TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, March 18, 2015
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
KIJANA MMOJA MKAZI WA ITIMBO WILAYANI RUNGWE ALIYEFAHAMIKA
KWA
JINA LA HODAR JOHN (22) ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI NA MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA GILBERT MWASIMA NA KUFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MISHENI ITETE KWA MATIBABU.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 17.03.2015 HUKO
KATIKA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI KILICHOPO KATIKA KITONGOJI CHA ITIMBO, KIJIJI CHA ISALE, KATA YA LUTEBA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA ULEVI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA KUWEZESHA KUMPATA MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
TAARIFA YA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA KISEPE ALPHONCE (28) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA KASUMULU-KYELA PAMOJA NA NSAJIGWA MWAKALONGE (39) DEREVA NA MKAZI WA KYELA WAKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] KUTOKA NCHINI MALAWI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA DOUBLE PUNCH KATONI 70, BOSS KATONI 18, CHARGER KATONI 14 NA RIDDER KATONI 08.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.03.2015 MAJIRA YA SAA 03:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA WALIKAMATWA WAKIWA WANASAFIRISHA BIDHAA HIZO KWENYE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.479 CJM TOYOTA IPSUM LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA NSAJIGWA MWAKALONGE WAKITOKEA KASUMULU KUELEKEA MBEYA MJINI.
KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA MKAZI WA SIMBALIVE WILAYANI CHUNYA AITWAYE ELIZA KISUNGA (33) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA SIMBALIVE AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA NNE NA NUSU PAMOJA NA POMBE KALI [VIROBA] AINA YA RIDDER PAKETI 03 NA VIPODOZI AINA YA EPIDEMIC PAKETI 02.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 17.03.2015 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA SIMBALIVE, KIJIJI CHA ITUMBA, KATA YA CHALANGWA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA BIDHAA HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA UINGIZAJI, USAMBAZAJI NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment