MWAKILISHI
wa jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said, akikabidhi msaada wa
mabati 24 kwa familia ya mzee Ali Nyau (kushoto) na mkewe Bi. Tamasina
Thomas (wa tatu kutoka kushoto), baada ya nyumba yao iliyoko Kibele Kwa
Bohora kuanguka kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha
nchini. (Picha na Martin Kabemba).
Na Salum Vuai, MAELEZO
VIONGOZI
wa majimbo pamoja na watu wengine wenye uwezo, wamehimizwa kuendelea
kuwasaidia wananchi walioathirika na mvua za masika zinazoendelea
kunyesha kote nchini.
Mwakilishi
wa jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said, amesema maafa yaliyowakumba
wananchi mbalimbali, yanahitaji msaada wa kila mwenye uwezo bila
kuangalia tofauti za kisiasa, kidini au maeneo waliko.
Said
alisema hayo huko Kibele Kwa Bohora, jimbo la Tunguu baada ya kukabidhi
mabati 24 yenye thamani ya shilingi laki tatu kwa familia ya mzee Ali
Nyau Mavangu na Bi. Tamasina Thomas, ambao nyumba yao ilianguka kutokana
na mvua zinazoendelea.
Mwakilishi
huyo alisema, kipindi hichi ambacho wananchi wengi wameathiriwa na
mvua, ndicho muafaka kwa viongozi wa majimbo walioshinda uchaguzi,
kufanya mrejesho kwa wapiga kura wao.Hata hivyo, alisema jambo la kutoa
msaada halipaswi kufanywa na viongozi hao wa majimbo pekee, bali ni
wajibu wa kila mmoja kwa uwezo alionao.
Alifahamisha
kuwa baada ya kupata taarifa za familia hiyo yenye watoto kadhaa
kuangukiwa na nyumba yao usiku wa Aprili 16, mwaka huu, yeye na mbunge
wa jimbo hilo Khalifa Salum pamoja na madiwani, wameamua kutoa mabati
hayo kuifuta machozi familia hiyo.
Mbali
na mabati hayo, pia ameahidi kutoa msaada mwengine wa madirisha na
kifusi kwa wananchi hao ambao sasa wanapata usumbufu wa pahala pa kulala
kwa amani kutokana na mvua zinazonyesha.Wakitoa shukurani
zao, baba wa familia hiyo mzee Ali Nyau na mkewe Tamasina Thomas,
walisema msaada huo umewapa faraja kwani utawawezesha kupata sehemu
nzuri ya kujistiri.
Walieleza
kufurahishwa sana na viongozi wao kwa hatua ya haraka waliyochukua
kuwasaidia, mara baada ya kupata taarifa za maafa yaliyowapata.“Hatuna
neno linaloweza kutosha kuelezea shukurani zetu, lakini kubwa ni
kuwaombea dua viongozi wetu hawa Mwenyezi Mungu awazidishie moyo wa
imani na waendelee kuwa pamoja nasi katika shida na raha,”
walisema.Aidha, walisema kufuatia kupata msaada huo, wametambua kwamba
kura zao hazikupotea na zimekwenda kwa watu sahihi
No comments:
Post a Comment