TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 19, 2016

TANZIA- TAARIFA YA MSIBA DMV SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA FAMILIA YA SEBO KUTOKA KWA BALOZI LIBERATA MULAMULA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA YAFANYIKA KATIKA MAKABURI YA KISUTU LLEO Shule ya Chipu wajisaidia porini TECNO OWN THE STAGE EPISODE 10 MBUNGE WA JIMBO LA LINDI AENDELEA KUTIMIZA AHADI ZAKE JIMBONI KWAKE MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU LETICIA NYERERE JAPAN YASAINI MIKATABA YENYE THAMANI YA DOLA 204,300 KWA AJILI YA KUSAIDIA MAENDELEO YA JAMII TANZANIA Tusingempeleka shule asingesombwa na mafuriko-Mama HISTORIA FUPI YA HAYATI PADRI CALISTI NYAMBO ALIYEFARIKI NCHINI MAREKANI AKIFANYA SHUGHULI ZA UTUME UKISHIKWA SHIKAMANA BALOZI MLIMA AKUTANA NA KAIMU BALOZI WA CHINA WEMA SEPETU AWAFUNDA WABUNIFU WA MAVAZI CHIPUKIZI WATAKAOPAMBA LADY IN RED FASHION SHOW 2016 PAPASO WITH DIAMOND PLUTNUMZ PART THREE PAPASO WITH DIAMOND PLATNUMZ PART TWO PAPASO WITH DIAMOND PLUTNUMZ PART ONE WAZIRI SIMBACHAWENE ASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI KATAVI NA KIGOMA Kichupa cha leo John rodgers_MAMA [Official video] LONGA NA VIJIMAMBOBLOG NA DR CRISPIN SEMAKULA PART ONE AND TWO TANZIA: GEORGE SEBO MWENYEKITI WA CCM DMV HATUNAE TENA BREAKING NEWS: WANANCHI WA BONDE LA MKWAJUNI WAFUNGA BARABARA NA KUFANYA FUJO Machungu rungu la Magufuli yaanza.

Nimepokea taarifa ya msiba wa Mzee George Sebo kwa mstuko na huzuni kubwa. Naomba kuwapa pole wana jumuiya wote na wanachama wa CCM DMV kwa msiba huo mkubwa sana. Naomba munifikishie salaaam zangu za rambirambi kwa mkewe Mama Grace Sebo na wanafamilia. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake ya upendo mahali pema peponi. Bwana ametoa, Bwana amechukua, jina lake lihidimiwe.


==============================================
Mwili ukiwasili katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi. 
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman kabla ya mazishi yake.
Mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman uwasili katika makaburi ya Kisutu leo.
Mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman ukihifadhiwa katika nyumba yake ya milele. 
Mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman ukihifadhiwa katika nyumba yake ya milele.
Waombolezaji.
Baadhi ya waombolezaji wakiweka udongo katika kaburi la marehemu. 
Baadhi ya waombolezaji wakiweka udongo katika kaburi la marehemu.
Wadau wa michezo wakibadilishana mawazo. Kutoka kushoto ni Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva, Msemaji wa Simba, Haji Manara, Muhidin Issa Michuzi na Mpoki Bukuku wakibadilishana mawazo wakazi wa mazishi ya aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman. (Picha na Francis Dande)

DAR ES SALAAM, TANZANIA

SIMANZI, majonzi na vilio vimetawala nyumbani kwa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman aliyefariki dunia leo wakati akiogelea katika bahari ya hindi.

Suleiman alifariki dunia asubuhi akiwa njiani akipelekwa katika hospitali ya Aga Khan mara baada ya misuli kukaza ghafla alipokuwa akiogelea.

Ofisa Uhusiano wa TAA, Ramadhan Maleta alisema marehemu huwa anautaratibu wa kufanya mazoezi ya kuogelea kila siku asubuhi kutoka feri hadi Kigamboni.

Alisema leo asubuhi kama kawaida yake alikwenda Feri kwa ajili ya kuogelea saa 12.00 ambapo aliogelea hadi Kigamboni na alipokuwa anarudi alipata tatizo la kukaza kwa misuli na kuishiwa nguvu.

Maleta alisema mwenzake aliyekuwa anaogelea nae alimuona na kujaribu kumuokoa na kuomba msaada kutoka boti za wavuvi ambao walifika na kumpeleka nchi kavu na kumpa huduma ya kwanza, ambapo alikuwa akiwa njiani kupelekwa hospitali.

Alisema TAA imepata pigo kubwa kwa kupotea kiongozi mahiri ambaye alikuwa hana majigambo wala hakuweka matabaka baina na wafanyakazi na alishirikiana na wote bila kujali nyadhifa zao.

Alisema marehemu alikuwa miongoni mwa viongozi waanzilishi wa kwanza wa TAA mwaka 1999 na atakumbukwa kwa mchango mkubwa alioutoa na usimamizi wa ujenzi wa viwanja vya ndege vya Songwe na Mpanda.

Pia ujenzi wa awamu ya tatu ta Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julkias Nyerere (JNIA) na viwanja vingine vya ndege vinavyoendelea na ujenzi katika mikoa mbalimbali nchini.

Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo waliofika nyumbani kwa marehemu walisikika wakilia huku wakisema kuwa TAA wameacha yatima na kwamba pengo la Suleimani ni kubwa kwao na kwa taifa.

Kaka wa marehemu, Farid Karamma alisema Suleima atakumbukwa kwa ukarimu wake na alikuwa mtu wa kupenda watu na asiyependa migogoro.

Alisema marehemu ameacha mke mmoja na watoto watatu wa kiume ambao ni Mohammed, Said na Husam Suleima anayesoma katika shule ya sekondari Mzizima Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu uliwasili nyumbani kwake Upanda saa 7.25 mchana ukiwa katika gari la kubebea wagonjwa la msikiti wa Maamur ambapo saa 9.21 ulichukuliwa na kupelekwa msikitini hapo tena kwa ajili ya kuswaliwa, na kisha kwenda kuzikwa katika makabiri ya Kisutu.
=======================================================
By Mussa Mwangoka, Mwananchi

Sumbawanga. Wanafunzi 1,045 wa Shule ya Msingi Chipu, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa na walimu wao wanajisaidia porini kwa mwaka mmoja baada ya vyoo kufurika vinyesi.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Arord Mkwama, mwishoni mwa wiki iliyopita alisema ametoa taarifa za tatizo hilo katika ofisi ya mkurugenzi kwa muda mrefu.

Mwalimu Mkwamba ambaye pia ni Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Chipu, alisema amekuwa akisubiri fedha kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo vya shule na katika nyumba mbili za walimu.

“Shule hii inakabiliwa na changamoto kadhaa lakini kubwa ni kukosa vyoo, pia walimu wanakabiliwa na changamoto.

“Kati ya nyumba tisa za walimu, mbili hazina vyoo kwa kipindi kirefu sasa na mbili nyingine vyoo vyake vimejaa na havifai kwa matumizi ya binadamu,” alisema Mwalimu Mkwama.

Mkazi wa kijiji hicho, Sunday Kuboja, alisema kwa ushirikiano na wazazi wenzake wamekubaliana kuwa baada ya wiki moja kama Manispaa ya Sumbawanga haitatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo watawakataza watoto wao kwenda shule hadi vitakapojengwa.

“Kadhia ya wanafunzi na walimu wa shule hii ni kukosa pahala pa staha pa kujisaidia. Mwaka 2013 wazazi tulilazimika ‘kutapisha vyoo’ vya shuleni hapo kwa kuwa vilikuwa vimejaa, lakini sasa vimefurika tena na wanafunzi hawawezi kuvitumia kwa sababu vimetapakaa kinyesi sakafuni,” alisema Kuboja.

Mkazi mwingine, Filbeth Ntinda alisema watoto wao wanalazimika kutoroka shuleni na kurudi kujisaidia nyumbani.

Naye Lucia Sawe, alisema kijiji hicho kiko katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kikiwamo kipindupindu.

Wanafunzi Edward Ntalasha na Maria Mbokosi wa darasa la saba, walisema wanafunzi wa shule ya awali wanakanyaga vinyesi na mikojo wanapokwenda kujisadia chooni kwa kuwa hawaelewi lolote kutokana na umri wao kuwa mdogo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Deus Masanja alisema waliwahimiza wananchi kufyatua tofali zaidi ya 35,000 na kuchimba mashimo kwa ajili ya ujenzi wa vyoo, lakini kikwazo ni saruji, mabati na nondo kwa ajili ya kuanza ujenzi.
===================================================
Hassani Selemani Kaunje

Akikabidhi majokofu hayo leo hii Mh. Mbunge amewataka wachuuzi hao kutunza vitu hivyo kwani ni vyagharama na vitadumu kwa muda mrefu endapo wataviweka katika mazingira mazuri. Nao wanakikundi hicho cha akinamama wachuuzi wa samaki wameweza kupongeza hatua hiyo, wamemsifia kuwa ni mtu wa kutimiza ahadi kwani ametimiza kile alicho ahidi.
Hassani Kaunje
===================================================

===========================================================
Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida akisoma hotuba wakati wa halfa ya kusaini mikataba ya msaada kutoka kwa serikali ya Japan, halfa iliyofanyika kwa balozi jijini Dar es Salaam. Na Rabi Hume, Modewjiblog
Serikali ya Japan kupitia mfuko wake wa misaada wa Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects (GGHSP) imesaini mkataba wenye thamani ya Dola 204,300 sawa na Milioni 430 za Kitanzania kwa ajili ya kusaidia miradi mitatu ya kijamii.
Akisoma hotuba katika halfa ya kusaini mikataba hiyo ambapo Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Mhe. Edward Lowassa alikuwa mgeni rasmi, balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida alisema serikali ya Japan imetoa msaada huo kwa kutambua changamoto zilizopo katika sehemu ambazo wanatoa msaada huo na wanataraji utaleta mabadiliko.

Akizungumza na Mo Dewji Blog baada ya kusaini mikataba hiyo, mwakilishi wa Arusha Lutheran Medical Centre, Askofu Solomon Massangwa alisema msaada ambao umetolewa na serikali ya Japan utatumika kununua vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Alisema kwa mwaka 2014 kituo hiyo ilikuwa ikipokea hadi wagonjwa 9000 wa nje na imekuwa ikipokea hadi wagonjwa kutoka nje za nje kama Kenya na hivyo ununuzi wa vifaa hivyo vitasaidia kuwahudumia wagonjwa wanaofika katika kituo hicho cha afya wakiwa mahututi.
“Wametupatia msaada wa wa vifaa vya kwenye vyumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na tunawashukuru sana kwa msaada huo na tunaamini utasaidia kuokoa maisha ya wananchi wengi wanaofika kituoni kwetu kupata matibabu,” alisema Askofu Massangwa.
 Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida akiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi katika halfa hiyo, Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Edward Lowassa wakati kusaini mikataba ya miradi mitatu yenye thamani ya Dola 204,300 sawa Milioni 430 ya Kitanzania kwa ajili kusaidia Shule ya Kingolwira, Shule ya Muyuni na Kituo cha Afya cha Lutheran kilichopo Arusha. 
=====================================================
Kijana akijaribu kunusuru uhai wake kwa kupanda
By Jesse Mikofu, Mwananchi

Mwanza. Mama wa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mabatini, Janeth James (6), aliyekufa maji baada ya kusombwa na mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita, amesema anajuta kumpeleka mwanaye kuanza darasa la kwanza.

Mama huyo, Nyanchuga John mwenye watoto wawili alisema juzi kuwa asingempeleka shule mtoto wake asingesombwa na mafuriko na kufa maji.

“Najuta kwanini mwanangu tulikupeleka shuleni, bora tungekuacha uendelee kukaa nyumbani, kwani haya yote ya kusombwa na mafuriko yasingekupata, shule imenipotezea mtoto.

“Kifo chako kimeicha familia katika simanzi kubwa kwasababu ulikuwa mtoto wetu wa kwanza na umemuacha mdogo wako pekee yake.

“Mwanagu aliipenda shule, alikuwa na ndoto kubwa maishani mwake, lakini bora angeiacha shule machoni mwetu, umeniachia simanzi umeondoka kipenzi changu,” alisema Nyanchuga.

Baba wa marehemu, James Japheth alisema kifo ni mipango ya Mungu na hakuna anayeweza kuibadilisha.

Mwili wa Janeth ulizikwa juzi katika makaburi ya Kisesa baada ya kupatikana kwenye Mwalo wa Kirumba Ziwa Victoria ukielea.


Janeth alisombwa na mafuriko Januari 14, saa sita mchana baada ya kumponyoka baba yake katika daraja la Mabatini wakati akitoka kumfuata shuleni siku ya pili tangu aandikishwe darasa la kwanza.
=========================================================
Hayati Padri Calisti Nauli Nyambo

Hayati Padre Calisti Nauli Nyambo(pichani) ni mtoto wa tatu wa Familia ya hayati Baba Laurenti Ngasamiaku Nyambo na Mama Augustina Ngambakiha Msaki, alizaliwa tarehe 17/5/1939, katika Kijiji cha Kwamare Kirua Vunjo. Ndugu zake wa kuzaliwa ni Clementina, Martina, Beda, Damas, Adela, Eligi, Flora, Hilda, Domitila na Mary. Calisti alibatizwa na kupokea Sakramenti ya Ekaristi na Kipaimara katika Parokia ya Kirua.

ELIMU YA MSINGI

Mwaka 1948 hadi 1953 alisoma katika Shule ya Msingi Iwa hadi darasa la sita. Kwakuwa wakati ule shule ya msingi Iwa ilikua na darasa la kwanza hadi la sita tu, Calisti aliendelea na masomo ya darasa la saba kule milimaniUsambara mwaka 1954 katika shule ya Msingi Gare. Mwaka 1955 aliendelea na masome ya darasa la nane katika Shule ya Msingi Kichwele (au Uhuru) katika Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.

ELIMU YA SEKONDARI

Mwaka 1956-1957 Calisti aliendelea na masomo kidato cha kwanza na cha pili katika Shule ya Sekondari Umbwe.Alifuzu vizuri masomo yake akachaguliwa kujiunga na kidato cha tatu na cha nne katika Shule ya Sekondari yaPugu Dar es Salaam 1958 hadi 1959.

WITO WA UPADRE

Calisti aliongozwa na Roho Mtakatifu alijisikia kuitwa na kuvutwa na wito wa Upadre. Akaomba kujiunga na masomo ya Seminari kupitia Jimbo Katoliki Moshi. Mwaka 1960 hadi 1962 alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho.

Baada ya kuhitimu masomo ya Falsafa, aliamua kukatiza masomo na malezi ya Seminari. Akaajiriwa kufanya kazi Benki na Serikalini. Kutokana na nguvu ya wito wa Upadre fedha za mshahara hazikutosheleza dhamira na malengo ya maisha yake ya kupenda kumtumikia Mungu. Hivyo aliamua arudi Seminari kuendelea na safari yawito wa Upadre.

Akaomba kujiunga na Jimbo Kuu la Dar-es-Saam. Mwaka 1966 alipelekwa kusoma Teolojia katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo, Kipalapala Tabora. Mwaka 1969 alihitimu masomo na malezi ya seminari akapewa Ushemasi na mwaka huo huo tarehe 14 December 1969 akapewa sacramenti ya daraja la upadre na Mwadhama Cardinal Laurian Rugambwa na akawa padre wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

UTUME WA UPADRE

Kwa muda wa miaka tisa alifanya utume katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Alianza kama paroko msaidizi nabaadaye paroko katika parokia kadhaa za Jimbo Kuu la Dar es salaam. Tangu mwaka 1973 hadi 1976 aliteuliwa na Mwadhama Kardinali Rugambwa kuwa Vikari wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam. Kutoka Dar Es Salaam alifanya utume pia katika Jimbo Kuu la Arusha kwa muda mfupi kisha Mhashamu Askofu Denis wa Jimbo la Arusha akamtuma Marekani kwa masomo ya Chuo Kikuu.

MASOMO YA CHUO KIKUU

Mwaka 1978 alienda Marekani akasoma katika Chuo cha Majesuiti kilichoko Berkeley, California, akatunukiwa Master Degree ya Teolojia mwaka 1982. Alipenda bado kujiendeleza ndipo alipoenda katika Jiji la Washington DC akasoma katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Amerika (Catholic University of America) na akafuzu vizuri akatunukiwa Master of Arts Degree in Religious Education mwaka 1987.

UTUME NCHINI MAREKANI


Padre Nyambo alikuwa padre wa kwanza mwafrika kufanya kazi katika jimbo la St. Petersburg, Florida, Amerika. Alianza kwa kufanya utume wakati wa kiangazi (Summer holidays) katika parokia ya Mt. Joseph 1982 na Parokia ya Utatu Mtakatifu (Blessed Trinity) mwaka 1986-1987.

Askofu wa jimbo la St. Petersburg alifurahiwa na kuridhika na maisha na utendaji wa Padre Nyambo ndipo akampa utume kamili kama wakili paroko katika parokia moja katika jiji la Tampa, Florida mwaka 1988-1991. Wakati huo huo alikuwa Mkurugenzi wa jimbo wa utume wa Wakatoliki Waamerika Weusi katika jimbo la St. Petersburg.

Mwaka 1992-1993 alikuwa Paroko Kiongozi wa parokia ya Mt. Peter Claver Tampa. Kwa kuwa alifanya utume wake vizuri alipewa cheo cha Uparoko tangu mwaka 1993-1997.

Kwa muda wa miaka sita alikuwa Paroko katika Parokia ya Mt. Joseph St Petersburg, yaani, tangu mwaka 1997 hadi 2003. Mwaka huo huo wa 2003 alikuwa Paroko wa Parokia ya Watakatifu Wote (All Saints Parish) hadi mwaka 2013 alipostaafu kisheria.

Pamoja na majukumu ya uparoko na ya Kijimbo, Padre Nyambo alikuwa raisi wa utume wa Waamerika Weusi Wakatoliki katika Mkoa wa Florida.

Alikuwa pia Mjumbe katika Bodi ya Kitaifa ya Wakleri Waamerika Weusi. Padre Nyambo alikuwa pia ni Raisi Mwanzilishi wa Wakatoliki Wakleri Weusi na Umoja wa Mashirika ya Kidini Amerika. Alikuwa pia Mwakilishi wa Kitaifa wa Utume wa Walei Amerika, Mshauri wa Kitaifa wa Shirikisho la Kitume la Watanzania kule Amerika, Mjumbe wa Bodi katika Ofisi za Utume wa Kichungaji kwa Wahamiaji, Wakimbizi na Wasafiri.

Mwaka 2008 alitunukiwa tuzo ya heshima ya askofu mkuu Silvano Tomas kutokana na majitoleo na kazi nzuri kwa wahamiaji. Mwaka 2012 alitunukiwa tuzo ya mtumishi wa Kristu kutoka kwa Congress ya Kitaifa ya Wakatoliki Weusi wa Amerika.

WASIFU WA PADRE KALIST NYAMBO


Padre Kalist alikuwa mtu wa watu. Aliwapenda watu na hasa watu wa taifa lake. Alipenda na kuheshimu nyumbani alikozaliwa, alikokulia, kanisa alikobatizwa, kupata komunyo na kipaimara na shule Msingi ya Iwa alikosoma hadi darasa la sita. Ni miaka michache tu iliyopita alijenga vyumba vipya vya madarasa na vyoo katika shule ya Iwakama shukrani upendo kwa watu wa Kirua.

Alipenda na kutamani sana kuona maendeleo mazuri ya taifa letu. Alipenda kufadhili miradi ya maendeleo hususan elimu na afya. Watu wote waliomfahamu na kumtembelea kule Marekani watashuhudia alivyokuwa akishirikiana vizuri na watu wote na hasa watanzania aliowafahamu kule Marekani. Alikuwa mchapakazi na mwenye furaha kila wakati.

UGONJWA NA KIFO


Mwishoni mwa Mwaka jana, masaa machache kabla ya mwaka mpya Padre Calist Nyambo alishikwa na ugonjwa wa kiharusi akiwa nyumbani kwake akiwa anajiandaa kwenda kufanya Ibada kesho yake ambapo alipelekwa Hospitali kwa matibabu zaidi huko nchini Marekani lakini jitihada za Madaktari Bingwa za kuokoa uhai wake hazikuzaa matunda. Ilipofika tarehe 3 Januari, 2016 Mungu aliyempenda sana Padre Calist Nyambo alimwita kwake akamshikirishe furaha za Ufalme wake.

Ndugu wa marehemu na wanaukoo wote wa Nyambo wanatoa shukrani za kipekee kwa Uongozi wa Diocese ya St. Petersburg, Askofu Amani wa Moshi, Paroko, Watanzania wote wanaoishi USA pamoja na Madaktari kwa namna walivyoshiriki kwa hali na mali katika kufanikisha kuokoa maisha ya mpendwa wetu. Mungu awajalieni wingi wa Baraka na hasa afya ya roho na mwili. Asanteni sana. Taratibu za kuusafirisha Mwili wa Padre Calisti kutoka nchini Marekani kuja nchini Tanzania zinafanyika ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii katika Kanisa Katoliki Kirua Iwa, Diocese ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie. Ampumzike kwa amani. Amina.
=========================================================
Abou wa Houston. TX na mdhamini wa pendo lake.
==========================================================
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima (kulia) akisalimiana na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Zhang Biao wakati wawili hao walipokutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo Ofisini kwa Katibu Mkuu.
Balozi Mlima akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa China, Mhe. Zhang. Katika mazungumzo hayo, wawili hao waliahidi kuwa nchi zao zitaendelea kushirikiana na kuungana mkono katika masuala mbalimbali ya kimataifa. 
Maafisa kutoka Ubalozi wa China uliopo hapa nchini wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Mlima na Mhe. Zhang Biao (hawapo pichani). 
Balozi Mlima akimsikiliza Kaimu Balozi wa China, Mhe. Biao 
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakinukuu mambo muhimu yaliyojitokeza katika Mazungumzo kati ya Balozi Mlima na Mhe. Biao (hawapo pichani). 
Mazungumzo yakiendelea 

Picha na Reginald Philip
Mkurugenzi wa Fabak Fashions na mwandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asya Idarous Khamsin (katikati) akimtambulisha rasmi mwanadada, Wema Sepetu (kushoto) ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. (Kulia) ni Martin Kadinda ambaye naye miongoni mwa watendaji wanaoratibu jukwaa hilo la Lady in Red. katika usiku wa Lady In Red fashion show 2016, litakalofanyika 31 Januari ndani ya ukumbi wa Danken House wa Mikocheni jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Mkutano huo wa utambulisho wa jukwaa la Lady Inn Red fashion show 2016 kama inavyoonekana pichani.
Mwanadada Wema Sepetu akitoa nasaha zake kwa Wabunifu wa mavazi na wanamitindo (hawapo pichani) wakati wa utamburisho wa jukwaa la Lady In Red fashion show 2016 linalotarajiwa kufanyika 31 Januari.
Martin Kadinda akitoa nasaha zake kwa wabunifu na wanamitindo waliojitokeza katika mkutano huo (hawapo pichani) kuhusiana na jukwaa la Lady In Red fashion show 2016.
Wabunifu wa mavazi na wanamitindo wakifuatilia mkutano huo wa utambulisho wa jukwaa la Lady In Red fashion show 2016.
Baadhi ya wabunifu wa mavazi na mitindo wakifuatilia mkutano huo.
..Wakipata 'selfie' na Wema Sepetu
..Wakipata 'selfie' na Martin Kadinda
Picha ya pamoja...

Na Andrew Chale, Modewjiblog

Nyota wa filamu za Bongo, ambaye pia aliwai kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Wema Issac Sepetu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye onesho na jukwaa maalum la mitindo la kila mwaka la “Lady In Red 2016” litakalofanyika 31 Januari katika ukumbi wa Danken House uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Fabak Fashions na mwandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asya Idarous Khamsin amebainisha hilo alipokutana na badhi ya wabunifu wa mavazi na wanamitindo watakaopamba jukwaa hilo hiyo 31 Januari, ambapo amewataka kujipanga ilikuchangamkia fursa ya kupata kuinua tasnia ya mitindo nchini.

“Lady In Red fashion show 2016 ni ya kipekee na jukwaa hili ni fursa kwa kuinua wabunifu wa mavazi chipukizi kupata kuonekana zaidi na hata kukuza majina na ubunifu wao kujulikana ndani na nje” amefafanua Mama wa Mitindo, Asya Idarous.

Aidha, ameeleza kuwa, ilikutoa msisimko zaidi kwa jukwaa hilo. Mwanadada Wema Sepetu ndiye atakaye bariki siku hiyo ikiwemo utoaji wa vyeti kwa washiriki ilikuweka kumbukumbu.

Asya Idarous ameongeza kuwa, hadi sasa jukwaa hilo la Lady in red linafikia umri wa miaka 12 litaendelea kuwa juu zaidi na kuwa shule kwa tasnia ya mitindo ambapo kwa sasa pia linafanyika na nje ya Tanzania ikiwemo nchini Uingereza.

Hata hivyo wadau mbalimbali wameombwa kujitokeza kuliunga mkono ikiwemo kudhamini onesho hilo.





==================================================
================================================================
Hatua ya serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi kwa kuzuia wizara, taasisi na mashirika ya umma kukutana katika hoteli kwa shughuli mbalimbali za kikazi, imeanza kuleta athari chungu huku baadhi ya wamiliki wa hoteli wakisema wameathirika kimapato na sasa wako mbioni kupunguza wafanyakazi.

Kadhalika, baadhi ya wasomi wamesema licha ya dhamira nzuri ya serikali katika kuhakikisha inabana matumizi ili fedha zitakazopatikana zielekezwe katika miradi ya maendeleo, bado kuna haja ya kuangalia kwa umakini athari zake. Pia wameonya kuwa sekta ya hoteli ikiyumba itaathiri wajasiriamali wengi na sekta binafsi kwa ujumla.

Baada ya kuapishwa na kuingia madarakani Novemba 5, mwaka jana, Rais Dk. John Magufuli ilitangaza hatua kadhaa za kubana matumizi yasiyo ya lazima ili kuipa nguvu ya kuwatumikia wananchi.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni ni kupiga marufuku vikao vya kazi vya taasisi na mashirika ya umma kufanyika hotelini, kufanyika kwa hafla za kupongezana, kuadhimisha wiki mbalimbali zikiwamo za maji na Siku ya Ukimwi, warsha, semina, makongamano, mikutano na mafunzo.

Zingine ambazo sasa zinaelezwa kuathiri baadhi ya wajasiriamali na sekta binafsi ni pamoja na kufutwa kwa sherehe mbalimbali ikiwamo ya Uhuru, maadhimisho ya kitaifa na kimataifa yaliyokuwa yakiwalazimu wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi kutua Tanzania au kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa tangu kutolewa kwa agizo la serikali kuzuia hafla, vikao na shughuli za serikali kwenye kumbi za hoteli, karibu hoteli zote hazijapata mikutano wala shughuli yoyote kutoka kweye taasisi za umma, mashirika wala wizara.

CHAMA CHA WENYE HOTELI
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT), Latifa Sykes, alisema sekta ya hoteli ni moja ya maeneo yanayoajiri watu wengi kwa sababu ya kuangalia wageni na kushughulikia matukio mbalimbali, ikiwamo mikutano.

“Kitu kitakachotokea na ambacho kwa sasa kinatokea ni kwamba hoteli za mjini ambazo zilikuwa zikipokea mikutano mingi, sasa zitapunguza wafanyakazi,” alisema.

Alisema mbali na kupunguzwa kwa watu na pato la hoteli hizo kupungua, kutaathiri pia serikali kwa sababu ilikuwa ikipata kodi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya ongezeko la thamani (VAT).

“Lazima tuwe makini na tujue kila hatua ina matokeo yake. Kwenye hii ya kupunguza mikutano, matokeo yake ni kupungua kwa mapato yaliyokuwa yalipwe serikalini na hakuna tena sababu ya kuwa na wafanyakazi wengi.

“Tunamuunga mkono Rais kwenye kubana matumizi mabaya ya serikali lakini ni vyema akaangalia hatua za utekelezaji zisiathiri uchumi na biashara zinazosaidia ukusanyaji wa kodi,” alisema.

HALI HALISI
Ofisa Mauzo wa hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro Kempinsk), Godlove Mlaki, aliiambia Nipashe kuwa agizo la Rais Magufuli halijawaathiri sana kwa sababu hawategemei mikutano pekee ya serikali na taasisi zake kwa kuwa hoteli yao ni ya hadhi ya kimataifa.

Alisema athari ya moja kwa moja waliyopata kutokana na uamuzi wa serikali ni kukosa wateja ambao kwa kawaida huwapata wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru, Desemba 9 ya kila mwaka.

Wakati wa sherehe za kitaifa, ikiwamo Uhuru, wageni mbalimbali ambao hualikwa kutoka nje ya nchi wakiwamo na marais na wafanyabishara, hufika kwa wingi nchini na kusaidia kuingiza fedha za kigeni kutokana na kulala kwenye hoteli na huduma zingine wanazohitaji katika siku zote wanazokuwapo nchini.

Mlaki alisema kutofanyika kwa sherehe za Uhuru kuliwakosesha fedha nyingi kwa sababu awali hoteli yao ilikuwa ikipokea wageni kutoka nje waliokuwa wakialikwa kuhudhuria sherehe hizo.

Alisema hoteli hiyo yenye kumbi 10 za mikutano, wateja wake wakubwa walikuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na wastani wa mikutano waliyokuwa wakifanya kwa mwezi ilikuwa ikifikia 19.

Alisema kuna wakati walikuwa wakipata mikutano ya siku mbili hadi sita mfululizo kutoka serikalini.

“Toka mwaka jana Desemba hadi Januari hatujapata (kuandaa) mikutano yoyote kutoka serikalini,” alisema Mlaki.

Mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo, alisema mbali na wateja wananaotaka kumbi za mikutano, hata baadhi ya maaofisa wa serikali waliokuwa wakifika hapo ili kupata kifungua kinywa na chakula cha mchana, siku hizi hawapo tena.

Akifafanua juu ya ugeni wa marais waliokuwa wakifika kuhudhuria shehere za kitaifa, alisema: “Wakija marais wawili tu kwa mfano, ukiweka na walinzi wao, utakuta umeshafanya biashara ya zaidi ya vyumba 30, hapo hujaweka chakula na vinywaji. Kwa hiyo ile ni biashara kubwa sana kwetu,” alisema.

Katika hoteli ya Bahari Beach, Meneja anayehusika na kukodisha kumbi, Robert Vitus, alisema wameathirika kwa kiasi kikubwa kwa kuwa tangu kutolewa agizo la kuzuiwa kwa vikao na mikutano hotelini, hawajawahi kupata wateja kutoka serikalini.

Alisema hivi sasa wateja wanaowapata zaidi ni wale wanaotoka katika taasisi na kampuni binafsi pekee.

"Kwa ujumla, siku zote wateja wetu wakuu ni wale wanaotoka katika taasisi binafsi na wengine kutoka nje ya nchi. Watu wa serikalini kwa kiasi fulani walikuwa wateja wetu, japo si kama ilivyo kwa hawa wengine. Hivi sasa, hata hao asilimia ndogo ya wateja kutoka serikalini hatuwapati tena," aliongeza.

Meneja Masoko wa Hoteli ya Blue Pearl iliyoko Ubungo, Abdul Sheikh, alisema kutokana na serikali kuacha kufanya mikutano kwenye hoteli yao, baadhi ya wafanyakazi wamekosa kazi za kufanya.

“Yaani hakuna kabisa biashara siku hizi kulinganisha na ilivyokuwa awali ambapo kumbi zote zilikuwa zinajaa. Sasa hivi ni kama ulivyotukuta, hakuna kazi, kuanzia asubuhi hadi jioni, ni hivi hivi tu tunakaa” alisema Sheikh.

WASOMI WANENA
Mtafiti wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Haji Semboja, alisema ingawa hoteli kadhaa zitakuwa zimeingia katika msukosuko wa kiuchumi, bado kuna haja kwa serikali kuangalia ushirikiano mkubwa wa maendeleo baina ya sekta binafsi na ya umma katika kukuza pato la nchi.

Alisema kadri anavyoona, agizo la Rais Magufuli, moja kwa moja halikulenga kusitisha mikutano mikubwa yenye idadi ya watu zaidi ya 200 hadi 500, bali ile midogo ambayo haikuwa na ulazima wa kufanyika katika kumbi za hoteli kwa lengo la kuokoa rasilimali fedha ambayo inaweza kufanya jambo mbadala.

“Kuyumba kiuchumi kwa hoteli hizo huenda kumechangiwa na uelewa mdogo wa tabia za Waswahili, ambao wanajumuisha kila kitu na kusababisha hofu iliyochangia kuyumba kiuchumi kwa sekta binafsi ambayo ni miongoni mwa mihimili muhimu ya serikali hasa katika uchangiaji wa uchumi wa ndani,” alisema.

Mkurugenzi wa Sera wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Hussein Kamote, alisema katika nchi yoyote serikali ni muhimili wa kwanza wa ununuzi wa bidhaa na huduma, hivyo inavyobana sana matumizi yake itasababisha kuathirika kwa sekta mbalimbali na kusababisha uchumi mkuu kushindwa kukua.

“Kubana bajeti ni jambo la kawaida, ila ibane na kuachia ili kutoa ushirikiano mzuri kwa sababu inaweza kusababisha madhara kwa sekta iliyodhamiria kuibana. Tunajua inaweza kubana na fedha zile zikatumika katika sekta nyingine kama elimu au afya,” alisema Kamote.

Alisema ni vigumu hoteli nyingi kumudu kujiendesha bila kupata mteja muhimu ambaye ni serikali, hasa kwa sababu serikali imeanza kwenye eneo linalogusa sekta ya utalii ambayo ni kitovu kikubwa cha uchumi.

Alisema huenda ajira nyingi kwa wafanyakazi wa hoteli zikapungua huku wengi wasijue la kufanya na kujikuta wakiangukia katika kundi la wazururaji au shughuli haramu kama za utapeli.

IKULU YAFUNGUKA
Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, alisema kuyumba kiuchumi kwa hoteli nchini kutokana na agizo la Rais Magufuli si kazi ya serikali na wala agizo hilo haliwezi kubadilishwa.

Alisema Rais Magufuli alitoa agizo hilo kwa dhumuni la kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali na kuwataka Watanzania wote wapenda maendeleo wamuunge mkono katika suala hilo.

“Wizara zilikuwa zinatumia pesa nyingi sana kukodi kumbi kwa saa kadhaa wakati kuna kumbi katika wizara zao. Sasa kuyumba kiuchumi au kukosa wateja katika hoteli hiyo si kazi ya Ikulu,” alisema Msigwa.

Alisema hoteli zinapaswa kuwa wabunifu wa kupata fedha zaidi na si kutegemea wizara au taasisi kwenda kufanya mikutano katika hoteli zao.

Imeandaliwa na Gwamaka Alipipi, Fredy Azzah, Elizabeth Zaya na Efracia Massawe.
www.shaabanmpalule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment