Rais
Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete akiwa pamoja na uongozi
na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma chuo cha Kilimo na Misitu FAFU.
Dkt Kikwete akiwa katika chuo cha Kilimo FAFU ambapo alialikwa kutembea leo hii.
Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana Aprili
23, 2016 alitembelea Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha jimbo la Fujian
(Fujian Agriculture and Forest University-FAFU) kilichopo katika mji
mkuu wake Fu Zhou.
Mwenyekiti
alikaribishwa chuoni hapo kuonyeshwa hatua ambazo jimbo hilo imepiga
katika kuendeleza kilimo cha kisasa, teknolojia ya kuzalisha mbegu na
teknolojia ya kupambana na magonjwa na wadudu waharibio mazao. Akiwa
chuoni hapo, alikutana pia na wanafunzi wa kitanzania wanaosomea shahada
za uzamivu kwa ufadhili wa serikali ya China.
Katika
mazungumzo yake na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Lan Siren, Mhe Kikwete
amependekeza kuanzishwa kwa mahusiano na ushirikiano baina ya Chuo Cha
Kilimo SUA na Chuo hiko. Pia amependekeza wanafunzi na wakufunzi wa
chuoni hapo kuja Tanzania kufanya mafunzo ya vitendo na tafiti zao.
Kufuatia
pendekezo hilo, Rais wa Chuo hicho ameelezea utayari wa Chuo hicho
kushirikiana na SUA. Aidha, ameelezea kulipokea ombi la Mwenyekiti la
kuongeza nafasi za masomo kwa vijana wa Tanzania na kuahidi kulifanyia
kazi ombi hilo.
Chuo
Kikuu cha FUFA kina takribani wanafunzi elfu arobaini (40,000) ambapo
wanafunzi kutoka Afrika ni takribani 120 kati yao watatu tu (3) wanatoka
nchini Tanzania.
Mhe
Kikwete yuko nchini China kwa ziara ya kichama iliyotokana na mualiko
rasmi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China na Katibu Mkuu wa
Chama Cha Kikomunisti cha China Mhe Xi Jinping.
No comments:
Post a Comment