TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, March 18, 2015
PINDA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO JAPAN
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanayojirudiarudia nchini yanachafua heshima na jina la Tanzania kwa kuwa yanakwenda kinyume na haki za binadamu.
Akizungumza na watanzania waishio nchini Japan kwenye ubalozi wa Tanzania jijini Tokyo Machi 17, 2015, Mheshimiwa Pinda amesema kusekana kwa hofu ya Mungu na elimu kwa badhi ya watu nchini ndiyo chanzo kikubwa cha mauaji hayo.
Amesema Binadamu yeyote anayemwamini Mungu na kushika maagizo yake hawezi kudanganyika wala kusahawishika kuwa kiungo cha mtu mwenye ulemavu wa ngozi kinaweza kuwa chanzo kikubwa cha mafanikio ya kifedha.
Mheshimiwa Pinda ambaye alikuwa akijibu risala ya watanzania hao waishio Japan alisisitiza kuwa serkali haijalifumbia macho tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ndiyo maana watu kadhaa wamekakatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sharia
Amesema kunguliwa kwa vituo maalum vya kuwatunza watoto wenye ulemavu wa ngozi ili kuwalinda ni moja ya hatua ambazo serikali imechukuwa lli kukomesha mauaji hayo.
Waziri Mkuu, amewataka watanzania na hasa wa watoto wenye ulemavu wa ngozi kuacha tamaa ya fedha, mali na utajiri wa harakaharaka ambao mwisho wake ni majuto na laana.
Amesema ushirikiano wa dhati kati ya serikali na wananchi wote ndiyo utakaokomesha kabisa tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kuwa wanaotenda uovu huo ni watanzania wenzetu, tunaishi nao, tunakula nao na kwa vyovyote vile wanafahamika.
“Mauaji haya yanafanyika usiku yanafanyika usiku na wakati mwingine ndugu wa karibu au mzazi ametajwa kuwa ameshirikiana kwa siri na wauaji kwani mara kadhaa yanapofanyika baba mwenye motto anakuwa hayupo nyumbani” alifafanua Waziri Mkuu.
Katika risala iliyosomwa na Mwenyekiti wao, Bw. David Semiono watanzania hao waliitaka serikali kuhakikisha kwamba mauaji ya wtu wenye ulemavu wa ngozi yanakomeshwa kwa vile yamekuwa chanzo cha kejeli, fedhaha na aibu kwao.
Wamesema wanalazimika kujibu maswali mengi na magumu wanayoulizwa mara nyingi na wenyeji wao Wajapan na wageni wengine kutoka nchi mbalimbali ambao waziwazi wameeleza kukerwa kwao na mauaji hayo na wengine wanasita kutembelea Tanzania kwa hofu kuwa huenda wauaji hao wakawafananisha na watu wenye ulemavu wa ngozi jambo ambalo linaweza kuwafanya wapoteze maisha.
Ziara ya Waziri Mkuu MIZENGO PINDA inaendelea hapa TOKYO JAPAN ambapo Waziri Mkuu pamoja na kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa serikali ya JAPAN, wafanyabishara, washirika wa maendeleo na watendaji wa makampuni mbalimbali na kuwaeleza fursa za uwekezaji nchini, na kuwaeleza hali ya uchumi wa Taifa pamoja na shughuli za maendeleo zinafanywa na serikali na kutamka wazi kuwa kwa tafiti zilizofanywa zinaonyesha kuwa Tanzania kwa sasa imeondolewa kwenye kundi la nchi maskini kutoka na uchumi wake kuendelea.
Mheshimiwa Pinda amewaasa watanzania wote waishio nje ya nchi kukumbaka kuwekeza nyumbani ili watakapoamua kurudi nyumbani kwa hiyari au kwa lazima wasije wakaumbuka kwa kukosa hata mahali pa kuishi au chanzo cha mapato kitakachowawezesha kupata mahitaji yao muhimu.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment