TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, April 26, 2016
Bunge Sports Club kamili kucheza dhidi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar jioni ya leo
Timu ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania, Bunge Sports Club jioni ya leo kinatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo maalum na wa kwanza dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mchezoutakaochezwa uwanja wa Amaan, Unguja.
Tayari asubuhi ya leo kikosi hicho cha timu ya Bunge kimefanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo huo wa jioni ambao unatarajia kuchezwa majira ya saa 12:45 Jioni katika uwanja wa Amaani. Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto amebainisha kuwa lengo la mchezo huo ni kiuimalisha Muungano ambapo pia michezo ni afya hivyo mchezo utakuwa ni wa ushindani na wa kuvutia kwa pande zote mbili.
“Tunawaomba wabunge wote kutuunga mkono katika mchezo huu kwani tmu imejindaa vya kutosha kuhakikisha tunashinda wetu huu wa leo Aprili 26 katika uwanja wa Amaan karibuni watu wote kutushuhudia tutakavyoonyesha uwezo wa hali ya juu katika michezo” alieleza Mh. Mwamotto.
Naye Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani ‘Maji Marefu’ ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa timu hiyo ya Bunge amewaomba wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapiga hatua kwani timu ni nzuri na ina hali ya ushindi kwa pande zote hivyo anahakika na kuibuka na ushindi kwa mchezo wa leo.
Kwa upande wake Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Bunge amewataka wabunge wote wanaounda timu hiyo kuzingatia maelekezo ya Kocha pamoja na kuzingatia taratibu za mchezo wa soka ilikuweza kupata ushindi mnono.
Kwa upande wa Kapteni mpya wa timu hiyo, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Mh. Sixtus Mapunda amesema kikosi cha timu yake kimejiandaa vya kutosha na kiko kamili kwa mchezo huo wa jioni ya leo huku akiahidi ushindi mkubwa.
Mchezo huo wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ni maalum kwa ajili ya maadhimisho ya Muungano wa Nchi ya Jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambapo jioni ya leo viongozi mbalimbali watajumuika kushuhudia mchezo maalum.
Kikosi cha Bunge chenye wachezaji zaidi ya 19 kimejiandaa vya kutosha katika kuakikisha inapata ushindi mnono ambapo kimepiga kambi visiwni hapa kwa siku kadhaa hivyo mchezo huo utakuwa ni wa ushindani kwa pande zote mbili licha ya timu ya Baraza la Wawakilishi ambayo imejaa vijana wengi yenyewe ikiwa imejificha katika kambi yao nje ya mji wa Unguja.
Aidha, mbali na mchezo huo, pia kutakuwa na michezo mingine ikiwemo mchezo wa Ligi ya Zanzibar pamoja na mchezo maalum ambapo Wekundu wa Msimbazi Simba Sc ikitarajiwa kushuka dimbani kucheza na moja ya timu ya Visiwani hapa mchezo ambao ni wa kirafiki katika kunogesha Muungano huo.
Kapteni mpya wa timu ya Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Mh. Sixtus Mapunda akifanya mazoezi ya mwisho mwisho asubuhi ya leo katika uwanja wa Amaan, Unguja
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni akiwa katika mazoezi hayo leo uwanja wa Amaan
Mbunge wa Mbulu Vijijini , Mh.Flatei Massay akifanya mazoezi katika kujiandaa na mchezo huo wa leo jioni
Read more »
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment