Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Ruth Mtoi Simba amesema
kuwa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya wameamua kuchangia huduma
za kijamii ili kuwasaidia watanzania wenye kipato cha chini kupata
huduma bora za afya.Mwanachama wa Umoja huo Fadhili Mganya na Katibu
wake Costantini Mashauri wamesema kuwa umoja huo umelenga kuwasaidia
watanzania kutatua changamoto mbalimbali za afya ,kijamii na kiuchumi
kwa kushiriki katika kutatua changamoto hizo
Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika
Mashariki leo wamesheherekea sikukuu ya Muungano kwa kutembelea
hospitali ya Ngarenaro na kutoa msaada wa vifaa tiba ili kusaidia
kuboresha huduma za afya .
No comments:
Post a Comment