kumi na moja jioni
DSC_1678
Chief Judge wa Shindano la vipaji vya watoto na vijana wadogo la “MO Kids Got Talent”, Salma Mziray, akitoa maoni yake kwa baadhi ya washiriki walioingia semi finals za shindano hilo linalofanyika kwenye hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji Neema Theobald na kushoto ni msanii wa filamu nchini Hidaya Njaidi wakiwa meza kuu.
DSC_1666 
Sehemu ya zawadi zilizotolewa kwa watoto walioshiriki kwenye usaili wa shindalo la “MO Kids Got Talent 2013″ ambapo fainali zake zinafanyika leo kuanzia saa Kumi na moja jioni ndani ya Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar.
DSC_1706 
Pichani juu na chini ni baadhi ya kati ya watoto 15 wakionyesha vipaji vyao kwenye semi finals za shindano la kusaka vipaji kwa watoto na vijana la “MO Kids Got Talent” lililoandaliwa na Kampuni ya Frost Africa na kudhaminiwa na kampuni ya MeTL Group, ambapo leo jioni kutafanyika fainali za mashindano hayo kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar na mshindi kujinyakulia fedha taslim shilingi Milioni 5 za Kitanzania.
DSC_1875
Mambo ya Sugua Gaga hayo…… Wapi Shaa….??? Kipaji hicho…!!!
DSC_1928
DSC_1760
Sehemu ya watoto wakionyesha vipaji vyao vya aina mbalimbali ikiwemo kucheza, kuimba na vingine kibao.
DSC_1781
DSC_1801
DSC_1822
DSC_1686
Kipaji cha mchezo wa Karate pia kilikuwepo.
DSC_1745
DSC_1789
Sehemu ya watoto wakisubiria kuingia kwenye chumba maalum kuonyesha vipaji vyao.
DSC_1702
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko akigawa zawadi zilizotolewa na MeTL Group pamoja na kupata picha ya kumbukumbu kwa washiriki waliojitokeza kwenye usaili wa shindano la “MO Kids Got Talent” ambapo fainali za shindano hilo zitafanyika leo kuanzia saa kumi na moja jioni kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar.
DSC_1715
DSC_1773
DSC_1812
DSC_1824
DSC_1836
DSC_1857
DSC_1915

DSC_1785

DSC_1749
DSC_1860 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa ambao ndio waandaji wa shindano la “MO Kids Got Talent” Bw. Peter Sekasiko, katika picha ya pamoja na Operations Manager wa MOblog, Zainul Mzige na Mwandishi wa Gazeti la Nipashe, Enles Mbegalo.

EPL HABARI NYINGINE, LIVERPOO WANNE KATIKA MSIMAMO BAADA YA KULIZWA 2-1 ETIHAD, ARSENAL WAREJEA KILELENI..CITY WAPILI…HAHAHAH!


Alvaro Negredo ameifungia Manchester City bao la ushindi usiku huu  dhidi ya Liverpool na kuendeleza ubabe wao katika dimba la Etihad.
Liverpool ambao wamekuwa wapinzani wa Man City nafasi za juu katika msimamo wa ligi kuu nchini England msimu huu walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 24 kupitia kwa  Philippe Coutinho akipokea pasi nzuri kutoka kwa Raheem Sterling.
Lakini wenyeji walijibu mapigo katika dakika ya 31 baada ya beki wa kati na nahodha wa Man City, Vincent Kompany kuunganisha mpira wa kona uliochongwa Mhispania David Sliva.
Sherehe ya ushindi kwa City ilikuja dakika ya 45 baada ya mshambuliaji hatari Alvaro Negredo kufunga bao la pili kufuatia kazi nzuri ya Jesus Navas.
Huwezi amini mpaka saa 12 kasorobo jioni ya leo, Liverpool walikuwa kileleni mwa EPL, hivi sasa ni saa nne usiku wameporomoka mpaka nafasi ya nne katika msimamo na Arsenal wakirudi kileleni kama kawaida.
Kali zaidi wiki ijayo, Liverpool wataingia kwenye kibarua kizito dhidi ya vijana wa Jose Mourinho, klabu ya Chelsea ya London.
Baada ya mechi za leo, timu tano za juu ni kama ifuatavyo;
Pos Team P W D L GF GA GD Pts
1 Arsenal 18 12 3 3 36 18 18 39
2 Manchester City 18 12 2 4 53 21 32 38
3 Chelsea 18 11 4 3 33 18 15 37
4 Liverpool 18 11 3 4 43 21 22 36
5 Everton 18 9 7 2 29 17 12 3
City slicker: Alvaro Negredo (right) celebrates after scoring the decisive goal for Manchester City 
Raha duniani: Alvaro Negredo (kulia) akishangilia bao lake la ushindi kwa klabu yake ya Manchester City
Kikosi cha Man City usiku huu: Hart 7, Zabaleta 6, Kompany 7, Lescott 7, Kolarov 5, Y Toure 6, Fernandinho 7, Navas 8, Silva 7 (Garcia, 86), Nasri 6 (Milner 71, 6), Negredo 8 (Dzeko 76).
Kikosi cha Liverpool: Mignolet 6, Johnson 6, Sakho 7, Skrtel 6, Cissokho 5; Lucas 6 (Aspas, 81), Sterling 7, Henderson 7, Allen 6, Coutinho 6 (Moses, 67), Suarez 7.
Strike: Negredo lifts the ball over the oncoming Simon Mignolet, who made a hash of his attempted save 
Shambulizi: Negredo akipiga mpira wakati Simon Mignolet  akijaribu kuokoa
Flapping: Mignolet waves the ball into the net as Negredo (left) begins to celebrate 
Manyoya: Mignolet akijaribu kuokoa mpira uliotinga wavuni, huku Negredo (kushoto) akianza kushangilia
Jumping for joy: Samir Nasri (right) can't contain his delight as Mignolet is on his knees 
Akiruka kwa furaha: Samir Nasri (kulia)  akionesha furaha yake wakati kipa Mignolet akiwa amejipigia magoti kuugulia maumovu ya goli hilo
He knows what he's done: Mignolet is crestfallen after his error, which led to Negredo's goal 
Anajua alichofanya: Mignolet  akijutia makosa yake yaliyosababisha Negredo afunge bao zuri na la ushindi
Down and out: Negredo lies on the turf clutching his leg and eventually is replaced by Edin Dzeko 
Chini na alitoka nje: Negredo akiwa amelala chini akiugulia maumivu ya mguu na alitolewa nje huku nafasi yake ikienda kwa mshambuliaji mwingine Edin Dzeko
Good Kompany: City captain Vincent Kompany (second left) rises to head the home side's equaliser 
Kompany Mzuri: Nahodha wa City , Vincent Kompany (wa pili kushoto) akiruka juu na kupiga kichwa mpira uliozaa bao la kusawazisha 
Roar talent: Kompany (centre) screams with delight after heading City level 
Kipaji cha juu: Kompany (katikati) akishangilia bao lake na wachezaji wenzake
Tussle: Joleon Lescott (left) and Luis Suarez grapple for possession of the ball 
Huendi mzee:  Joleon Lescott (kushoto) na  Luis Suarez wakigombania mpira
Trying to get away: Suarez attempts to break clear of Lescott with Yaya Toure (centre) trailing 
Anajiribu kutafuta njia: Suarez akijaribu kupasua njia pembeni ya  Lescott  huku  Yaya Toure (katikati) akiunga `traila`
Doubling up: Jesus Navas (left) and Pablo Zabaleta (right) combine to stop Aly Cissokho 
Wawili jamani!: Jesus Navas (kushoto) na Pablo Zabaleta (kulia) wakiungana kumzuia Aly Cissokho

WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TAMASHA LA KRISMAS WASUUZA MIOYO YA MASHABIKI UWANJA WA JAMHURI MOROGORO

Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba katika tamasha la Krismas lililofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki huo hapa nchini na mwimbaji wa kimataifa kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti wamesuuza mioyo ya mashabiki baada ya kushusha burudani ya nguvu katika tamasha hilo, Katika tamasha hilo, mashabiki wamejitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Jamhuri, Tamasha hilo linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam na linatarajiwa kuendelea mkoani Tanga  Desemba 28 mwaka huu.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MOROGORO)  2 
Mwimbaji Edson Mwasabwite akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo jioni. 3 
Boniface Mwaiteje naye akawanyanyua kwenye viti mashabiki waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo. 
Hapa akiimba kwa furaha kumtukuza mungu wake mbele ya mashabiki wake kwenye uwanja wa Jamhuri. 
 7 
Vijana wa  kazi kutoka kundi la Kitimtim la Rose Muhando wakionyesha umahiri wao katika kucheza. 
 8 
Mwimbaji Edson Mwasabwite akiimba na mmoja wa mashabiki wake katika tamasha hilo. 9 
Mwimbaji wa kmataifa wa Zambia Ephraim Sekereti akiimba jukwaani katika tamasha hilo. 10 
Hapa akiimba na mashabiki wake 11 
Upendo Nkone akicheza na mastaeji shoo wake.