TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 13, 2016

PROF. MUHONGO:TUNATAKA TANESCO IJIENDESHE KIBIASHARA:

RA7
RA8
RA9
RA10

RA11
RA12
RA13
Serikali imesema matarajio yake ni kuona kuwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linajiendesha kibiashara kuhakikisha kuwa wazalishaji wanaliuzia shirika hilo umeme kwa bei ambayo haitawaumiza wananchi. Kauli hiyo imetolewa leo (Januari 11,) na Waziri wa Nishati na Madin, Profesa Sospeter Muhongo alipotembelea eneo la utafiti la Makaa ya Mawe Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe. Profesa Muhongo alieleza kuwa, endapo Tanesco itanunua umeme kwa bei ya juu kutoka kwa wauzaji inamaanisha kuwa itaendelea kuwauzia wananchi umeme wa bei ya juu ambapo pia Serikali italazimika kutoa ruzuku kwa shirika hilo ili lijiendeshe. “Tunatoka huko sasa. Hatutaki tena kuendelea kuwapa Tanesco ruzuku, tunataka shirika hili lijiendeshe kibiashara lakini pia hatutaki kuwaumiza wananchi.” Kauli ya Waziri Muhongo imekuja kufuatia kutokukubaliana kwa gharama za kuuziana umeme mara baada ya mradi wa Makaa ya Mawe ya Mchuchuma utakapoanza kuzalisha umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe, ambapo Kampuni ya Tanzania International Resource Limited ambayo ni mbia wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) katika mradi wa Makaa ya Mawe kupanga kuiuzia Tanesco umeme kwa bei ya kiasi cha senti za Marekeni 13 ambapo Tanesco wanataka kununua kwa nusu ya bei hiyo.Kufuatia hali hiyo Profesa Muhongo aliitaka kampuni hiyo ya NDC na TANESCO kukaa kikao chini ya Uenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo siku ya Jumatano, Januari 13, 2016 ili kujadiliana kuhusu suala hilo na kufahamu mustakabali wa uendelezaji wa mradi huo ambao utakapokamilika, unatarajiwa kuwezesha uzalishaji wa megawati 600 za umeme ambazo kati yake megawati 350 zitaingizwa katika Gridi ya Taifa. “Tunataka mradi uiuzie Tanesco umeme kwa bei rahisi lakini pia tufike mwisho wa majadiliano na mradi uanze haraka. Endapo hatutaafikiana katika hili tutafute mwekezaji mwingine,” alisema Profesa Muhongo. Akizungumzia kuhusu suala la fidia kwa wananchi waliopisha mradi huo, Profesa ameitaka kampuni hiyo kuharakisha suala la fidia na kuwaruhusu wakulima kutumia ardhi kwa shughuli za kilimo cha mazao ya muda mfupi wakati makubaliano kati ya Tanesco na kampuni yanaendelea. Naye Mbunge Mteule wa Jimbo la Ludewa Deo Ngalawa amemshukuru Profesa Muhongo kwa kufika kwake na kuendesha majadiliano kuhusu mradi huo na kuongeza kuwa, jitihada za Profesa Muhongo katika kuongeza kiwango cha umeme nchini zinaonekana na kwamba wananchi wa Ludewa wanausubiri mradi huo kwa kuwa ni ajira na fursa kwao. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Antony Choya amemuelezea Profesa Muhongo kuwa amekuwa ni zaidi ya Mwalimu katika kuwafahamisha kuhusu mradi huo na namna anavyosimamia masuala ya nishati na hususan kutafuta ufumbuzi juu ya mradi husika. “Nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa uteuzi wako kushika nafasi hii,” ameongeza Mkuu wa Wilaya. Kampuni hiyo inamiliki asilimia 80 ya hisa katika mradi huo ambapo NDC wanamiliki asilimia 20.

No comments:

Post a Comment