TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, January 13, 2016
WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA QATAR NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdallah Jassim al Maadadi ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na na balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdallah Jassim al Maadadi kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jasem Al Najem, ofisini kwake jijini Dar es salaam , Januari 13, 2016. (Pichana Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekuatana na kufanya mazungumzo na mabalozi wawili kutoka nchi za Qatar na Kuwait.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na mabalozi hao leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amewashukuru mabalozi hao kwa pongeza walizokuja kumpatia, pamoja na namna ambavyo nchi zao zimekua zikisaidia Tanzania, ambapo ameahidi kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na nchi zao.
Kwa upande wake, Balozi wa Qatar, Abdallah Jassim al Maadad amesema Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo yote ambayo Qatar imepiga hatua kubwa na inaweza kutoa msaada kwa Tanzania.
Amesema Quwait iko tayari kuwekeza nchini katika sekta ya kilimo, kwa vile ardhi ya Tanzania ni yenye rutuba na inafaa kwa shughuli za kilimo. Aidha, ametaja sekta nyingine ambazo wangependa kuwekeza ni pamoja na sekta ya uvuvi na viwanda.
Naye, Balozi wa Kuwait, Jasem Al Najem ambaye amekuja kujitambulisha kwa Waziri Mkuu, amesema nchi yake kupitia ‘Kuwait fund’ iko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Balozi Najem, pia ameshauri vituo vya uwekezaji vya Tanzania na Kuwait kufanya kazi kwa ushirikiano zaidi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment