TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, September 11, 2013

'SERIKALI IELEZE ZILIPO FEDHA ZA DECI'

Posted: 11 Sep 2013 03:22 AM PDT
  •  MWALIMU ALIYEMBAKA MWANAFUNZI 'MTEGONI'
  • MAHAKAMA YAMPELEKA GEREZANI MIAKA 30

 Na Nickson Mahundi, Ludewa



MAHAKAMA ya Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe, imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani na kuchapwa viboko 30 mwalimu wa Shuile ya Msingi Ingwachanya.



Mwalimu huyo, Bw. Romanus Msango, mkazi wa Lupembe, wilayani Njombe, alitiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) na kumuumiza vibaya sehemu za siri.



Akisoma hukumu hiyo Septemba 6 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ludewa, Bw.



Fredrick Lukuna, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao haukuwa na shaka yoyote.



Alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 1309(1) na 31(1) cha kanuni ya adhabu ya mwaka 2002 hivyo adhabu hiyo ni fundisho kwa wengine.



"Natoa adhabu hii ili kukomesha vitendo hivi kwenye jamii



kwani vinaleta madhara makubwa kwa watoto na wanawake pamoja na kusababisha magonjwa ya kuambukiza," alisema.



Awali ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka, Edison Kasekwa kuwa, mshtakiwa alitenda ukatili huo wa kinyama Agosti 20,2012 katika Kijiji cha Masimbwe, Kata ya Mlangali.



Alisema kabla mshtakiwa hajatenda kosa hilo, alimshambulia mwanafunzi huyo, kumbaka na kumlawiti jambo ambalo lilimsababishia maumivu makali.



"Serikali ilimpa mshtakiwa dhamana kubwa ya kulea watoto ambao ni nguvukazi ya Taifa la kesho lakini amewageuka na kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yake, kuidharirisha taaluma hivyo naomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundisho kwa walimu wengine," alisema.



Bw. Kasekwa aliongeza kuwa, mshtakiwa alikusudia kutenda makosa hayo kwa sababu alimfuata mwanafunzi huyo shambani wakati akivuna mahindi na wenzake ambao walikimbia kwenda kijijini kutoa taarifa baada ya mshtakiwa kumkamata mwenzao na kumpeleka kichakani.



Wa k a t i h u o h u o , wa t u wawili Bahati Mtega na Flowin Mtweve, wote wakazi wa Milo, wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na kuchapwa viboko 12 kila mmoja kwa kosa la kumbaka mke wa mtu na kumsababishia maumivu makali
Posted: 11 Sep 2013 03:21 AM PDT

THE HAGUE, Uholanzi

MAKAMUwa Raisnch ini Kenya, Bw.Wi lliamRuto, ameka nam asht akayakufanyauhal ifudhidi yabina damuk atikaM ahakama yaKimataifayaUh alifu(ICC) ,iliyop oMjini TheHag ue, Uholan zi.Bw. Ru tonaRais wa nchihiyo, Bw.U huruKenyatta,wa nat uhumiwakusha bikiag hasi abaada yaUch aguziMkuu mwaka2007.



K wamuji bu waShirika la Utangazaji nchini Uingere za (BBC ), Bw . Rutoanakuwa Ofi sawakwanzaambayeyuposerikalin i kushtakiwaka tika mahakamah iyoyak imataifa.Mashtaka dhid i y aviongozihao yanaonekana ni jar ibiokubwa kwaICC kuendesha mashtaka dhidi yavion gozi wa sia sa.



Bw. Rutoalik uwa akitabasam uw akatiwote katikachum bachamahakaman akukan ushamashtakay oteya mauaji, utesaji na kulazimisha kuhamish awat u.



Mwend eshaM ashtakaMkuuwamahakama hiyo, Bi.Fato uBensoud a, alise ma "Bw. Rutoalikuwamwanasi asa mwenyeng uvu amba yealipanga uhalifuilikukinaish akiuyakeya madar aka,"lili daiShir ikala Habari laAFP.



"Nivigum ukufi kirijins iw anaume, wanawake nawa totowali vyop atatabuauhof uyaku chomwa mo towan galihai,kuc hara ng wam pa kakufa aukuf ukuzwakutoka kwenye makazi yao," aliongeza Bi.Bensou da.



Watu1,2 00wa liuawanaweng ine60 0,000kujeruhi wakat ikakipindi cho te chagha siabaada yakut angazwamatokeo yaliyokuwa yakipingwa ka tikauchaguz i huo.



Zaid i yara ia 40,000nchinihu mo wanad aiwakuishikatik amakambi kutokan anav uruguhizo. Hivik aribuni Rais Kenya ttaaliahidi kuwaond katik akambihizoi fakapoSe ptemba20, 2013
Posted: 11 Sep 2013 03:16 AM PDT
  • ZMA YATOA TAMKO ZITO,YAKIRI KUISAJILI

 Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), Bw. Abeid Omar Maalim, amesema Zanzibar haipaswi kulaumiwa kutokana na tukio la kukamatwa kwa meli ambayo ilibeba shehena ya bangi nchini Italia.



Bw. Maalim aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar katika kumbukumbu ya kutimiza miaka miwili tangu kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander.
Alisema meli hiyo ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Gold
Star, iliyopo kwenye Visiwa vya Marshal, Amerika ya Kusini ilisajiliwa Zanzibar mwaka 2011 ambapo usajili huo hauna maana kuwa Zanzibar inahusika na tukio hilo.
"Kweli meli hii ilisajiliwa Zanzibar, jambo la msingi ni kuangalia bangi iliyokamatwa ilipakiwa wapi na nani anahusika na biashara hiyo," alisema Bw. Maalim.
Aliongeza kuwa, kama itabainika mmiliki wa meli hiyo anahusika moja kwa moja na usafirishaji huo, ZMA haitasita kuchukua hatua za kufuta usajili na kuangalia sheria nyingine.
"Kwa mujibu wa sheria za usajili wa meli, kuna kipengele ambacho mmiliki anajifunga kwa kusema meli yake haitasafirisha biashara haramu ikiwemo ya dawa za kulevya, ikibainika kafanya hivyo meli yake itafutiwa usajili," alisema.
Posted: 10 Sep 2013 11:16 PM PDT

Na Mariam Mziwanda

JUKWAA la Katiba nchini,linatarajia kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili kupeleka mapendekezo ya kufutwa maamuzi yaliyofanywa na Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013.



Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Bw. Deus Kibamba,aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano ulioshirikisha wadau na wataalamu 200 kutoka ndani na nje ya nchi. Mkutano huo ulikua  ukijadili mwelekeo wa  maandalizi ya Katiba Mpya na kuongeza kuwa,wabunge hawakutumwa na wananchi kufanya maamuzi hayo.

Alisema lengo la kumwona Rais Kikwete ni kumtaka asitishe hatua za wabunge na wanasiasa kutokufanya kazi isiyowahusu ili kuepusha vurugu na malumbano ndani ya Bunge.

“Mwelekeo uliopo utasababisha wananchi wakose Katiba waitakayo,kutokamilika kwa wakana Uchaguzi Mkuu 2015 kufanyika bila katiba mpya hali ambayo itazua mgogoro.”Ni hatari kuingia katika uchaguzi tukiwa na Katiba ya zamani….hali hii itasababisha Tume ya Mabadiliko ya Katiba iongezewe muda jambo ambalo wananchi hawapo tayari,hivyo ni muhimu Rais Kikwete aliangalie,”alisema.

Aliongeza kuwa mchakato huo kwa sasa upo njia panda kwani hakuna mwananchi aliyemtuma mbunge kuingilia kazi ya mchakato wa katiba,bali Bunge limesahau kuwa kazi yao ni kutunga sheria ya mabadiliko ya katiba na kusimamia bajeti ili wananchi kushiriki na kufanya maamuzi juu ya Katiba waitakayo.

Alisema kupitia kikao chao na Rais Kikwete ,watapendekeza wabunge kabisa kwenye mchakato huo kwani kuna watu waliochoshwa na maisha ya sasa. Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Palamagamba Kabudi,alisema watahakikisha maoni ya wananchi ambayo hayapo katika Rasimu ya Katiba,yanawasilishwa kwa Rais Kikwete na kusisitiza kuwa,upatikanaji wa katiba bora unawezekana.
Posted: 11 Sep 2013 01:01 AM PDT

 Na Eliasa Ally, Iringa
MAHABUSU waliofikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Iringa, jana waligoma kuteremka katika karandinga (gari), walilopanda kutoka gerezani ili kuishinikiza mahakama hiyo isikilize kesi zao, kuzitolea uamuzi kwani zimekaa muda mrefu bila kusikilizwa.



Walidai hali hiyo haiwatendei haki kwani wapo baadhi ya watu wanaokamatwa na kuachiwa muda mfupi lakini wao wanaendelea kusota gerezani bila sababu za msingi.Wakizungumza kwa makelele n d an i y a k ar an d in g a h ilo jana, mahabusu hao walisema hawatateremka kwani wengi wao kesi zao zimechukua muda mrefu bila kutolewa hukumu.
"Sisi tunataka haki itendeke, kitendo cha kesi zetu kuchukua zaidi ya miaka minne hadi mitano hakikubaliki, tunaomba kesi zetu zisikilizwe kwa haraka kama zilivyo kesi zingine."Huu ni uonevu wa hali ya juu, tunataka haki itendeke badala ya kuendelea kunyanyaswa na kuonewa kwa kubambikiwa kesi na watu wenye fedha," walilalamika mahabusu hao.
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo la mahakamani kwa sharti ya kutotajwa majina yao gazetini, walisema mahabusu hao wana madai ya msingi kwani kesi zao zinashindwa kusikilizwa wakiambiwa ushahidi haujakamilika."Tu n a z i omb a ma h a k ama zitende haki kwa kila mshtakiwa, tunashuhudia kesi nyingine zinasikilizwa katika muda mfupi, kwa nini kesi za mahabusu wengine zikwame," walisema.
Kamanda wa Polisi wa mkoani humo, Ramadhan Mungi, alikiri mahabusu hao kugoma kuteremka kwenye karandinga walilokuwa wamepanda kutoka magereza ya mkoa huo."Madai yao ni kesi zao kukaa muda mrefu bila kusikilizwa; hivyo kukaa muda mrefu mahabusu, wengine wanakamatwa na baada ya muda mfupi huachiwa," alisema.
Alisema kutokana na mgomo huo, alimtuma Mkuu wa Upelelezi mkoani humo kwenda kuwasikiliza mahabusu hao na kuzungumza nao ili kuwashawishi wateremke na kwenda kusikiliza kesi zao mahakamani
Posted: 11 Sep 2013 01:09 AM PDT

Na Charles Mwakipesile, Mbeya
SERIKALI imetangaza kufuta vibali vya wanaofanya kazi ya kuingiza kemikali nchini kwa ajili ya kudhibiti matumizi yake ikiwemo tindikali ambayo imekuwa ikitumika kwa ajili ya uhalifu na kutishia maisha ya Watanzania.



Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele alitangaza uamuzi huyo jana wakati akizungumza na Dawati la Mkoa la Ukatili wa Kijinsia katika ofisi ya Mganga Mkuu mkoani Mbeya.
Alisema kuwa, Serikali imekuwa ikipambana na uingizaji holela wa kemikali ambao ndiyo umekuwa chanzo cha kubadili matumizi ya kemikali ambazo zimekuwa zikitumika ovyo katika machimbo na wahalifu ambao wamekuwa wakitumia kwa ajili ya kuangamiza maisha ya Watanzania.
"Tatizo kubwa tulilolipata ni kutokana na waingizaji, wasafirishaji, watumiaji kubadili matumizi ya kemikali na kuishia kuzifanya ni sehemu ya silaha za kuangamiza Watanzania, hali ambayo sisi kama wadhibiti hatuwezi kukubali iendelee, sasa tumefuta vibali vyote na wanaotaka wataomba upya ili tuweze kupata nafasi ya kuwabaini wanaopotosha matumizi," alisema.
Hata hivyo, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Agnes Buto alisema kuwa ujio wa Mkemia Mkuu unatoa majibu ya maswali mengi waliyokuwa nayo kuhusiana na utendaji wa ofisi hiyo ambayo imekuwa ni muhimu sana kwa kazi zao wakati wote.
Posted: 11 Sep 2013 01:06 AM PDT

Na Suleiman Abeid, Kahama

CHAMAChaMapinduz i(CCM), k imewatakawawekeza ji wa naowekezak atika sektambalimbali nchini,w aoneum uh imuwakushirikiana na wananchi kwenye maene oyauwe kez aji.KatibuMk uuwachamahichoTaif a, Bw. Abdulrahm anKin ana, aliyasem a hayo janawakatiakihutubia wananchi kwenyeKa tay aMwen dak ulima alipokuwaakikaguamaende leoy au jenziwaKituochaAfya kin achojengwakw a msaada wa Mgodi wa Dha habuwaBuzwagi Go ldMine.



A lisema ha kun asababuya waweke zaji kuishim aisha yakujitenganak uwatak awaachekuchangia fedhanying ikati kah arambeemb alimb aliza kitaifab adalayakefe dhahiz oziwekezw ekatikaviji jiv ilivyop ojirani namaeneow aliyow eke zailikuc hocheamaend eleo.A lionge z akuwanimu hi muwawek ezajikuwa nauhus ianoyakaribunaw an anchi wanaozung uka ma eneowa u wek ezaji b ada layakujenga uhusianohuonaviongo zi wakitaifa.
" Kamawaw ekezaji watashirikiana vizuri na wananchi, mig ogoroinayo jitokez aba inayapandehizi itapung ua,naushu kurumgodihu ukwa ku kubali kujengaKituo chaAf ya, kitawasaidia wananchi wanaozu ngukam aen eohaya.
"M s aadahuuu tas aidiakujengauhusianomzur ikati yaonawana nch iwaMwe ndakulim a, wawek ezajiw otenchini wanap aswakubadil iuta rat ibuwakuchangia fedha nyingiwana pokuwaD aresSa laam , DodomaauMwanzambeleyavion gozi wa kitaifa.
" Misaada i tolewe ka tikamaeneow aliyowekeza kwa asil imia10naa sil imia10iliyo baki,wa nawezakuitoa njeya en eo lao lauwe kez aji,"alisem aBw. Kin ana.
Katika hatua nyingine, Bw. Kinana aliwaahidi wakazi wa Kijiji cha Kishima kuwa atayafanyia kazi malalamiko yao ya kutokulipwa fidia na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) baada ya mashamba yao kuharibiwa ili kupisha upitishaji nguzo za umeme na kupatiwa huduma hiyo ambayo wameiomba muda mrefu bila mafanikio.
"Mnahaki ya kulipwa fidia, fanyeni subira niweze kuwasiliana na Waziri wa Nishati na Madini ili taratibu za kulipwa fidia ziweze kufanyika...pia ombi lenu la kupatiwa umeme litafanyiwa kazi," alisema.

Kwa upande wake, Meneja wa mradi huo kutoka mgodi wa Buzwagi, Bw. Richard Ojendo, alisema gharama zilizotumika katika mradi huo awamu ya kwanza ni sh milioni 530 ambapo gharama zilizobaki ni sh. milioni 470.

Posted: 11 Sep 2013 01:31 AM PDT

Na Mwandishi Maalumu

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali itahakikisha kuwa ardhi ambayo Watanzania wamepewa na Mungu haibadiliki na kuwa chanzo cha upotevu wa amani nchini.Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Kimataifa wa siku tatu unaojadili haki na amani katika masuala ya ardhi Tanzania.



"Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa ardhi yetu haileti laana, bali inabakia kuwa baraka ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia. Ninawasihi wale wote wenye mamlaka na utoaji wa ardhi wahakikishe kuwa wanatimiza wajibu wao wanaposimamia masuala ya ardhi ili haki isipotee na hatimaye kuepusha migogoro ya ardhi.



"Ninawasihi Watanzania iwe ni wanasiasa, viongozi wa dini, asasi za kiraia, wasomi na umma wote kwa ujumla. Ninaomba tuitunze amani tuliyonayo na tutambue kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee tuliyojaliwa kuwa nayo. Madhara ya ukosefu wa amani ni makubwa, tuangalie nchi za wenzetu zenye migogoro na tuone jinsi machafuko hayo yatatuathiri sisi wenyewe, watoto wetu na wajukuu wetu," alisisitiza Waziri Mkuu.



Alisema, anatambua hofu ambayo imewakumba watu wengi kuhusiana na uwekezaji iwe ni kwenye kilimo ama madini."Ninatambua kwamba kuna hofu kubwa imejengeka miongoni mwa wananchi wengi hasa wanaposikia suala la uwekezaji hasa kwenye kilimo," alisema. Alisema, tangu wakati wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa madarakani, alishasema kuwa ardhi ni rasilimali ya watu wote.



"Aliweka mifumo ambayo hairuhusu mtu kumiliki ardhi ambayo haina ukomo, kuna ukomo wa miaka kati ya 33 na 99. Na pia kuliwekwa masharti kuwa ni lazima ukipata ardhi uiendeleze, usipoiendeleza, unanyang'anywa," aliongeza.



Alisema, kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, imekataza mgeni (mtu ambaye si raia wa Tanzania) kumiliki ardhi hapa nchini." A r d h i i n a t o l e w a k w a wawekezaji, chini ya sheria ya uwekezaji kwa muda maalumu. Mwekezaji akimaliza muda wake, anatuachia ardhi yetu na ndiyo maana Serikali ya Kijiji hairuhusiwi kutoa ardhi zaidi ya ekari 50," alisema.



Alisema, chini ya sheria ya ardhi na sheria ya uwekezaji, hapa nchini kuna wawekezaji wakubwa 122 ambao ni wa ndani na wa nje na kwa ujumla wao wanamiliki kilomita za mraba 1,296 kati ya kilomita za mraba 945,087 ambazo ni ukubwa wa nchi nzima.



Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe 200 wakiwemo Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wa dini, washiriki kutoka nchi za Ujerumani, Sweden, Burma, Finland, Norway na Afrika Kusin


Posted: 11 Sep 2013 01:33 AM PDT

 Na Rehema Maigala

MBUNGE wa Ubungo, J o h n Mn y i k a , amemtaka Gavana wa Benki Kuu (BoT), Benno Ndulu, kuwaeleza Wa t a n z a n i a , h u s u s a n waliokuwa wanachama wa Kampuni ya Development En t e r p r e n e u r s h i p f o r Community Initiative (DECI) fedha zao zipo kwenye akaunti gani.



Mnyika amesema kuwa wakati sakata la DECI linaanza mwaka 2009, Serikali ilizuia akaunti ya DECI iliyokuwa na sh.bilioni 19, sawa na asilimia 40 ya fedha zote ambazo ni za wanachama wa taasisi hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara juzi, Kata ya Kimara, Mtaa wa Mavurunza, baada ya kuulizwa swali na mmoja wa wananchi aliyetaka kujua hatima ya fedha zao, Mnyika alitoa tahadhari kuwa dana dana inayotaka kufanywa na Serikali kuwalipa watu hao kiasi cha sh.bilioni 19, inaweza kutia shaka kuwa fedha hizo hazipo.

"Sasa naomba nimjibu yule mwananchi aliyetaka kujua hatima ya fedha za DECI...mtakumbuka hili suala nimekuwa nikitaka majibu yake bungeni, lakini kila mara wanatumia kisingizio kuwa suala hili liko mahakamani. Juzi baada ya hukumu kutoka tumemsikia Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, akisema hawawezi kuwalipa wananchi walioweka fedha zao DECI.

"Wanasema waliocheza DECI nao ni watuhumiwa, walipaswa kuhukumiwa, lakini Gavana hakusema hizo fedha sh.bilioni 19 sawa na asilimia 40, ambazo Serikali ilizitaifisha na kuwekwa BoT, ziko kwenye akaunti gani, tunataka atuambie, maana kwa hali inavyoanza isijekuwa fedha hizo walizitumia kwenye uchaguzi mkuu wa 2010.

Mbunge huyo alisema kuwa wananchi waliopanda fedha zao wana haki ya kulipwa kwa sababu zipo zikishikiliwa kwenye akaunti na Serikali. Zinapaswa kurejeshwa kwa msingi kwamba pamoja na mahakama kuwahukumu waendeshaji wa DECI kuwa ni wahalifu, haikuwahukumu washiriki.

Aliongeza kuwa DECI ilisajiliwa na Serikali na viongozi wa Serikali, akiwemo Waziri wa Fedha na Uchumi wa wakati huo, Mustafa Mkulo, walihamasisha watu kujiunga. Serikali iliachia kuendeshwa na kuzilinda ofisi za kampuni hiyo maeneo ya Mabibo, ambapo ni jimboni kwa mbunge huyo.  
Posted: 11 Sep 2013 01:35 AM PDT

 Na Rachel Balama

MAHAKAMA y a Rufaa Tanzania leo itaanza kusikiliza rufaa ya kesi ya Naibu Waziri wa zamani wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Maua Daftari, dhidi ya mfanyabiashara Fatuma Salimini Said.



Dkt. Daftari ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM, alikata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwamuru kumlipa mfanyabiashara huyo sh. milioni 100.7.

Rufaa hiyo imepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, linaloongozwa na Jaji Januari Msoffe, akisaidiana na Jaji Dkt. Steven Bwana na Jaji Sauda Mjasiri.

Rufaa hiyo inatarajiwa kusikilizwa leo chini ya jopo jipya la majaji watatu wa Mahakama hiyo ambapo wakili wa mkata rufaa (Dkt. Daftari) atawasilisha hoja zake za kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, kabla ya mawakili wa mjibu rufaa kujibu hoja hizo.

Awali rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa Juni 12, 2013 na jopo la majaji watatu lililoongozwa na Jaji Nathali Kimaro, akisaidiana na Jaji Salum Massati na Jaji William Mandia, lakini ilikwama kusikilizwa baada ya Jaji Kimaro kujiondoa.

Jaji Kimaro alitangaza kujitoa katika rufaa hiyo baada ya kubaini kuwa alishawahi kuisikiliza kesi ya msingi mwaka 2011, akiwa Mahakama Kuu.

Katika kesi ya msingi, mlalamikaji Fatuma Salimin Said, alikuwa akimlalamikia Dkt. Daftari kumtapeli fedha taslimu pamoja na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 200.

Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, Fatma alikuwa akimdai Dkt. Daftari sh. milioni 100,092,400 alizompa ili amnunulie vifaa mbalimbali kati ya mwaka 1994 na 1997, lakini mlalamikiwa hakufanya hivyo
Posted: 10 Sep 2013 10:53 PM PDT

Na Mwandishi Wetu
 Hali ya usalama katika kambi ya wakimbizi Ndutta,si nzuri kutokana na ongezeko la vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na majambazi wanaofanya vitendo vya uhalifu nchunina wenzao kutoka nchi jirani ya Burundi. Kutokana na hali hiyo,Serikali ya Burundi imeitaka Serikali ya Tanzania kuendelea na msimamo wa kubadili matumizi ya ardhi katika kambi hiyo iliyopo wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.



Akizingumza na Majira katika mahojiano maalum, Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Venance Mwamotto,alisema Serikali ya Burundi imefurahishwa na msimahuo kwani majambaziwaliokuwa wakifanya uhalifu nchini kwao,walikuwa wakijificha eneo hilo.
“Kambi ya Nduta ipo mpakani mwa Tanzania na Burundi,baada ya wakimbizi waliokuwa wakiishi katika kambi hiyo kuondolewa, Serikali iliamua kugawa ardhi kwa vijana ili kuwa na kijiji cha mfano katika swala la kilimo.” alisema. Alisema awali Serikali ilitoa eneo hilo kwa vijana amabao badala ya kuayatumia kwa kilimo cha mazao ambayo yanayokubalika wao waliyatumia kwa kilimocha bangi,kuharibu mazingira na wengine kuchoma miti ili kupata mkaa na kuuza.
“Ni hali ya kusikitisha,tumeweza kubaini tatizo hili katika operesheni maalumtuliyoifanya katika eneo hili na kukamata kilo 1,500 za bangi” alisema Bw. Mwamottto. Alisema uamuzi wa kubadili matumizi ya ardhi hiyo ulifanywa na madiwani wa halmashauri hiyo na katika kikao cha maendeleo wilayani humo ambapo kilibariki azimio hilo. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na mbunge wa Muhambwe,Felix Mkosamali
Aliongeza kuwa jambo la kushangaza Bw. Mkosamali watendaji wenzake na kuamua kufungua kesi mahakamani na kudai vijana wameny’ang’anywa ardhi. Bw. Mwamotto alisema kutokana na uhalifu uliokuwa ukifanyika eneo hilo umekuwa ulisababisha hofu kwa wananchi..

Alisema hivi sasa ,uongozi wa Wilaya hiyo na Jeshi la Polisi,umetangaza operesheni ya usalimishaji silaha,utoaji taarifa za siri kwa watu wanaojihusihsa na matukio ya uhalifu
Posted: 10 Sep 2013 08:51 PM PDT
  •  HATIMA YA WALIOPANDA  FEDHA SAS NJIA PANDA
  • DPP AKATA RUFAA,APINGA AMRI YA MAHAKAMA

 Na Rachel Balama

MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), amewasilisha kusudio la kukata rufaa hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam dhidi ya vigogo wa Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI).



Kampuni hiyo ilikuwa ikiendesha na kusimamia mchezo wa upatu ambapo taarifa ya kusudio la kukata rufaa, iliwasilishwa katika mahakama hiyo Agosti 23 mwaka huu.

Pamoja na mambo mengine, katika kusudio hilo DPP anapinga amri iliyotolewa na mahakama hiyo kuitaka Serikali pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ifanye utaratibu wa kurudisha fedha zilizopandwa na wanachama wa kampuni hiyo.

Wanachama hao ni wale watakaoonesha uthibitisho wa kupanda fedha zao DECI ambapo DPP anataka mahakama itamke wazi na kutoa maelekezi ni nani anayestahili kurejesha fedha hizo kwa wanachama hao.

Katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Agosti 19 mwaka huu, mahakama iliwahukumu vigogo wanne kati ya watano kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh. milioni 21 kila mmoja.

Hukumu hiyo ilisomwa na Hakimu Aloyce Katemana kwa niaba ya Hakimu Stuwart Sanga aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo na kudai kuwa, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili washtakiwa na kuwatia hatiani.

Hakimu Katemana alisema, pamoja na hukumu hiyo Serikali ifanye mchanganuo wa mali za DECI ambazo inazishikilia kwa kuwa zipo mali ambazo zinashikiliwa lakini ni za watu wengine.

Washtakiwa waliotiwa hatiani katika kesi hiyo ni Jackson Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo Ole Loitignye na Samwel Sifael Mtares ambapo mshtakiwa Arbogast Kapilimba aliachiwa huru baada ya mahakama kushindwa kumtia hatiani.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanakabiliwa na

mashtaka mawili ambayo ni kuendesha na kusimamia mradi wa upatu kinyume na kifungu 111A(1,3) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16.

Ilidaiwa kuwa, kati ya mwaka 2007 na Machi 2009, katika Makao Makuu ya DECI, yaliyopo Mabibo Mwisho, Dar es Salaam, washtakiwa waliendesha na kusimamia mradi wa upatu katika sehemu tofauti nchini kwa ahadi ya kuwapa wanachama wake fedha zaidi.

Shtaka la pili ni kupokea amana za umma bila kuwa na leseni kinyume na kifungu cha 6(1,2) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha namba 5 ya mwaka 2006 na kwamba washtakiwa wote katika kipindi hicho, wakiwa kwenye Ofisi za DECI, walipokea amana kutoka kwa umma bila leseni.

DECI iliwanufaisha watu wengi hasa waliojiunga mwanzoni na badaye kuibuka malumbano kati yao, Serikali na wanachama waliopinga kusitishwa kwa shughuli za taasisi hiyo.

Kusimamishwa kwa shughuli za DECI, kulitokana na uamuzi wa BoT kutoa taarifa ya kuwahadharisha Watanzania waliojiunga na upatu huo kuwa taasisi hiyo haiko kisheria na wanaweza kupoteza fedha walizopanda.

Upandaji mbegu katika taasisi hiyo, ulisitishwa baada ya Serikali kusimamisha akaunti za taasisi hiyo hadi uchunguzi utakapokamilika na kusababisha uvunjifu wa amani kwa wanachama wa DECI na viongozi wa taasisi hiyo.

Baadhi ya wanachama waliamua kuchukua sheria mkononi kwa kuvunja vioo vya magari ya viongozi, wakitaka warejeshwe fedha zao.

Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri ulikuwa unawakilishwa na Wakili, Prosper Mwangamila na Justus Mulokozi, ambapo washtakiwa hao walikuwa wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Hudson Ndusyepo na Onesmo Kyauke.

Wakili wa DECI

Siku moja baada ya mahakama hiyo kutoa hukumu, Majiralilizungumza na Wakili wa washtakiwa Bw. Ndusyepo, ambaye alisema kuwa, mahakama hiyo imeshindwa kusimamia vizuri sheria iliyowatia hatiani wateja wake na kuwaacha wanachama.

Alisema yeye hapingani na hukumu iliyotolewa na mahakama lakini sheria ya adhabu kifungu cha 171 (A), kama ilivyorekebishwa na sheria namba 8 ya mwaka 2006, haikutekelezwa ipasavyo.

Bw. Ndusyepo alisema sheria hiyo pia inawatia hatiani wanachama wote waliopanda fedha zao DECI kwa kushiriki upatu, hivyo mahakama inapotoa amri kwa Serikali irudishe fedha za wanachama hao ni sawa na kuwazawadia wahalifu.

Aliongeza kuwa, kama sheria hiyo imetumika kuwatia hatiani wateja wake, haikupaswa kuwaacha wanachama ambao kwa mujibu wa sheria nao walipaswa kutiwa hatiani kwani kitendo cha kushiriki upatu kinakatazwa na sheria hiyo.

“Wanachama wa DECI nao ni wahalifu kwa mujibu wa sheria hii hivyo walipaswa kutiwa hatiani kwa kujihusisha na upatu ambao upo kinyume cha sheria.

“Haikuwa rahisi kuwakusanya wanachama wote na kuwaunganisha katika hati ya mashtaka moja ndio maana ilikuwa rahisi kuwashtaki Wakurugenzi kwa niaba ya wote,” alisema.

Aliongeza kuwa, amri iliyotolewa na mahakama hiyo kutaka wanachama wa DECI warudishiwe fedha zao inaondoa dhana ya Bunge kutunga sheria inayozuia mchezo wa upatu.

No comments:

Post a Comment