Na: Veronica Kazimoto, Dar es
Salaam,
17
Machi, 2015.
Chuo cha Takwimu
Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimekamilisha maadalizi ya kutiliana saini ya
mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo cha Takwimu
cha nchini India.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha EASTC Prof. Innocent
Ngalinda amesema mkataba huo utasainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
“Maandalizi ya
kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo
cha Takwimu cha nchini India yamekamilika kwa kiasi kikubwa na ndio maana hapa
mbele yenu mnamuona Naibu Balozi wa Ubalozi wa India hapa nchini amefika kwa
ajili ya kujirizisha”, amesema Prof. Ngalinda.
Prof. Ngalinda amesema
kuwa mkataba huo una manufaa makubwa kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa wataalam
wengi katika tasnia ya takwimu hapa nchini.
Pamoja na ongezeko la
watalaam wa takwimu hasa wakufunzi, kutakuwa na ukarabati wa miundombinu katika
chuo hicho ambapo mabweni ya wanafunzi pamoja na ofisi za chuo hicho zitakarabatiwa.
Prof. Innocent Ngalinda
amefafanua kuwa katika mkataba huo, kutakuwa na mpango wa kubadilishana wanafunzi
katika vyuo hivyo viwili ili kupanua uelewa wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na
kuongeza ujuzi zaidi katika masuala ya kitakwimu.
Kwa upande wake Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal amefurahishwa na maandalizi
yaliyofanyika na kusema kuwa nchi yake iko tayari kutiliana saini ya mkataba wa
makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa Takwimu kutoka chuo cha Takwimu Mashariki
mwa Afrika na chuo cha Takwimu cha nchini India.
“Nimefurahishwa na
maandalizi yaliyofanyika katika chuo hiki na sasa tunamsubiri Waziri wa mambo
ya Nje wa nchini India kwa ajili ya kutiliana saini ya mkataba huu ifikapo tarehe
28 Machi, 2015,” amesema Naibu Balozi Humpal.
Chuo cha Takwimu
Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam na chuo cha
Takwimu cha India vimekuwa vikishirikiana tangu mwaka 2012 lakini ushirikiano
huo haukuwa rasmi hivyo vyuo hivyo vimeamua kusaini mkataba wa makubaliano kwa
ajili kufanya ushirikiano huo kuwa rasmi.
==================================================================
Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akiangalia vitabu mbalimbali vilivyopo
katika maktaba ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati wa kuangalia maadalizi
ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India
utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akisoma moja ya vitabu kilivyopo katika
maktaba ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati wa kuangalia maadalizi
ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India
utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
Mkuu wa Chuo cha
Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akimwelezea Naibu
Balozi wa India nchini Balvinder Humpal kuhusu chumba cha kompyuta kilichopo
chuoni hapo wakati wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano
ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo
cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. (PICHA ZOTE NA
VERONICA KAZIMOTO)
No comments:
Post a Comment