Siku ya Malaria
Duniani inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 25, ni moja ya siku adhimu inayopaswa
kuzingatiwa na kutiliwa maanani.Maadhimisho hayo yalianza
kuadhimishwa tangu mwaka 2001 inatoa nafasi kwa Wataalamu wa Afya na Wananchi
kwa jumla kuchambua kwa kina utekelezaji wa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa
Malaria kwa kila mwaka.Siku hiyo inatoa
nafasi ya kuangalia tulikotoka, tulipo na tunakokwenda katika suala zima la
kufanikisha mapambano dhidi ya malaria.
Juhudi hizo kupambanana ugonjwa wa malaria sio za kuachiwa Serikali tu, kila mtu awajibike na atambuekuwa zama zimebadilika, “Sio kila homa ni malaria, nenda ukapime” na “lalakwenye chandarua kila siku” kujikinga na malaria.
No comments:
Post a Comment