TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, January 13, 2016
WAZIRI MKUU AMFARIJI MAMA MARIA NYERERE KUFUATIA KIFO CHA MKWEWE MH. LETICIA NYERERE
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitia saini kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mbunge wa zamani,Leticia mageni Nyerere wakati alipokwenda kumhani mjane wa Baba wa taifa, Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es salaam Januari 12, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa neno la faraja kwa Mjane wa baba wa taifa Mama Maria Nyerere (kulia) wakati alipokwenda nyumbani kwa Baba wa taifa, Msasani jijini Dar es salaam kuhani msiba wa Mbunge wa zamani Leticia Nyerere. Kushoto ni mkewe Mary.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (wapili kulia) wakiifariji familia ya Mjane wa Baba waTaifa, Mama Maria Nyerere (kulia) wakati walipokwenda nyumbani kwa Baba wa taifa Msasani jijini Dar es salaam kuhani msiba wa mbunge wa zamani, Leticia Nyerere, Januari 12, 2016. Kushoto ni mtoto wa baba wa Taifa, Rose Nyerere na wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakiagana na mjane wa Baba wa taifa, Mama Maria Nyerere wakati walipokwenda nyumbani kwa Baba wa taifa, Msasani jijini Dar es salaam Januari 12, 2016 kuhani msiba wa Mbunge wa zamani, Leticia Nyerere.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwa katika picha ya pamoja na Mjane wa baba wa taifa Mama Maria Nyerere (kushoto kwa Waziri Mkuu) baada ya kuhani msiba wa mbunge wa zamani, Leticia Nyerere, Msasani jijini Dar es slaam Januari 12, 2016. Picha na ofisi ya Waziri Mkuu.
WAZIRI MKUU,Kassim Majaliwa amemtembelea na kuampa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Maria Nyerere kwa kufiwa na mkwewe Leticia Nyerere.
Akizungumza na mama Maria alipomtembelea nyumbani kwake jana(Jumanne, Januari 12,2016), Msasani jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Mama Maria Nyerere pamoja na familia na kuwaomba waendelee kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondokewa na mpendwa wao.
“Kipindi hiki ni kigumu, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo, pia tutajumuika nanyi katika kipindi hichi chote, tuendelee kuwa watulivu na kumwomba Mungu” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Ndugu wa marehemu, John Shibuda (aliyewahi kuwa mbunge wa CHADEMA) ameeleza kutokea kwa msiba huo. Ambapo amesema “Desemba, 19 mwaka huu Leticia Nyerere alipelekwa nchini Marekani kwa matibabu na alifariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lanham, Maryland juzi saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Aidha, Shibuda amemshukuru Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa kwenda kuipa pole familia na Serikali kwa namna ambavyo inatoa ushirikiano mzuri kwa familia.
Naye, Rose Nyerere amesema familia inaendelea na maaandalizi, hivyo watatoa taarifa ya baada ya kuandaa utaratibu wa siku ambayo mwili utaletwa nchini, kuagwa na hatimaye kuzikwa Butiama.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ambaye amelazwa siku kadhaa zilizopita katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Majaliwa, amesema amefarijika baada ya kumuona Waziri Mkuu huyo mstaafu akiendelea vizuri na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa kumpatia matibabu na kumhudumia vizuri. Pamoja na kumpa pole, Waziri Mkuu amemwombea apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Naye, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa kumtembelea hospitalini hapo, pia ameipongeza Serikali kwa jitihada mbalimbali inazofanya ili kusaidia wananchi na hatimaye kuiletea nchi maendeleo.
“Naipongeza Serikali kwa namna ambavyo inaendelea kutekeleza majukumu yake katika masuala mbalimbali yenye lengo la kusaidia wananchi” alisema Sumaye.
Waziri Mkuu Majaliwa, pia amemtembelea na kumjulia hali Balozi Hassan kibelloh ambaye amelazwa na anaendelea kupatiwa matibabau katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment