Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa
Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake
bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na
Biashara, Charles Mwijage.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Dk. Koon ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 27, 2016), wakati
alipomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma,
na kwamba Singapore ipo tayari kutoa fursa kwa wataalam wa Tanzania
kwenda kufanya kazi katika Bandari ya Singapore ili kupata uzoefu
utakaosaidia uendeshaji wa bandari za Tanzania.
Dk. Koon ambaye ameambatana na wafanyabiashara wakubwa wapatao 40,
amemweleza Waziri Mkuu kwamba kampuni ya Hyflux ya Singapore imeanza
kuwekeza nchini kwa kujenga eneo maalum la uchumi (Special Economic
Zone) mkoani Morogoro ambapo ndani ya kipindi cha miaka mitano
wanatarajia kujenga miundombinu wezeshi ya kuweka viwanda vya kati
(light industries), maeneo ya biashara na nyumba za makazi zipatazo
37,000.
“Jiwe la msingi la mradi huo litawekwa tarehe 29 Aprili 2016 na Waziri
wa Biashara,Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage,” alisema.
Mbali na ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji, Dk Koon
amweleza Waziri Mkuu kwamba nchi yake itaisaidia Tanzania kujenga uwezo
wa kiufundi katika maeneo mbalimbali ya menejimenti na uendeshaji wa
bandari na ufundi katika sekta ya gesi na mafuta.
“Hadi sasa makampuni ya Singapore yaliyowekeza nchini ni pamoja na
Pavillion Energy ambayo imewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni
1.2 katika sekta ya gesi na inatarajia kuwekeza zaidi dola za kimarekani
bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa kinu cha kuchakata gesi (LNG plant)
kitakachojengwa mikoa ya Kusini kwa ubia na makampuni ya gesi kutoka
Ulaya na Marekani”.
Amesema kampuni ya PIL ya Singapore inatarajia kuwekeza Dola za
Kimarekani milioni 400 kwa ajili ya kuanzisha kituo cha kutoa huduma kwa
makampuni ya gesi.
No comments:
Post a Comment