TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, April 26, 2016
UVCCM ARUMERU WALAANI KITENDO CHA MWENYEKITI WA MKOA KUMSIMAMISHA KAMANDA WAO
Na Woinde Shizza,Arusha
BARAZA la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya
Arumeru umelaani kitendo cha UVCCM mkoani hapa kumsimamisha kamanda wa
umoja wa Vijana wa UVCCM wilaya ya Arumeru Mathias Manga kutokana na
kuisaliti CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.
Aidda baraza hilo limelaani tamko lililotolewa wiki iliyopita na
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Sabaya na kumtaka ajitathmini
na kujipima kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa,kama ataona
hawezi ajing'oe mwenyewe.
Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya,alisema kuwa
wanamtambua Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa
(NEC),kama Kamanda wao wa vijana.
"Tunalaani tamko lililotolewa na Mkoa na hatumtambui kamanda
mwingine,Kamanda wetu hajatendewa haki,wajumbe wa baraza tumetathmini
tamko la Lengai tunaona ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni,amepoka madaraka
yasiyo yake,kitendo ambacho ni kurudisha chama nyuma badala ya
kukijenga.
Mungaya alisema kuwa "Sabaya ajitathmini,ajipime kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa kwani tunaona akiendelea hivi kukiuka kanuni atakiua chama,ni bora ajing'oe
mwenyewe kama anaona hawezi,tunampa siku saba akanushe madai aliyoyatoa
dhidi ya kamanda wetu".
Alisema kuwa tamko hilo ni batili na hawalitambui na kumtaka Manga
asivunjike moyo aendelee na haratkati za kukijenga chama hivyo asirudishwe
nyuma na changamoto anazokabiliana nazo.Akizungumzia yeye kuwepo kwenye baraza hilo alidai kuwa siku ya kikao alikuwepo ila alikataa kupiga kura ya kumkataa Kamanda wake na kuamua
kutoka nje.
Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment