Mhandisi mitambo wa Azam TV, (kushoto), akiwapatia maelezo ya juu
ya chumba cha uthibiti matangazo, (control room), wabunge wa
EALA-Tanzania walipotembelea studio za Televisheni hiyo, Tabata jijini
Dar es Salaam, Aprili 22, 2016.
NA: Mwandishi Wetu.
WABUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania,
wamewafagilia wafanyabiashara wakubwa hapa nchini, Dkt. Reginald Mengi
na Mzee Said Salim Bakhresa, kwa uthubutu wao wa kutambua na kuzitumia
fursa zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwahimiza
watanzania wengi kuiga mfano huo.
Pongezi hizo walizitoa Aprili 22, 2016 wakati walipotembelea
studio za Azam Media, mwishoni mwa ziara yao ya kuvitembelea vyombo vya
habari kwa lengo la kuhamasisha umma wa Watanzania kuchangamkia fursa
kwenye Jumuiya hiyo ambayo mwenyekiti wa wabunge hao Mh. Charles
Makongoro Nyerere ameiita kuwa ni jumuiya ya watu wa Afrika Mashariki
na sio ya viongozi.
“Napenda kumpongeza sana mzee Said Salim Bakhresa kwa kutambua
fursa zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo Azam TV
inaonekana kwenye nchi kadhaa wanachama wa Jumuiya lakini pia bidhaa za
Azam zimesambaa karibu Afrika Mashariki na Kati, na Mzee Mengi pia
anastahili pongezi kwa utambuzi wao wa fursa zilizopo kwenye Jumuiya.”
Alisema Mh. Shy-Rose Bhanji, ambaye alikuwa miongoni mwa wabunge hao.
Kuna haja ya watanzania kuondokana na dhana ya kujiona wanyonge
kwenye Jumuiya hii kwani wanatakiwa kuchangamkia kila fursa iliopo,
mfano mimi ni mwalimu wa hisabati, ukijumlisha na Kiswahili, unaweza
kupata kazi huko Sudani Kusini na maeneo mengine ya Afrika Mashariki,
kwani walimu wa Kiswahili wanahitajika sana, unachopaswa ni kujiongeza
tu, unakuwa na kitu kingine cha ziada.” Alisema Mh. Nderaikindo Kessy.
Kwa upande wake, Mh. Abdulla Mwinyi, alisema, wabunge wa EALA
kutoka Tanzania, wamefanya jitihada hizo za kutembelea vyombo vya habari
kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na waandishi wa habari katika
kuhabarisha umma na vyombo vya habari vinao mchango mkubwa wa kutangaza
kwa kina fursa za kiuchumi kwenye Jumuiya.
Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kituo cha televisheni cha Azam
TV, Mkurugenzi wa uendeshaji vipindi wa Azam TV, Yahya Mohammed
alisema, malengo ya Azam TV ni kufika kufanya kazi zake kwenye nchi zote
za Afrika Mashariki, na Kati, ambapo kwa sasa wana soko zuri tu DRC,
Rwanda, Uganda. Kenya na Burundi zinajikongoja lakini matumaini makubwa
ya kulishika soko la nchi hizo yapo.
Mh. Shy-Rose Bhanji, (kulia), na Mkurugenzi wa TV, Bi. Jane Shirima
Mkurugenzi wa uendeshaji vipindi wa Azam TV, Yahaya Mohammed,
(wapili kushoto), akizungumza wakati akitoa taarifa yake kwa wabuneg hao
Mkurugenzi wa uendeshaji vipindi wa Azam TV, Yahaya Mohammed,
(wapili kushoto), akizungumza wakati akitoa taarifa yake kwa wabuneg
hao. Wanne kulia ni Mkurugenzi wa TV, Jane Shirima
Mkuu wa chumba cha habari Azam TV, Bw. Hassan Mhelela, akizungumza
wakati wabunge hao (hawapo pichani), walipotembelea chumba cha habari
Bw. Mhelela akimpokea Mh. Shy-Rose Bhanji
Mh. Nderaikindo Kessy
Mh. Shy-Rose Bhanji
Mh. Abdulla Mwinyi
Mh. Nderaikindo Kessy
Mh. Shy-Rose Bhanji, akipokewa na Bi. Jane Shirima
Mh. Shy-Rose Bhanji
Picha ya pamoja, wabunge na uongozi wa Azam TV
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda, (wapili kushoto),
Mh. Makongoro Nyerere, (wakwanza kushoto) Mh. Shy-Rose Bhanji (wakwanza
kulia) na msanii nguli, Mrisho Mpoto, (mjomba), wakiwa kwenye picha ya
pamoja kwenye chumba cha wageni Azam TV, waheshimiwa hawa walikutana.
wakati Mh Mkuu wa mkoa na "mjomba" walifika kwenye mahojiano maalum
kuhusu kampeni ya usafi, wabunge walifika kwa ziara ya kikazi
No comments:
Post a Comment