TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 20, 2012

“CHAGGA DAY” yaikaribisha Krismasi Uchagani



“CHAGGA DAY” yaikaribisha Krismasi Uchagani

Katika kuzikaribisha sikukuu za Krismasi na mwaka mpya, tamasha la kihistoria la siku ya wachaga kufanyika siku ya Jumamosi Tarehe 22-12-2012 katika viwanja vya Ushirika, Moshi Mjini, Kilimanjaro kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka usiku.

Tamasha hili linalenga kuhamasisha jamii ya kabila hilo na makabila mengine kuenzi mila na tamaduni. Vilevile, kuhamasisha jamii na falimia zao zilizopo ndani na nje ya mikoa yao kukumbuka nyumbani na kutembelea wazee mara kwa mara.

Tuna imani kubwa kuwa zaidi ya watu 3,000 na familia zao, watahudhuria kwa wingi tamasha hili la kihistoria huku wakipata fursa ya:

Ø  Kusikia historia ya wachagga kwa kina toka kwa wazee wanatoka kwenye familia za wafalme na machief “MANGI MKUU” wa kichaga waishio mkoani Kilimanjaro.
Ø  Kuona na kucheza ngoma zote za asili za kichaga pamoja na vikundi tofauti tofauti vya ngoma za asili na sanaa za makabila mengine.
Ø  Kula aina zote za vyakula vya asili vya kichagga kama kiburu, kisusio, mtori, ndafu, shiro, kiumbo, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande n.k   
Ø  Kunywa vinywaji vyote vya asili vya kichagga kama mbege, dadii n.k
Ø  Kupata burudani kutoka bendi ya Akudo Impact, Msanii Costa Siboka kutoka Dar es Salaam na wasanii wote kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Tumewaalika viongozi wa serikali yetu, wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro, viongozi wa asasi zisizo za kiserikali pamoja na asasi za serikali yetu, wakurugenzi wa makampuni ya utalii na hoteli kubwa za mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Tumejipanga vizuri katika kufanikisha siku za makabila yote Tanzania kila mwaka tukianza na makabila wa kaskazini, lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kuenzi mila na tamaduni za makabila yetu na kukumbuka kuzipeleka familia zetu nyumbani tuwapo nje ya mikoa yetu.

Imedhaminiwa na;-
Safari Lager, Pepsi, Konyagi, Precision Air, Radio 5 FM, Toyo, Samsung, Michuzi Blog Spot, Zizou Fashion, Mlonge Bi Makai, Egesha Trading Agency, Delina Group Enterprises and Albert Msando Legal Consultant.  

Waandaaji:      MyWay Entertainment Company.
Mkurugenzi Mkuu: Paul Siboka. Mganga
                       

No comments:

Post a Comment