TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, April 26, 2016
HOSPITALI YA TENGERU INAKABIRIWA NA UHABA WA VITANDA
Na Woinde Shizza,Arusha
Hospitali ya wilaya ya Tengeru (Patandi) inakabiriwa na ukosefu wa vitanda ,hali inayopelekea baadhi ya wagonjwa kulala zaidi ya mmoja katika kitanda kimoja.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii,Wagonjwa hao mara baada ya kupokea msaada wa vyandarua kutoka kwa wafanyakazi wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) tawi la Arusha, walisema kuwa wao kama wagonjwa wa hospitali hiyo wamekuwa wakipata tabu sana haswa wakati wakiandikiwa kulazwa,kwani wamekuwa wakibanana sana na wakati mwingine wamekuwa wakikosa kabisa vitanda.
Mmoja wa wagonjwa hao ambaye alijitambulisha kwa jina la Anna Akyoo alisema kuwa wamekuwa wakilala wagonjwa wawili hadi watatu hali ambayo imekuwa ikiwafanya wajisikie vibaya kwani wana banana sana katika vitanda hivyo vichache.
picha ikionyesha wafanyakazi wa NSSF pamoja na Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Tengeru katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua
wafanyakazi wa NSSF wakiwa wanabadilishana mawazo nje ya hospitali hiyo
mmoja ya wagonjwa akiwa amekaa kitanda kimoja na watoto wawili wakiwa kila mmoja ana mama yake.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment