TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, April 27, 2016
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi afungua Mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa Elimu mkoani IRINGA
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dr Ndalichako alifungua mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa elimu Tanzania yaliyo fanyika katika chuo cha walimu Kleruu leo. waliojumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Sumbawanga, Songwe na Mbeya.
Mafunzo hayo yana husu uhakiki wa ubora wa KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu). Akifungua mafunzo hayo Dr Ndalichako alisema serikali imepania kukuza ubora wa elimu inayo tolewa hivyo basi lazima itaboresha kitengo cha uhakiki ubora wa elimu Tanzania.
Mkuu wa wilaya bwana Richard Kasesela akitoa salamu alisema " ni wakati muafaka kubadili KKK iliyopo iliyo zoeleka sasa yaani KULA, KULALA na KUCHEZA kuiirejesha kwenye maana halisi ya KUSOMA, KUANDIKA na KUHESABU.
Mkuu wa mkoa Bi.Amina Masenza akimkaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Ndalichako,Bi Masenza alimuomba waziri wa Elimu kuhakikisha Wahakiki ubora wanapewa kipaumbele katika kukuza elimu Tanzania.
Baadhi ya waliohudhuria mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa elimu Tanzania yaliyofanyika katika chuo cha walimu Kleruu leo. Mafunzo hayo yajumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Sumbawanga, Songwe na Mbeya.
Sehemu ya meza kuu kwenye mkutano huo
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment