WAZIRI
MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, amemuomba
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama,
kupeleka huduma hiyo katika mikoa ya Kusini kwa sababu wanakosa huduma
ya neno la Mungu.
Kampuni
ya Msama huandaa Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba
mwaka huu na Pasaka linalotarajia kufanyika mwakani hapa nchini.
Majaliwa
alisema kwa sasa tamasha hilo limekuwa na nguvu kubwa ya kuhakikisha
inahamasisha jamii katika mambo mbalimbali hivyo ni wakati wa mikoa ya
kusini kufaidika.
Alisema
kuwa serikali yake imejipanga kuhakikisha kuwa kila Mtanzania ana haki
ya kuona serikali yake inawajali na kuwapenda hivyo taasisi kama Msama
Promotions, sasa inahitaji kujitanua na kufika mikoa mingi ya Tanzania.
Waziri
Mkuu alisema kuwa amekuwa akifuatilia namna Tamasha la Pasaka
linavyojitahidi katika kuelimisha na kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia
hasa wajane na yatima hivyo na mikoa kama Lindi na Mtwara nayo
inahitaji huduma hiyo.
“Nimefarijika
sana na namna kampuni ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake,
Alex Msama namna inavyofanyakazi zake katika kutoa burudani na
kuelimisha jamii kwa maana hivyo ningependa kuwaunga mkono katika hilo,”
alisema Majaliwa.
Alisema
mikoa mingi ikiwamo Lindi na Mtwara nayo inachangamoto nyingi hivyo
wanahitaji ujumbe kama unatolewa katika Tamasha la Pasaka kuhakikisha
kila kitu kinakwenda sawa.
“Kutoa
misaada kwa yatima sio kitu kidogo lakini kubwa ni namna kampuni ya
Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, inavyofanyakazi
zake kwa kufuata sheria katika hili nawapongeza lakini kubwa ni
kukumbuka mikoa ya Kusini nayo inahitaji huduma hiyo.
Alisema
kuwa kuna waimbaji wengi wakubwa ambao kwa sasa wamekuwa wakifanya kazi
kwa ushirikiano na Msama lakini bado hawajawahi kufika katika mikoa ya
kusini hivyo ni wakati wake kuhakikisha nao wananufaika na tamasha hilo.
Majaliwa amemtaka Msama kuendelea na huduma hiyo kwani serikali iko tayari kutoa msaada wa hali na mali.
Aidha
Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama amemshukuru Waziri Mkuu
Majaliwa na kusema kuwa atajitahidi kuboresha na kuhakikisha wananchi
wote wa Tanzania wananufaika na huduma hiyo.
Msama
amesema kuwa amesikia kilio cha Waziri Mkuu nakusema kuwa kamati yake
iko makini na inajipanga kuhakikisha ombi hilo linafanyiwa kazi.
No comments:
Post a Comment