BENKI ya Exim Tanzania imezindua mashine yake ya kwanza ya kuweka pesa (CDM) itakayowawezesha wateja wa kampuni ya Pacific International Lines, PIL kuweka pesa kwenye akaunti zao moja kwa moja bila kulazimika kufika kwenye ofisi au kuhudumiwa na wafanyakazi wa benki hiyo.
Ufunguzi wa mashine hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni ukihusisha mwakilishi wa benki hiyo ambaye ni Mkuu wa Huduma za matawi Bw Eugine Massawe pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni ya PIL Bw. Kevin Stone.
“Mteja atapokea ujumbe mfupi wa maneno kuhusiana na mwenendo ya muhamala alioufanya,’’ alisema Bw Massawe huku akisisitiza: “Benki ya Exim itabaki kuwa benki pekee yenye kubuni huduma zinazokidhi matakwa ya wateja kulingana na mabadiliko ya kimahitaji katika huduma za kibenki,’’
Alisema huduma hiyo imewekwa jirani na makao makuu ya benki hiyo ili kuwawezesha watumiaji wa huduma hiyo kupata msaada kwa urahisi kutoka kwa wafanyakazi wa benki pale wanapohitaji.“Itakapofikia kipindi ambacho wateja wetu watakuwa tayari wamejenga uelewa wa kutosha kuhusiana na matumizi sahihi ya mashine hii tutakuwa tayari kuongeza mashine nyingine katika maeneo mbalimbali ili waweze kufurahia huduma hii zaidi,’’ aliahidi.
No comments:
Post a Comment