TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, April 27, 2016
NEWS ALERT: Harry Kitilya na wenzake wafutiwa shtaka moja, dhamana yagonga mwamba
Aidha
mpaka mtandao huu unatoka Mahakamani hapo Mawakili walikuwa bado
wakihangaikia kupata dhamana kufutiwa shitaka hilo lililokuwa na kikwazo
kikubwa cha dhamana
Baada ya kufutiwa shitaka hilo, DPP aliwasilisha hati ya mapendekezo ya kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufuta shitaka namba nane la utakatishaji Fedha linalowakabili watuhumiwa hao, ambapo zoezi la dhamana liligonga mwamba na Washitakiwa hao wamerudishwa rumande.

Sherehe za miaka 5 ya kitchen party gala zafana!
afya,ujasiriamali
n.k.
Mwanamke
amezungukwa na mambo mengi sana ambayo kila wakati anahitaji
kukumbushwa na kufundishwa ikibidi ndio tukaanza KITCHEN PARTY GALA 2011
mpaka Leo 2016 " Alisema Dina Marios moja ya waandaaji wa tukio hilo
akishirikiana na Vida Mndolwa. "Tumelidesign Tamasha letu liwe la
kuelimisha na kuburudisha pia ili kukufanya urelax na ufurahi na kila
utakachosikia usikisahau." Aliongeza Dina Marios.
Mratibu wa Sherehe za miaka 5 ya kitchen party gala Dina Marios akitoa mwongozo mfupi wa shughuli nzima ukumbini.
mkuu wa wilaya ya kinondoni akagua miradi mbalimbali ya maendeleo manispaa ya Kinondoni
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh . Ally Salum Hapi akielekezwa jambo alipokuwa akikagua moja ya mradi ndani ya wilaya hiyo.
Mh.
Hapi akikagua na kupokea taarifa ya miradi mbalimbali iliyokamilika na
inayoendelea kukamilika.
Mh. Hapi akipata maeelezo mara baada ya kagua na kupokea taarifa ya miradi mbalimbali iliyokamilika na inayoendelea kukamilika.
RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU TAWALA WAPYA WA MIKOA 10 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha
Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na
kuwapangia vituo vyao vya kazi.
Makatibu Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Makatibu Tawala walioapishwa ni;
1. Arusha - Richard Kwitega
2. Geita - Selestine Muhochi Gesimba
3. Kagera - Armatus C. Msole
4. Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
5. Pwani - Zuberi Mhina Samataba
6. Shinyanga - Albert Gabriel Msovela
7. Singida - Dr. Angelina Mageni Lutambi
8. Simiyu - Jumanne Abdallah Sagini
9. Tabora - Dkt. Thea Medard Ntara
10. Tanga - Eng. Zena Said
Makatibu Tawala wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa vituo vya kazi na wale waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwep,o ambao tayari walishakula kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016

Benki ya Exim yazindua mashine yake ya kwanza ya kuweka pesa kwenye akaunti.
BENKI ya Exim Tanzania imezindua mashine yake ya kwanza ya kuweka pesa (CDM) itakayowawezesha wateja wa kampuni ya Pacific International Lines, PIL kuweka pesa kwenye akaunti zao moja kwa moja bila kulazimika kufika kwenye ofisi au kuhudumiwa na wafanyakazi wa benki hiyo.
Ufunguzi wa mashine hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni ukihusisha mwakilishi wa benki hiyo ambaye ni Mkuu wa Huduma za matawi Bw Eugine Massawe pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni ya PIL Bw. Kevin Stone.
“Mteja atapokea ujumbe mfupi wa maneno kuhusiana na mwenendo ya muhamala alioufanya,’’ alisema Bw Massawe huku akisisitiza: “Benki ya Exim itabaki kuwa benki pekee yenye kubuni huduma zinazokidhi matakwa ya wateja kulingana na mabadiliko ya kimahitaji katika huduma za kibenki,’’
Alisema huduma hiyo imewekwa jirani na makao makuu ya benki hiyo ili kuwawezesha watumiaji wa huduma hiyo kupata msaada kwa urahisi kutoka kwa wafanyakazi wa benki pale wanapohitaji.“Itakapofikia kipindi ambacho wateja wetu watakuwa tayari wamejenga uelewa wa kutosha kuhusiana na matumizi sahihi ya mashine hii tutakuwa tayari kuongeza mashine nyingine katika maeneo mbalimbali ili waweze kufurahia huduma hii zaidi,’’ aliahidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)