TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, March 18, 2015
Rais Kikwete afungua Kituo Cha Taifa Cha Kumbukumbu Dodoma
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Taifa Kumbukumbu
huko kisasa mjini Dodoma leo.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue, watatu kushoto ni Mwenyekiti wa BungeMh. Zungu na
kulia ni Waziri wan chi Ofisi ya Rais Utawala BoraMh.George Mkuchika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kufungua rasmi Kituo cha Taifa
Cha Kumbukumbu kilichopo Kisasa mjini Dodoma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiangalia jalada la mwaka 1940 ambapo alisoma utendaji kazi wa Babu
yake Chifu wa Kabila la Wakwere Mrisho Kikwete wakati huo.Jalada hilo
ni moja ya majalada ya zamani yaliyohifadhiwa kutumia teknolojia ya
kisasa katika Kituo Cha Taifa Cha Kumbukumbu kilichopo Kisasa mjini
Dodoma.Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa kituo hicho Rais Kikwete
ametoa agizo la kuanzishwa maktaba za Viongozi wa kitaifa hususan
marais wastaafu ili kuhifadhi vyema historia ya nchi.
(picha na Freddy Maro)
ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI
Hakuna sababu itayoifanya Zanzibar
kushindwa kuitumia lugha ya Kiswahili katika kufundishia wanafunzi
Skuli kwani Zanzibar inahazina kubwa ya watalamu na ndio chimbuko la
Kiswahili katika Nchi za Afrika na Dunian kwa ujmlai.
Hayo yamesemwa leo huko Eacrotanal
Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Mohamed
Seif Khatib wakati wa ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya siku ya
Kiswahili Duniani yalio fanyika hapo.
Amesema
inawezekana kabisa na
frusa hiyo ifanyiwekazi kwa kukaa pamoja Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar pamoja na Wizara ya Habari UtAMADUNI Utalii na Michezo
Zanzibar kuzipitia sera zilizo tangulia kulipatia mamuzi suala hilo.
Amesema kunanchi nyingi tu duniani ambazo zinasomeshwa kwakutumia lugha
zao na haijawa tatizo katika nchihizo.
“Kuna nchi kama China,Uholazi na nyengnezo wanatumia furusa ya kusomeshea wanafunzi kupitia lugha zao,”
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar Khadija Bakar na Naibu Katibu Mkuu Wiara ya
Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo Zanzibar Issa Mlingoti alisema
watakaa pamoja na wizara zao kulijadili suala hilo kwani hadi sasa kuna
sera mbilizo pingana.
Wamesema wizara ya Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo wao wamelikubali hilo kuwa wanafunzi
wafundishwe kupitia lugha ya Kiswahili la kini Wizara ya Elimu wao
wanalipinga,hivyo watakaa pamoja na kusawazisha ili waendesambamba na
wezao wa Tanzania Bara.
Nae Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Taifa (SUZA) pia mjumbe wa baraza la kiswahili Zanzibar Mmanga M.
Mjawiri amesema kuna umuhimu mkubwa wanafunzi Skuli wafundishwe kupitia
lugha yao ya kishwahili kwani kiengereza Tanzania bado kikwazo. Hakuna masiliano mazuri kati ya
walimu na wanafunzi wakati wa kufundisha hivyo Kiswahili ndio suluhisho
la wanafunzi kumuelewa mwalimu.
CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA KUTILIANA SAINI YA MKATABA WA MAKUBALIANO YA MAFUNZO YA WATALAAM WA TAKWIMU NA CHUO CHA TAKWIMU CHA INDIA.
Na: Veronica Kazimoto, Dar es
Salaam,
17
Machi, 2015.
Chuo cha Takwimu
Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimekamilisha maadalizi ya kutiliana saini ya
mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo cha Takwimu
cha nchini India.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha EASTC Prof. Innocent
Ngalinda amesema mkataba huo utasainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
“Maandalizi ya
kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo
cha Takwimu cha nchini India yamekamilika kwa kiasi kikubwa na ndio maana hapa
mbele yenu mnamuona Naibu Balozi wa Ubalozi wa India hapa nchini amefika kwa
ajili ya kujirizisha”, amesema Prof. Ngalinda.
Prof. Ngalinda amesema
kuwa mkataba huo una manufaa makubwa kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa wataalam
wengi katika tasnia ya takwimu hapa nchini.
Pamoja na ongezeko la
watalaam wa takwimu hasa wakufunzi, kutakuwa na ukarabati wa miundombinu katika
chuo hicho ambapo mabweni ya wanafunzi pamoja na ofisi za chuo hicho zitakarabatiwa.
Prof. Innocent Ngalinda
amefafanua kuwa katika mkataba huo, kutakuwa na mpango wa kubadilishana wanafunzi
katika vyuo hivyo viwili ili kupanua uelewa wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na
kuongeza ujuzi zaidi katika masuala ya kitakwimu.
Kwa upande wake Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal amefurahishwa na maandalizi
yaliyofanyika na kusema kuwa nchi yake iko tayari kutiliana saini ya mkataba wa
makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa Takwimu kutoka chuo cha Takwimu Mashariki
mwa Afrika na chuo cha Takwimu cha nchini India.
“Nimefurahishwa na
maandalizi yaliyofanyika katika chuo hiki na sasa tunamsubiri Waziri wa mambo
ya Nje wa nchini India kwa ajili ya kutiliana saini ya mkataba huu ifikapo tarehe
28 Machi, 2015,” amesema Naibu Balozi Humpal.
Chuo cha Takwimu
Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam na chuo cha
Takwimu cha India vimekuwa vikishirikiana tangu mwaka 2012 lakini ushirikiano
huo haukuwa rasmi hivyo vyuo hivyo vimeamua kusaini mkataba wa makubaliano kwa
ajili kufanya ushirikiano huo kuwa rasmi.
==================================================================
Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akiangalia vitabu mbalimbali vilivyopo
katika maktaba ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati wa kuangalia maadalizi
ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India
utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akisoma moja ya vitabu kilivyopo katika
maktaba ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati wa kuangalia maadalizi
ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India
utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
Mkuu wa Chuo cha
Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akimwelezea Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal kuhusu chumba cha kompyuta kilichopo
chuoni hapo wakati wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano
ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo
cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. (PICHA ZOTE NA
VERONICA KAZIMOTO)
Subscribe to:
Posts (Atom)






