TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 13, 2016

UCHUMI WA TANZANIA WAZIDI KUSHIKA KASI

dk1

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), kulia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, DkHaji Semboja na kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Utafiti toka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Hussein Kamote.
dk2
Mhadhiri mwandamizi wa uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, DkHaji Semboja (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wakitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
dk3
Mkurugenzi wa Sera na Utafiti toka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania Bw. Hussein Kamote akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya mchango wa viwanda katika kuongeza pato la taifa wakati wakitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
dk4
Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati akitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba).
dk5
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati akitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Eliphace Marwa – MAELEZO

……………………………………
Na. Frank Shija
Pato la Taifa katika kipindi cha Robo tatu ya mwaka 2015 limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.4 katika kipindi cha mwaka 2014.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.Dkt. Albina amesema kuwa kutokana na ongezeko hilo Serikali imeendelea kutoa huduma za kijamii zikiwemo umeme, afya na maji

“ Pato la Taifa kwa robo tatu ya mwaka 2015 limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ukilinganisha na asilimia 5.4 katika robo tatu ya mwaka 2014” Alisema Dkt. Albina.

Dkt. Albina ameongeza kuwa kuongezeka kwa Pato la Taifa kumeenda sanjari na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa na huduma nje ya nchi kwa takribani asilimia 3.3 ambapo bidhaa na huduma zilizochangia ongezeko hilo ni pamoja na dhahabu, Almasi, madini mengine na Utalii.

Aliongeza kuwa utangazwaji wa Takwimu za Pato la Taifa unazingatia matakwa ya Sheria ya Takwimu na 9 ya mwaka 2015 inayotoa mamlaka kwa Tume ya Taifa ya Takwimu kukusanya, kuchambua na kutangaza takwimu za Pato la Taifa.

Aidha alitaja baadhi ya shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi kubwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2015 kuwa ni pamoja na Ujenzi (17.6%), Uchukuzi na Uhifadhi (10.6%), Uendeshaji Serikali na Ulinzi (10.6%) na Uchimbaji Madini na Kokoto (8.0%).

Dkt. Albina amesema kuwa jumla ya thamani ya Pato la Taifa kwa bei za miaka husika katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba 2015 ni takribani shilingi tilioni 71.7 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 6.9.

No comments:

Post a Comment