WAKAZI wa vijiji viwili vya Nyagasense na Rung’abure vilivyoko
kwenye wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wamehakikishiwa kuanza kupata
maji ifikapo mwishoni mwa wiki hii kufuatia wakandarasi wanaojenga
miradi ya maji ya vijiji hivyo kuahidi kufikisha maji katika kipindi
hicho.
Akitoa ahadi kwa Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakati
wa mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Nyagasense, Mhandisi wa mradi
wa maji wa kijiji hicho John Mapande amesema maji yataanza kutoka siku
tatu kuanzia leo.
Mhandisi Mapande alitoa ahadi hiyo wakati Waziri Prof. Maghembe
akizungumzia matumaini ya kukamilika kwa mradi huo wa maji ambapo
aliwaomba wananchi wa kijiji hicho kukaa mkao wa kunywa maji.
“Ninawomba sana mkae mkao wa kunywa maji kwa sababu nimeona kwa
macho yangu na nimeridhika, vinginevyo nisingeweka jiwe la msingi, hivyo
katika kipindi kifupi maji yatafika huku mitaani” alisema Waziri Prof.
Maghembe Baada ya kutoa matumaini hayo, Waziri Prof. Maghembe alimuita
mkandarasi wa mradi huo na kumsihi kukamilisha mradi huo na kwamba fedha
zake zilizobaki atalipwa, na mazungumzo yao yailikuwa hivi:
Waziri: Mkandarasi uko wapi?
Mkandarasi: Niko hapa mheshimiwa Waziri.
Waziri: Sasa wewe ukamilishe mradi wangu, ile miezi sita ikiisha
fedha zako zitakazokuwa zimebaki tutakulipa, kwa hiyo we maliza mradi
haraka wiki ijayo mimi ninywe maji hapa kabla sijakwenda Dar es Salaam.
Mkandarasi: Nitajitahidi Mhe Waziri kukamilisha.
Waziri: Jitahidi, maana kazi iliyobaki ni kidogo sana kukamilisha huu mradi Mkandarasi: Ni kazi ya siku mbili au siku tatu maji yatakuwa yameshatoka Waziri: Eeh sasa kazi ya siku mbili tatu mimi nitakuwa Mara hapa, nataka nikienda Mugumu nisimame hapa ninywe maji.
Kwa upande wa mradi wa Maji wa kijiji cha Rung’abure, Waziri
Prof. Maghembe alimuagiza mkandar akafunge jenereta na kupeleka pampu na
kuifunga ili maji yaanze kusukumwa kuanzia leo.
Waziri Prof. Maghembe alichukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya
wananchi kuzuia malori yanayopeleka jenereta na pampu kwenye eneo la
mradi, kupita kwenye eneo lao, lakini Serikali ya kijiji ilimuhakikishia
Waziri kwamba wananchi hao wameruhusu gari ipite.
Waziri: bwana mkadarasi yuko wapi Mkandarasi: Nipo hapa mheshimiwa
Waziri: Nimemuagiza huyu mkandarasi kesho alete jenereta ifungwe
kwenye nyumba ya genereta na alete pampu pale ifungwe ili maji yaanze
kusukumwa kesho (leo).
Kwa hiyo muangalie atafunga kesho labda jioni atakuwa
amekamilisha, lakini hata kama hakukamilisha Alhamisi atakamilisha,
Alihamisi akikamilishwa bado nitakuwa mkao wa Mara.
Kwa hiyo siku ya Alhamisi kwa uhakikka wataanza kusukuma maji,
nimeona kazi nyingi hazijakamilika, lakini hiyo ikamilishwe kesho na
Alhamisi ili sasa wakati wanaendelea na kazi nyingine mnaendelea kunywa
maji.
Baada ya kuzungumza hayo, wananchi walipiga vigelegele na makofi kuonesha kufurahishwa na hatua hiyo.
Wakizungumza kufurahishwa na matumaini hayo ya kupata maji,
baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nyagasense wamesema wamefurahi kupata
ujio wa Waziri na hatimaye kuahidiwa kupata maji.
“Kwa kweli tumefurahi sana kupata ujio wa Waziri wa Maji na
tumeridhika na ahadi ya kupata maji wiki hii kwa sababu tumekosa maji
kwa miaka miwili sasa tulikuwa tunapata shida ya kuyapata” alisema mkazi
wa kijiji hicho Christina Machota.
Mradi wa Maji wa kijiji cha Nyagasense unaotekelezwa chini ya
Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira, unatumia chanzo cha kisima
kirefu chenye uwezo wa kutoa maji lita 6000 kwa saa na utakapo kamilika
utahudmia watu 5,530 na mifugo 2620.
Mradi huo una jumla ya kilometa 19.54 za mtandao wa mabomba ya
maji na vituo 20 vya kuchote maji na birika 2 za kunyweshea mifugo.
Akiwasilisha taarifa ya mradi wa maji wa Rung’abure, Mhandisi wa
Maji Wilaya ya Serengeti Marwa Mulaza, alisema una chanzo cha maji
mtiririko na hutoa lita 10,000 kwa saa na ulianza kutekelezwa Oktoba
mwaka2013.
Alisema mradi huo utakapokamilika utahudumia watu 3, 457 na mifugo na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Aprili mwaka huu 2015.
No comments:
Post a Comment