TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, April 26, 2016
Wakuu wa wilaya Kilolo na Iringa watuliza hasira za wana kijiji cha ILambilore na Ilore
Mgogoro uliokuwa unaashiria kuvunja amani kati ya vijiji viwili Ilore (wilaya ya Kilolo) na Ilambilore (wilaya ya Iringa),ulitulizwa na wakuu wa wilaya ya Kilolo Mh Selemani Mzee na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela ambao walipofika kwenye eneo la tukio na kukutana na wananchi wa vijiji vyote viwili ambao walikuwa na hasira huku kila mmoja akidai mwenzie kaingilia eneo la mwenzake.
Katika mgogoro huo eneo la kijiji cha kitongoji cha Igominyi kwenye gazeti la serikali linaonyesha kipo Kijiji cha Ilore (Kilolo) lakini kwenye ramani ya mpaka wa wilaya kinaonyesha kipo Ilambilore (Iringa). wakuu hao waliahidi ndani ya siku 30 wataleta jibu.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo alipiga marufuku wananchi kujichukulia madaraka na kuanza kufyeka msitu. Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Kasesela aliagiza wafugaji wasivushe kabisa mifugo yao kwenda upande wa wenzao. Pia ni wakati mufaka wafuigaji wakaacha kuwa wachungaji bali wafugaji hii iwe ni pamoja na kubadili aina ya mifugo.
Mfugaji maarufu aitwaye Selemani alilaumiwa kwa mifugo yake kuvuka na kula mazao katika mashamba ya watu. Mkuu wa wilaya ya Iringa alimuamuru Mfugaji huyo kulipa kiasi cha shilingi 90,000/ na debe 2 za mahindi. Pia kufanya tathmini ya shamba la mkulima mwingine ili nalo lilipwe fidia. kikao hicho kiliisha mnamo majira ya saa 10 jioni.
Kikao hicho kikiendelea kati ya wananchi wa kijiji cha
Ilore (wilaya ya Kilolo) na Ilambilore (wilaya ya Iringa),kufuati mgogoro wao wa mipaka kati ya kijiji na kijiji.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akizungumza na baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo katika suala zima kuleta amani miongoni mwao.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akipewa ufafanuzi kutoka kwa mmoja wa wananchi wa vijiji hivyo katika suala zima kuleta amani miongoni mwao.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment