TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, September 10, 2013

RAIS KABILA ATOA TAMKO ZITO DRC

Posted: 08 Sep 2013 09:08 PM PDT
  • OPERESHENI YA JK YAIBUA MAKUBWA
  • MWANAMKE ASALIMISHA SMG POLISI

Na Mwandishi Wetu

OPERESHENI y a kuwaondoa wahamiaji haramu, kuwakamata watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, imeanza kuzaa matunda ambapo bastola 38 na bunduki za kivita zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uhalifu, zimerejeshwa polisi.


Kurejeshwa kwa silaha hizo kumetokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa hivi karibuni akiwataka wahamiaji haramu kurejea katika nchi zao ndani ya wiki mbili na watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wazisalimishe

 Akizungumza na Majira katika mahojiano maalumu kuhusu operesheni iliyoanza Agosti mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma, Bw. Venance Mwamotto, alisema operesheni hiyo ambayo ni endelevu, imelenga kukomesha vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha mkoani humo.

Alisema operesheni ya salimisha silaha kwa hiari na utoaji siri za watu wanaojihusisha na matukio ya uhalifu, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi mkoani humo, wananchi na viongozi wa mkoa huo.

“ H a d i s a s a b a s t o l a zilizosalimishwa ni 38 na bunduki za kivita SMG ni mbili, moja ilipelekwa katika Kituo cha Polisi Kibondo na mwanamke, Bi. Erica Josamu (35), mkazi wa Kibondo (picha yake ipo ukurasa wa mbele).“Kati ya watu waliorejesha silaha hizo zinazoweza kutumika kwenye vita ni mmoja ambaye ameonesha ujasiri, nasi hatukusita kumzawadia kwa hiari,” alisema.

Al i o n g e z a k uwa , k a t i k a mahojiano ya awali na mwanamke huyo, alisema silaha hiyo aliiokota njiani na kuamua kuifikisha kituoni hapo, lakini baadaye alikiri kuimiliki na kuitumia kinyume cha sheria na hakuchukuliwa hatua zozote.

“Hatukumchukulia hatua kwa sababu tulitangaza watu warejeshe silaha wanazomiliki kinyume cha sheria kwa hiari yao, hakukuwa na adhabu yoyote kwa watu walioziwasilisha polisi,” alisema.

Bw. Mwamo t t o a l i s ema wamefanikiwa kuokota silaha nyingi zilizotupwa na wananchi hasa maeneo ya Kambi ya Nduta, ambayo walikuwa wakiishi wakimbizi ambapo eneo hilo lilikuwa maficho ya majambazi sugu.Alisema maeneo mengine yaliyookotwa silaha ni Kamuhasha, Kumbanga na Kanembwa ambapo kulikuwa na matukio mengi ya uhalifu wa kutumia silaha.

“Majambazi sugu kutoka Burundi kwa kushirikiana na wakimbizi, walikuwa wakifanya uhalifu na kukimbilia katika Kambi ya Nduta hivyo maficho yao tumeyasambaratisha na kuongeza ulinzi.

“ P i a k a t i k a k amb i h i i tumefanikiwa kugundua shamba la bangi ambayo baada ya kuvunwa ilipatikana kilo 1,500...yote tumeichoma moto, ilikuwa vigumu kubaini kama eneo husika kulikuwa na kilimo cha bangi kutokana na mazingira yalivyokuwa,” alisema.

Aliongeza kuwa, Kambi ya Nduta ni eneo ambalo lina sifa kubwa ya uuzaji dawa za kulevya, bangi na maficho ya majambazi sugu ambapo uhalifu huo ulikuwa ukifanyika bila woga.Alisema operesheni hiyo haina mwisho hadi mtandao huo utakapomalizika ambapo asilimia kubwa ya wakimbizi waliokuwa wakijihusisha na matukio hayo, tayari wameondolewa nchin

Posted: 08 Sep 2013 09:15 PM PDT
  •  LIPUMBA ASEMA MBOWE AMEDHALILISHWA BUNGENI 

Rachel Balama na Darlin Said

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), tukio la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuondolewa bungeni mjini Dodoma kwa agizo la Naibu Spika, Bw. Job Ndugai, lilipangwa na Serikali ili kuhakikisha Muswada wa sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2013, unapitishwa bungeni ili kulinda masilahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CHADEMA, Bw. John Mnyika, ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.Alisema Serikali ilipanga kupitisha muswada huo bungeni ndio maana hata Bw. Mbowe kama Kiongozi wa Upinzani bungeni, aliposimama kutaka kuzungumza, hakupewa nafasi hiyo badala yake alitakiwa akae na alipokataa Bw. Ndugai aliagiza atolewa nje jambo ambalo hawakuliunga mkono.

Aliongeza kuwa, Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wabunge wa CCM wanakuwa wengi katika Bunge la Katiba ili kupitisha mambo wanayoyataka."Kilichopitishwa bungeni na wabunge wa CCM ni kibaya kuliko ilivyokuwa awali...wameharibu zaidi, CHADEMA imepinga kwa masilahi ya makundi mengine ya kijamii ili yaweze kupata uwakilishi katika bunge hilo," alisema.

Bw. Mnyika alisema CHADEMA walipendekeza Bunge la Katiba lipunguze uwakilishi wa chama kimoja ambapo katika kipengele cha wajumbe 166 wanaoteuliwa na rais, iongozwe na kufikia wajumbe 359 lakini Serikali imekataa."Lengo letu ni kutoa nafasi kwa makundi mengine ya kijamii kama wakulima, wafanyabiashara, wafanyakazi na taasisi nyinginezo kutoa wawakilishi wao kwenye bunge hili," alisema.

Alisema upande wa Zanzibar, hakukuwa na wawakilishi waliotoa maoni yao juu ya nafasi ya Zanzibar katika bunge hilo na kilichosemwa na Serikali ni uongo."Serikali baada ya kushindwa kuchakachua Mabaraza ya Katiba, sasa imeona njia pekee ya kufanya hivyo ni kuhakikisha kwenye Bunge la Katiba wabunge wa CCM wanakuwa wengi," alisema.

Akizungumzia uamuzi wa Bw. Ndugai kumtoa nje Bw. Mbowe, alisema Naibu Spika amevunja kanuni ya 76 ya Bunge kwani hana nguvu ya kuita askari ambapo kwa mujibu wa kanuni ya 20, alitakiwa kuhairisha shughuli za Bunge."Ndugai amefanya kosa la kuwaingiza watu wasiohusika bungeni na kuruhusu vitendo vya uhalifu vitokee ili kupitisha muswada walioutaka na kulinda masilahi ya chama kimoja.

"Sekretarieti ya CHADEMA itakutana kesho (leo) ili kujadili kwa undani suala hili na kulishughulikia, pia tutatumia nguvu ya umma (wananchi) kuhakikisha katiba haivurugwi, tutakutana na vyama vingine vya upinzani," alisema.Alisema chama hicho hakioni sababu ya kuharakisha katiba badala yake kama wanataka katiba hiyo itumike katika Uchaguzi Mkuu 2015 ni vyema ikaandaliwa ya mpito.

Aliongeza kuwea, katika Bunge lijalo Sheria ya Kura za Maoniambayo itajadiliwa ni ya hatari zaidi kuliko Bunge la Katiba na isipofanyiwa marekebisho, itazusha mgogoro mkubwa zaidi.Katika hatua nyingine, Chama cha Wananchi (CUF), kimepinga kitendo cha askari wa Bunge, kumtoa nje Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Bw. Freeman Mbowe, baada ya kuzuiwa kuzungumza.

Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.Alisema kitendo cha Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, kuwaagiza askari wa Bunge wamtoe nje Bw. Mbowe, hakiwezi kukubalika, bali ni unyanyasaji na udhalilishaji mkubwa.

"Ni kitendo cha aibu na hakikupaswa kufanywa na Naibu Spika (Ndugai), CUF tunajiuliza angesimama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kutaka kuzungumza angemnyima?" alihoji.Alisema Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2013, ulikuwa na utata mkubwa kwani Serikali imeubadili kwa kuondoa maoni muhimu ya wadau ambapo Wazanzibari hawakushirikishwa ipasavyo.

"CUF tunataka muswada huu urejeshwe kwa wananchi ili ujadiliwe upya, mbali ya Mbunge wa Singida Mashariki (Tundu Lissu- (CHADEMA) na Naibu Katibu Mkuu wa CUF upande wa Zanzibar (Hamadi Masoud), kuthibitisha kuwa Zanzibar haikushirikishwa, wabunge wetu hawana taarifa kama wananchi wao walishirikishwa.

"Kuupitisha muswada huu ni njama za wazi za Serikali na kiti cha Spika kutelekeza maoni ya wananchi na kuyapatia kipaumbele ya CCM, hivyo kuondoa uhalali wa Bunge na kiti cha Spika katika kusimamia mchakato wa kutafuta Katiba Mpya," alisema.Katika hatua nyingine, Prof. Lipumba muswada huo unampa Rais Jakaya Kikwete, mamlaka ya kuteua watu anaowataka kuwa wajumbe wa Bunge la kutunga sheria.

Aliongeza kuwa, hivi sasa kila taasisi itapaswa kuteua majina tisa na kumpa Rais ambaye atateua jina moja au asiteue kabisa,CCM na Serikali wanajua hujuma wanazofanya katika mchakato huu ili kupata katiba wanayoitaka wao si wananchi," alisema.Alisema upo umuhimu wa wananchi kuunga mkono msimamo wa wabunge wa upinzani na kudai kuwa, watendaji wa Serikali wakiwemo Mawaziri na Naibu Spika, wanamhujumu Rais Kikwete asifanikishe mchakatato wakupata Katiba Mpya.

Alisema muswada wa kwanza wa Mabadiliko ya Katiba ulikuwa mbovu ambapo Rais Kikwete alilazimika kuzungumza na wapinzani ili kuurekebishaWakati huo huo, CUF imedai kusikitishwa na kitendo cha kupigwa na kutupwa nje ya lango la Bunge Mbunge wa Mbeya Mjini, Bw. Joseph Mbilinyi (CHADEMA), na kuvuliwa hijab kwa Mbunge wa Viti Maalum, Bi. Mozza Abeid (CUF) na kudai huo ni udhalilisha usiokubalika.
Posted: 08 Sep 2013 09:17 PM PDT

 Na Said Hauni, Lindi

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe, amewaomba radhi wananchi wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi kwa kutoonekana jimboni kwake muda mrefu.Alisema hali hiyo imechangiwa na majukumu aliyonayo kitaifa, kimataifa na kuahidi kutumia muda wa likizo kufanya ziara katika jimbo hilo ili aweze kuzungumza na wananchi
.Bw. Membe aliyasema hayo juzi wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ili kumpata Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) wa chama hicho, uliofanyika kwenye Kata ya Kiwalala, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi. 

A l i s e m a m a j u k u m u aliyoongezewa serikalini, yamechangia kwa kiasi kikubwa kutofika jimboni kwake mara kwa mara hivyo hutuia muda mwingi kutekeleza majukumu hayo."Si kwamba nafanya makusudi, leo nimewaomba radhi lakini simaanishi kuanzia sasa muda wote nitakuwa jimboni si kweli, nazungumza hivi ili mnielewe," alisema Bw. Membe.

Alisema yeye ataendelea kuwapenda wapigakura wake ambao ndio waliompa nafasi ya kuwa mbunge wao hivyo kutoonekana kwake jimboni kusiwanyong'onyeze.Wakati sijaongezewa majukumu, nilikuwa nakuja kila mwezi lakini hivi sasa nashindwa kufanya hivyo, nimeelemewa na mzigo mzito, baadhi yenu mnafahamu hilo,," alisema
Posted: 08 Sep 2013 09:19 PM PDT

 Na Eliasa Ally, Kilolo

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uendezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye, amesema vyama vya upinzani nchini, vitaendelea kuwa na ndoto ya kushika dola kwani havina sifa hiyo zaidi kuvuruga amani na kufanya vurugu.Alisema CCM inalaani vurugu zilizofanywa na upinzani wiki iliyopita bungeni mjini Dodoma na kuwataka watambue dhamana waliyonayo katika Bunge hilo kwa masilahi ya nchi, wapigakura.


Bw. Nnauye aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Ruahambuyuni, Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, wakati akizindua mbio za bendera ya CCM inayokimbizwa mkoani humo na kuwaeleza wananchi utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Aliongeza kuwa, wabunge wa upinzani wamepewa dhamana na wananchi ili kutetea masilahi yao si kupigana ngumi katika Ukumbi wa Bunge na kumtaka Mbunge wa Mbeya Mjini, Bw. Joseph Mbilinyi (CHADEMA), kutafuta ukumbi wa kupigania.

"Kama Bw. Mbilinyi anajiamini kwa kuwa na uwezo wa kupigana, atafute ukumbi ili wananchi walipe kiingilio si kuharibu sifa ya Ukumbi wa Bunge, lazima atambue thamani aliyonayo kwa wananchi.

" H a t a Mw e n y e k i t i w a CHADEMA (Freeman Mbowe), atafute kazi nyingine ya kufanya kama ubunge umemshinda... wananchi mnapaswa kufanya maamuzi magumu katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kuwanyima kura wabunge wa upinzani ambao hawaendi bungeni kujadili masilahi yao," alisema.

Alisema vyama vya upinzani vimegeuka kuwa vibaraka wa wakoloni vikitumika kugombanisha wananchi, kuvuruga amani, umoja na mshikamano uliopo.

Bw. Nnauye alisema, CCM itaendelea kutawala nchi, kushika dola kwani hawapo tayari kuona Tanzania ikiongozwa na watu wasio na chembe ya uadilifu na chanzo cha vurugu ambazo zinachangia vifo kwa baadhi ya wananchi.

"CHADEMA wanapoanzisha vurugu, viongozi wao huwa hawapatwi na madhara yoyote, matokeo yake husababisha vijana wasio na hatia kupoteza maisha katika vurugu zao na wao hukimbia," alisema Bw. Nnauye.

Alisema upinzani wamefanikiwa kuchukua baadhi ya majimbo kwa sababu ya wana CCM wenyewe kwa wenyewe kutoelewana katika majimbo husika, hivyo aliwataka kuwa na mshikamano ili kutotoa nafasi kwa upinzani katika Uchaguzi Mkuu 2015.

"Viongozi wa CCM katika ngazi zote, wana haki ya kuwabana kikamilifu Wakuu wa Wilaya ili watoe taarifa za maendeleo yaliyofanywa na Serikali yao, akikataa tunamuomba aachie ngazi mwenyewe.

"Viongozi wazembe wasioweza kutekeleza Ilani ya CCM, kuendana na kasi tunayotaka, hatumhitaji kwani wanatuangusha na kutufanya tueleweke vibaya kwa wananchi," alisema.
Posted: 08 Sep 2013 09:30 PM PDT

 Na Rashid Mkwinda, Mbeya

AS ILIMIA 4 0 y a mapato ya Mkoa wa Mbeya yanatokana n a s h u g h u l i z a kiuchumi katika sekta za viwanda,biashara na kilimo huku asilimia 80 ya wakazi wake wakijishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara.


Akizungumza na timu ya waandishi wa habari waliokuwa katika mafunzo ya habari za Biashara na Uchumi, Mkoa wa Mbeya, Mchumi wa Mkoa, Rukia Manduta, alisema asilimia 40 ya mapato hayo yanatokana n a uwe k e z a j i k a t i k a viwanda, madini, biashara na usafirishaji.

Alisema kuwa serikali inaendelea kuimarisha miundo mbinu katika barabara ambapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe umeongeza chachu kwa wakulima kupata fursa ya kusafirisha mazao ya kilimo kama vile maua mboga mboga na matunda.

Alisema uwekezaji katika sekta ya utalii umeendelea kuimarika kwa Bonde la Ihefu lililopo wilayani Mbarali kuingizwa katika Hifadhi ya Taifa ilhali Ziwa Rukwa lililopo wilayani Mbozi na Chunya na Ziwa Nyasa lililopo katika wilaya ya Kyela yanasaidia pato la mkoa katika sekta ya usafirishaji na uvuvi.

Kwa upande wake Ofisa Biashara wa Mkoa wa Mbeya, Joseph Semu alizitaja baadhi ya changamoto zinazochangia kukosekana kwa wawekezaji wakubwa kuwa ni pamoja na uhaba wa maeneo na kwamba kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ameunda timu ya watu sita ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Semu alisema kuwa timu iliyoundwa na mkuu wa mkoa imechukua wataalamu kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo mkoa wa Mbeya(SIDO),TCCIA,TIC, Mhadhiri wa chuo kikuu Mzumbe, na wataalamu wawili kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa.

Awali, akizungumza na Katibu Tawala msaidizi wa Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha, mkufunzi wa mafunzo ya habari za Biashara na Uchumi kwa waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya, Mnaku Mbani alisema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa wanahabari ni kuwajengea uwezo wanahabari kuandika habari za biashara na uchumi.

Alisema fursa hiyo kwa wanahabari imelenga kuibua changamoto za kiuchumi kwa Mkoa wa Mbeya kwa nia ya kupatiwa ufumbuzi na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo.
Posted: 08 Sep 2013 09:24 PM PDT

 KINSHASA, DRC

RAIS Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), amesema hayupo tayari kuruhusu mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na waasi, eneo la Afrika ya Kati.Alisema mapigano hayo yanaweza kuligawa Taifa hilo ambapo jeshi la nchi hiyo litaendelea kulinda amani na kuchukua hatua kwa yeyote anayejaribu kuivuruga.


Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW), Rais Kabila aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa mwishoni mwa wiki mjini Kinshasa wakati akifungua mkutano wa maridhiano ya kitaifa nchini humo.

Hata hivyo, mkutano huo ulisusiwa na baadhi ya vyama vya siasa kutoka upinzani ambapo mazungumzo ya amani kati ya Serikali ya Congo na waasi wa M23 yanatarajiwa kuanza leo.Hali hiyo inatokana na ongezeko la vurugu karibu na eneo la mpaka wa Congo na nchi jirani ya Rwanda ambapo kundi la M23, lilianzisha uasi Mashariki mwa Kongo na kufanikiwa kuudhibiti Mji wa Goma kwa muda mfupi
Posted: 08 Sep 2013 09:33 PM PDT

Na Grace Ndossa 

WAZIRI wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, F e n e l l a Mu k a n g a r a , amewataka waandishi wa habari kujiendeleza kielimu ili sheria itakapopitishwa waweze kuwa na vigezo vinavyotakiwa.Hayo alibainisha mwishoni mwa wiki mjini Dodoma alipokuwa anazungumza na kikundi cha waandishi wa habari (Habari Group) na kueleza kuwa sheria itakuwa inawabana kama watakuwa hawajafikia vigezo.

A l i s e m a k u w a n i vyema waandishi wa habari wakaongeza elimu waliyonayo kwani walio wengi hawajafikia kiwango kitakachowekwa katika sheria ya habari."Nasisitiza mjiendeleze kielimu ili kufikia vigezo vitavyopitishwa na sheria ya habari kwani elimu ni muhimu na mjitahidi kuandika habari kwa umakini na usahihi," alisema Mukangara.

Pia alisema katika Wizara ya Habari yangu ina fursa nyingi za vijana,hivyo mnatakiwa kujitokeza na kutumia fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi.Alisema vijana wanaweza kujiunga kwenye vikundi na kufika katika wizara hiyo kuelezea kitu wanachotaka k u f a n y a i l i wawe z e kusaidiwa na mikopo, kwani ipo ambayo mtu atarudisha kwa riba nafuu.Hata hivyo, alisema kuwa vijana wengi wana fursa nyingi hivyo ni muhimu wajiunge kwenye vikundi kwani fursa za kilimo kwanza zipo.
Posted: 08 Sep 2013 09:39 PM PDT

 Na Mwandishi Wetu

UO N G O Z I w a Mamlaka ya Ukanda M a a l u m u w a Uwekezaji (EPZA) ume s ema u t a e n d e l e a kutekeleza mpango wa Serikali wa maendeleo wa miaka mitano kwa kuhakikisha inaendelea kuweka mazingira ya kuvutia wawekezaji katika sekta ya viwanda ili kuharakisha shughuli za maendeleo nchini.


Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Dkt. Adelhelm Meru, alibainisha hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, ambapo alifafanua maendeleo ya miradi na uwekezaji katika ukanda huo kwa miaka sita iliyopita.Alisema EPZA inaweka nguvu kubwa kwenye maendeleo ya viwanda kwa kuwa sekta hiyo ni msingi mkubwa wa maendeleo ya nchi yoyote duniani na kwamba Tanzania haiwezi kuachwa nyuma kwa hilo kama kweli inataka kupata maendeleo endelevu.

"Historia ni shahidi kuwa viwanda ndiyo moja ya misingi muhimu ya maendeleo," alisema na kuongeza kuwa ndiyo maana taasisi yake inafanya kila linalowezekana kuhakikisha sekta hiyo inakua hapa nchini.

"Taasisi hii inatekeleza kwa vitendo mpango huo wa maendeleo na tumedhamiria kuongeza nguvu zaidi," alisema.A l i s e m a m o j a y a vipaumbele vya mpango wa maendeleo wa miaka mitano ni maendeleo ya viwanda na kuwa EPZA inataka kuhakikisha kuwa hilo linafanikiwa kwa faida ya nchi nzima.

"Tunaunga mkono mpango wa maendeleo wa miaka mitano, tumedhamiria kufanikiwa katika hili," alisema. Alisema kuwa kuimarika kwa sekta ya viwanda nchini kutasaidia kuzalisha ajira mpya, upatikanaji wa teknolojia mpya na kuongeza kipato cha nchi hivyo kukuza uchumi na ustawi wa jamii.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa sekta ya viwanda katika kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa nchi, taasisi yake imejikita kuvutia wawekezaji wa ndani na nje katika sekta hiyo ili kunufaika na fursa hizo.
Awali, alisema kuwa mpaka sasa wastani wa viwanda vilivyowekeza kupitia 
Posted: 08 Sep 2013 09:42 PM PDT

Na Jovither Kaijage, Ukerewe

TATIZO la njaa katika Wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza limechukua sura mpya baada ya kuwepo taarifa za wakulima kula mbegu wanazopewa na halmashauri ya wilaya hiyo.Suala hilo limeibuliwa mwi s h o n i mwa wi k i katika kikao cha wadau wa maendeleo wa wilaya hiyo kilichojadili tatizo la njaa kwa muda mrefu.Ki k a o k i l i a n d a l iwa na mtandao wa asasi za kiraia wilayani Ukerewe ( U N G O N E T ) k w a kushirikiana na Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Mwanza (MPI) kwa kufadhiliwa na Shirika la Forum Syd .


Ofisa Kilimo wa Kata ya Namagondo, Kemimba Itogoza, alisema ni suala la kusikitisha kuona mkulima anafikia hatua ya kula mbegu alizopewa kupanda kwa sababu ya kukosa chakula.Akithibitisha kauli yake alisema katika msimu wa kilimo wa mwaka juzi kata yake, ilipokea na kugawa kwa wakulima 100 kilo 250 za mbegu ya mtama, lakini zilizopandwa ni kilo 20 pekee huku nyingine zikisagwa na kuliwa na wakulima.

Alisema katika uchunguzi wake alibaini kuwa tatizo kubwa la upungufu wa chakula katika kata hiyo ndiyo sababu kubwa ya wakulima hao kula mbegu hizo na kuongeza kuwa inahitajika juhudi kubwa za kukabili tatizo hilo.

Na y e Al l y Ms umo , akichangia hoja hiyo alisema pengine tatizo hilo la wakulima kula mbegu linasababishwa na uamuzi wa ngazi za juu kufanyika bila kuishirikisha jamii husika ambayo wakati mwingine mbegu hizo hazikuwa na mahitaji muhimu kwao.Ofisa mazao wa wilaya hiyo, William Balyahele mbali ya kubainisha kuwepo upungufu wa tani tisa za chakula msimu huu wa kilimo, pia ametaka idara hiyo ipewe nguvu za kisheria katika kusimamia shughuli zake.

Alisema wilaya hiyo ina eneo la ardhi ya kilimo ya hekta 33,765.5, ambazo zikitumika kwa kilimo cha kitaalamu zinaweza kuzalisha kilo milioni 2 za mahindi kwa msimu mmoja wa kilimo huku mahitaji ya chakula kwa mwaka yakiwa kilo milioni 1.5. za nafaka.Akifafanua aliwataka wajumbe waeleze kama wako tayari kurejea katika kilimo cha shuruti na kuchapwa mijeledi kama ilivyokuwa enzi za ukoloni.
Posted: 08 Sep 2013 09:45 PM PDT


Na Mwandishi Wetu

KA M P U N I y a mitandao ya simu za mkononi nchini, Airtel imetajwa kuwa moja kati ya kampuni ambazo zimekuwa zishirikiana na Serikali kwa dhati katika harakati za kupambana na tatizo la ajali za barabarani.Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Kikosi cha Us alama Barabarani, Mohamed Mpinga, wakati akieleza juhudi ambazo zimekuwa zikichukuliwa na kampuni hiyo.


Alisema Airtel imeweza kutoa mchango mkubwa wa kupunguza wimbi la ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa."Airtel ni wadau wakubwa wa kampeni za usalama barabarani, kwa miaka mitano mfululizo na hata mwaka huu 2013 Airtel inaendelea na udhamini wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani.

"Airtel pia imedhamini vipindi vya elimu ya usalama barabarani katika televisheni na redio, pia Airtel kwa kushirikiana na Rotary club na Jeshi la Polisi usalama barabarani imedhamini kampeni yenye ujumbe usemao Kuendesha + Simu = Kifo inayowaonya waendesha vyombo vya moto kutotumia simu wakati wakiendesha magari," alisema Mpinga.

Alisema mwaka jana Airtel ilidhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa wapanda pikipiki (bodaboda) yaliyokuwa na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki.Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel- Tanzania, Beatrice Singano Mallya, akizungumza juu ya suala hilo alisema "Airtel imeamua kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha inatokomeza kabisa wimbi la ajali za barabarani.

Alisema idadi ya vifo vinavyotokea barabarani ni kubwa mno na ndiyo maana Airtel imeamua kujikita katika kuokoa maisha ya wateja wake na Watanzania kwa ujuma.Alisema Airtel itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi usalama barabarani kuhakikisha lengo la kupunguza ajali linafanikiwa.
Posted: 08 Sep 2013 09:49 PM PDT

CHAMA cha walemavu wa ngozi (Albino) nchini kwa kushirikiana na madaktari kutoka Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili wanatarajia kufanya ukaguzi wa afya kwa jamii ya walemavu wa ngozi mkoani Tanga katika wilaya tatu za Muheza, Lushoto na Korogwe.Kazi hiyo inatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 22,23 na 24 mwaka huu katika wilaya hizo
Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Ernest Kimaya alisema hayo wakati wa kikao cha kujadili changamoto zinazowakabili jamii hiyo katika upatikanaji wa huduma za afya kilichowahusisha wadau wa sekta ya afya elimu na huduma nyingine muhimu za kijamii mkoani Tanga. 

Kimaya alisema kazi hiyo ambayo wanaamini itawasaidia walemavu wa ngozi kutambua hali ya afya zao haitakuwa endelevu kutokana na ufinyu wa bajeti. "Tungetamani sana kampeni hii iwe endelevu lakini kutokana na ufinyu wa bajeti itabidi ifanyike katika wilaya chache tu ila tunaomba wafadhili waendelee kujitokeza ili tufikie watu wengi zaidi," alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo kutokana na hali hiyo aliiomba Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuanzisha kliniki za matibabu ya ngozi katika hospitali na vituo vya afya nchini kwa ajili ukaguzi wa afya walemavu wa ngozi ili walioathirika na ugonjwa wa saratani ya ngozi waweze kujitambua mapema. "Unajua tukienda hospitalini watu wanaishia kupewa dawa za kuzuia mionzi ya jua tu lakini kumbe mwingine tayari ameathirika na saratani tunaomba kuwe na utaratibu maalum kwa ajili ya walemavu wa ngozi katika vituo vyote vya afya na hospitali za hapa nchini," alisisitiza Kimaya.

Kuhusu changamoto za ukosefu wa huduma muhimu zinazokosekana kwa walemavu wa ngozi, Ofisa Ustawi wa Jamii Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga, Eveline Hijja ameziagiza taasisi za afya za Serikali kuwapa kipaumbele walemavu wa ngozi mara wanapofika katika hospitali na vituo vya afya ili kuepuka dhana ya unyanyapaa iliyojengeka miongoni mwa jami
Posted: 08 Sep 2013 09:52 PM PDT


 UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Korogwe, umewataka watendaji wa halmashauri kuweka utaratibu utakaowezesha vijana kupatiwa mikopo itakayotokana na fedha zilizotengwa na Serikali kiasi cha shilingi bilioni 6.1.


Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Korogwe, Bendera Shekigenda alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa siku moja kwa Saccos ya vijana wa Korogwe vijijini ulioandaliwa kwa ajili ya kuwapatia mbinu vijana namna watakavyojiandaa na mikopo hiyo.

Mkutano huo uliohusisha vikundi 169 vya vijana wanaounda Saccos hiyo ambapo Shekigenda alisema ili waweze kunufaika na mikopo hiyo vijana wanatakiwa kuwa wabunifu wa miradi wakijitahidi kutumia rasilimali walizonazo na zilizowazunguka katika kuendesha miradi ya kujikwamua kiuchumi.

Alisema kwamba upatikanaji wa fedha hizo kama sehemu ya mikopo kwao kutoka kwa Serikali yao inahitaji ubunifu wa hali ya juu kuwawezesha kujikwamua kimaisha ambapo aliwasisitiza kuongeza ubunifu badala ya kufanya biashara zitakazofanana utaratibu ambao unaweza kuwakwamisha.

Mbali na kuyasema hayo, Shekigenda pia aliwashauri maofisa wa vijana kuwafikia vijana wote katika maeneo ya vijijini kuwaeleza juu ya fursa iliyopo lengo likiwa kuwawezesha kushiriki katika mchakato wa kujiunga na Saccos yao lengo likiwa kuwakwamua katika lindi la umaskini wa kipato kwa walio wengi.

Mwenyekiti huyo alisema utolewaji wa mikopo hiyo unawahusisha vijana wote bila ya kujali dini, itikadi za vyama vya siasa wala ukabila ambapo aliwahimiza wajumbe wa mkutano huo kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ambao hawakuweza kupata taarifa ili waweze kuungana nao.

Kuhusu vikwazo ambavyo vitajitokeza wakati wa mchakato wa upatikanaji wa mikopo, Shekigenda alisema kwamba ni vyema vijana watakaojihisi kukwama kutokana na kujitokeza kwa upungufu mbalimbali wakajitahidi kuonana na viongozi wao wakiwemo wale wa vijana ili kupatiwa ufumbuzi.
Katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga zaidi ya vijana 260 walihudhuria kutoka katika kata 12 ambapo walishiriki kuchangia rasimu ya katiba ya Saccos yao huku wakihimizwa kuwa kwenye vikundi vya watu kuanzia idadi ya watano hadi kumi

No comments:

Post a Comment