KAMATI
YA Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) ilikutana Dar es Salaam jana na kujadili masuala
mbalimbali.
A; MAFUNZO
Kikao kilikubaliana watafutwe
wataalamu wa kuendesha mafunzo kwa kada mbalimbali za waandishi wa
habari za michezo nchini ili kuongeza ufanisi katika namna ya kuripoti
habari za michezo michezo mbalimbali.
Kundi la kwanza litakuwa la
waandishi chipukizi ambao wapo chini ya miaka mitano katika taaluma,
ambapo mafunzo yao yatafanyika Machi 25 mwaka huu Dar es Salaam
yakishirikisha waandishi wa habari chipukizi 30 na wa kada ya kati 10.
Tayari TASWA imepata mdhamini wa
mafunzo hayo na kinachofanyika hivi sasa ni uteuzi wa washiriki, ambapo
wahariri wa habari za michezo watahusishwa kupendekeza washiriki kutoka
katika vyombo vyao.
Wakufunzi wa semina hiyo
watakuwa waandishi wa habari wakongwe, walimu wa uandishi wa habari na
wataalamu wa michezo mbalimbali nchini. Jumatano Machi 18 TASWA
itatangaza mdhamini wa mafunzo ya Dar es Salaam pamoja na majina ya
washiriki.
Awamu ya pili pia itafanyika
Dar es Salaamwaandamizi ikihusisha waandishi wa habari za michezo wa
kada ya kati 30 na waandishi wa habari waandamizi 10 na itafanyika
mwanzoni mwa Mei mwaka huu.
Awamu ya tatu itahusisha
waandishi wa habari za michezo waandamizi na wahariri wa habari za
michezo na jumla yao itakuwa 40 na itafanyika mkoani Mtwara Mei 29, 30
na 31 mwaka huu. TASWA ipo hatua za mwisho za mazungumzo na wadhamini wa
mafunzo hayo ya Mtwara.
B; MKUTANO MKUU
Mkutano Mkuu wa TASWA umepangwa
kufanyika Julai 25 na 26 mwaka huu mkoani Morogoro, ambapo pamoja na
mambo mengine utajadili Rasimu ya Katiba mpya ya chama hicho.
Kamati ya Utendaji ya TASWA
imeteua kamati maalum ya kushughulikia katiba hiyo, ambapo hivi sasa
Katibu Mkuu anawasiliana na wajumbe walioteuliwa katika kamati hiyo na
baada ya wote kupewa barua na kukubali uteuzi atatangaza majina hayo.
C: Kamati ya Faraja
Kikao kilikubaliana kuwa iundwe
Kamati ya Faraja kwa ajili ya kuwafariji wanachama wake kutokana na
matukio mbalimbali yanayowakuta ikiwemo ugonjwa.
Uamuzi huo umechukuliwa kwa nia
ya kuhakikisha waandishi wa habari za michezo wanakuwa wamoja kwa shida
na raha kwa vile wamekuwa kama ndugu.
Kwa kuanzia TASWA inawaomba
wadau wote kushirikiana na kamati hiyo ambayo jukumu lake la kwanza
itakuwa kumsaidia mwandishi mkongwe nchini, Masoud Sanani, ambaye
waandishi wengi kwa namna mbalimbali wamepita mikononi mwake.
Sanan hivi sasa ni mgonjwa kwa
zaidi ya mwaka mmoja na yupo kwao Zanzibar, ambapo juzi niliwasiliana
naye na amesema afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku.
Kutokana na hali hiyo TASWA kwa
kushirikiana na kamati hiyo imepanga kwenda kumjulia hali Jumapili Machi
22 mwaka huu.Tunaomba wadau waipe ushirikiano kamati yetu.
Walioteuliwa katika kamati hiyo
na nafasi zao kwenye mabano ni Angela Msangi (Mwenyekiti), Majuto Omary
(Katibu), Zena Chande (Mhazini), Asha Kigundula, Isakwisa Mwaifuge na
Elias Kambili (Wajumbe).
D;MEDIA DAY
Maandalizi kuhusiana na bonanza
kwa wanahabari yanaendelea na matumaini ni kuwa litafanyika Aprili 25
mwaka huu jijini Dar es Salaam kama ilivyopangwa.
E;MSIBA WA KOCHA MARSH
TASWA imepokea kwa masikitiko
taarifa ya kifo cha aliyepata kuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa
‘Taifa Stars’, Sylivestre Marsh, hivyo inatoa pole kwa familia na
wanamichezo wote hapa nchini katika kuomboleza kifo cha kocha huyo.
Marsh atakumbukwa na waandishi
wa habari za michezo kutokana na ukaribu wake na alikuwa na ushirikiano
wa kutosha pale alipoombwa kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment